Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Hizi ndio propaganda za ccm katika ubora wake. Tokea baada ya uchaguzi wa 2020, CHADEMA haikupeleka akaunti ambayo ingetumiwa kuwawekea fedha ya ruzuku, ambayo ni haki yao kikatiba na kwa mujibu wa sheria na kanuni. Kwa kupata zsidi ya 13% ya kura za urais tu, CHADEMA tayari wana kiasi kikubwa tu cha fedha stahili yao kama ruzuku. Lakini kwa kujali msimamo, wamekataa kuchukua hiyo ruzuku. Sasa huko CHADEMA kuna fedha ipi ambayo Mbowe anaitafuna? Maana alifungiwa akaunti zake binafsi, hakuna akaunti ya chama iliyoguswa. Ulichoandika ni umbeya wa bei ya chini kabisa.Kwanza mtu mwenyewe kwenye uongozi ameonekana kupwaya, akiwa amejikita kwenye kula pesa ya CHADEMA.
Kama kweli Mbowe angekuwa "amepwaya katika uongozi" basi wala asingeandamwa na serikali ya ccm. Anaandamwa kwa sababu yuko very effective katika kutekeleza malengo ya CHADEMA