Kana-Ka-Nsungu
JF-Expert Member
- Oct 4, 2007
- 2,257
- 353
Siku kadhaa zilizopita kulikuwa na tangazo kwenye website ya Michuzi likitujulisha kwamba Lady Jay Dee alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki wachache kutoka bara la Afrika ambao wangetumbuiza kwenye tamasha la Birthday ya Mandela. Nilibahatika kuona highlights za hiyo concerts lakini sikuona mtu anayefanana na Jide na baada ya kupitia list ya wanamuziki walikuwa wa perfom sikuliona jina lake. Sasa najiuliza aliperform au hakuperform? na kama hakushiriki kwa nini Michuzi alieneza hizi habari za uongo na hadi leo hajazikanusha au kueleza nini kilitokea? Nia hasa ilikua ni nini?