Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 56,155
- 29,607
Mwandishi Wetu
Daily News; Tuesday,May 14, 2008
Wasanii zaidi ya 10 wanatarajia kupamba tamasha la kimataifa la kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa kwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zain inayotoa huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi kwa Afrika Mashariki na Kati, Dk. Saad Al Barrak alisema kuwa wasanii hao ni kutoka bara la Afrika na Ulaya.
Alisema tamasha hilo la siku tatu litaanza kufanyika Juni 27, London, Uingereza. Alitaja baadhi ya wasanii kuwa ni Papa Wemba , Suzanna Owiyo, Johnny Clegg, Sipho Mabuze Loyiso, Kwaya ya Injili ya Soweto, rapa wa Sudan, Emmanuel Jal, Queen & Paul Rodgers, Annie Lennox, Simple Minds, Leona Lewis, the Sugababes, Dame Shirley Bassey, Razorlight, Andrea na Sharon Corr, Eddy Grant, na Jamelia.
Al Barrak alisema kuwa tamasha hilo litakwenda sambamba na hatua ya kampuni yake ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo kuchangisha fedha kwa ajili ya kazi za hisani. Alisema: Tunaona fahari kuwa sehemu ya tukio hili la heshima kwa Mandela, aliyejitoa kwa ajili ya watu wa Afrika. Al Barrak alisema fedha zitakazochangwa katika hafla hiyo, zitatolewa kwa Mfuko wa Nelson Mandela ili zitumike kwa kazi mbalimbali za hisani ya jamii.
Pia Zain inafanya mipango kuhakikisha watu wa Afrika wanashuhudia tukio hilo. "Ni sehemu ya malengo ya Zain ya kujenga na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa jamii, na tunafurahi kushiriki katika kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Mandela, alisema Dk. Al Barrak. Aidha, Al Barrak alisema tamasha hilo litahudhuriwa pia na aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton, Waziri Mkuu Gordon Brown wa Uingereza wakati wengine ni msanii Will Smith na Oprah Winfrey.