Tofauti ya siku ya Wanawake na Siku ya Mama duniani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Kwa ufupi sana.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake inatambua mafanikio ya wanawake, bila kujali utaifa, kabila, dini, utamaduni, lugha, hali ya kiuchumi au mwelekeo wa kisiasa.
Screenshot_20240308_220330_Chrome.jpg

Siku hii pia huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake, ambayo kampeni ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia duniani kote. Japo Watanzania wanadhani usawa wa kijinsia ni kuwaletea viburi wanaume zao. Usawa unaongelewa ni wa kupiga kura, kufanya kazi, Mazingira sawa ya kazi, Wanawake wajitume kufanya kazi sio kusubiri kuletewa.

Nia yake ni kuwezesha uthabiti wa kiuchumi wa wanawake, ambako kunaweza kuwa ni hatua chanya kufikia juhudi za usawa.

Lakini Siku ya Mama ni sikukuu ya maadhimisho ya kuonyesha heshima na thamani ya akina mama katika familia kutokana na mchango na ushawishi wao mkubwa katika Jamii.

Ni siku ambayo inamkumbusha kila mmoja wajibu wake kwa mama yake. Kwa wale ambao mama zao wametangulia mbele za haki, huitumia siku hii kuiwaombea na kuwashukuru kwa kujitoa kwao kuwalea watoto wao.
Screenshot_20240308_215834_Google.jpg

Siku ya Mama ni siku ya kurudisha fadhira japo Kila siku ni siku ya mama duniani kwasababu ukubwa wa mama na umuhimu wa mama haitakiwi kumpa siku yake maalumu ya kumbukizi bali inatakiwa aenziwe kila siku
 
Maneno uliandika Hapa, umeandika maneno mazuri, Ila tambua kua Pesa ya Mwanamke Ni yake, na Pesa ya Mwanaume Ni ya Wote.... Usawa hakuna hapo.
 
Back
Top Bottom