Jeshi la Israel lavamia Studio za Al jazeera wakiwa live

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,591
Reaction score
17,561
Vikosi vya Israel vimevamia ofisi za shirika la utangazaji la Al Jazeera huko Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuamuru kufungwa kwa muda wa siku 45.

Wanajeshi wa Israel wenye silaha na waliojifunika nyuso zao waliingia ndani ya jengo hilo mapema Jumapili wakati wa matangazo ya moja kwa moja.

Watazamaji walitazama wanajeshi wakitoa agizo la kufungwa kwa mkuu wa ofisi hiyo katika Ukingo wa Magharibi Walid al-Omari ambaye aliisoma moja kwa moja ujumbe huo hewani.

Israel ilivamia ofisi za Al Jazeera huko Nazareth na Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu mwezi Mei baada ya kulielezea shirika hilo la utangazaji lenye makao yake Qatar kuwa tishio kwa usalama wa taifa.

"Kulenga waandishi wa habari kwa njia hii kila mara kunalenga kufuta ukweli na kuzuia watu kusikia ukweli," Omari alisema katika maoni yaliyoripotiwa na mwajiri wake.

Wanajeshi hao walichukua maikrofoni na kamera ya mwisho nje ya barabara ya ofisi hizo na kumlazimisha Omari kutoka nje ya ofisi, mwandishi wa habari wa Al Jazeera Mohammad Alsaafin alisema.

Akichapisha kuhusu uvamizi huo kwenye mitandao ya kijamii, Alsaafin alisema wanajeshi hao pia waling'oa bango la Shireen Abu Aqla - ripota wa Al Jazeera ambaye aliuawa wakati akiripoti uvamizi wa vikosi vya Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Aljazeera na mashuhuda wa wakati huo walisema mwandishi huyo wa habari Mpalestina mwenye uraia wa Marekani alipigwa risasi na wanajeshi wa Israel. Hapo awali Israel ilidai kuwa alipigwa risasi na Mpalestina, hata hivyo miezi kadhaa baadaye ilihitimisha kuwa kulikuwa na "uwezekano mkubwa" kwamba mmoja wa askari wake alimuua.
20240922_105143.jpg
 
Wale wanaopiga kelele za demokrasia ndio waendelee kujifunza hapa
 
Vikosi vya Israel vimevamia ofisi za shirika la utangazaji la Al Jazeera huko Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuamuru kufungwa kwa muda wa siku 45.

Wanajeshi wa Israel wenye silaha na waliojifunika nyuso zao waliingia ndani ya jengo hilo mapema Jumapili wakati wa matangazo ya moja kwa moja.

Watazamaji walitazama wanajeshi wakitoa agizo la kufungwa kwa mkuu wa ofisi hiyo katika Ukingo wa Magharibi Walid al-Omari ambaye aliisoma moja kwa moja ujumbe huo hewani.

Israel ilivamia ofisi za Al Jazeera huko Nazareth na Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu mwezi Mei baada ya kulielezea shirika hilo la utangazaji lenye makao yake Qatar kuwa tishio kwa usalama wa taifa.

"Kulenga waandishi wa habari kwa njia hii kila mara kunalenga kufuta ukweli na kuzuia watu kusikia ukweli," Omari alisema katika maoni yaliyoripotiwa na mwajiri wake.

Wanajeshi hao walichukua maikrofoni na kamera ya mwisho nje ya barabara ya ofisi hizo na kumlazimisha Omari kutoka nje ya ofisi, mwandishi wa habari wa Al Jazeera Mohammad Alsaafin alisema.

Akichapisha kuhusu uvamizi huo kwenye mitandao ya kijamii, Alsaafin alisema wanajeshi hao pia waling'oa bango la Shireen Abu Aqla - ripota wa Al Jazeera ambaye aliuawa wakati akiripoti uvamizi wa vikosi vya Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Aljazeera na mashuhuda wa wakati huo walisema mwandishi huyo wa habari Mpalestina mwenye uraia wa Marekani alipigwa risasi na wanajeshi wa Israel. Hapo awali Israel ilidai kuwa alipigwa risasi na Mpalestina, hata hivyo miezi kadhaa baadaye ilihitimisha kuwa kulikuwa na "uwezekano mkubwa" kwamba mmoja wa askari wake alimuua.View attachment 3102932

Kuna kweli (Fact) na ukweli (the truth) Sasa ukweli wakati mwingine hujengwa juu ya nadharia za kweli za kilimani.
We unamaoni gani kati ya habari ya moja kwa moja (live) na habari iliyoratibiwa (taarifa) ipi ni fact na ipi ni the truth!?
 
Israel iko sahihi sana kufunga hiko kituo. Hakuna habari mule zaidi ya propaganda in favor of terrorists.
Hicho kituo ukifuatilia habari zake wako full biased kuhusu Israel mpaka watangazaji wake yaani kuna yule analyst wao anaitwa Marwan Bishara jamaa siku Israel ikitoaga kipondo akihojiwa utamuona usoni jinsi alivyoumia yaan full uchungu sasa ngoja rockets za magaidi zirushwe Israel utamuona likiongea kwa furaha kweli kweli
 
Israel iko sahihi sana kufunga hiko kituo. Hakuna habari mule zaidi ya propaganda in favor of terrorists.
Hamna lolote.
Kama ingekua ni propaganda basi Al-Jazeera isingepokea tuzo ya Chombo bora cha habari duniani iliyoandaliwa na Mmarekani New York Times.
Msiropoke tu ninyi jamaa.
Israel inaficha ukweli kuhusu hali ya wanajeshi wake.
 
Vikosi vya Israel vimevamia ofisi za shirika la utangazaji la Al Jazeera huko Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuamuru kufungwa kwa muda wa siku 45.

Wanajeshi wa Israel wenye silaha na waliojifunika nyuso zao waliingia ndani ya jengo hilo mapema Jumapili wakati wa matangazo ya moja kwa moja.

Watazamaji walitazama wanajeshi wakitoa agizo la kufungwa kwa mkuu wa ofisi hiyo katika Ukingo wa Magharibi Walid al-Omari ambaye aliisoma moja kwa moja ujumbe huo hewani.

Israel ilivamia ofisi za Al Jazeera huko Nazareth na Jerusalem Mashariki inayokaliwa kwa mabavu mwezi Mei baada ya kulielezea shirika hilo la utangazaji lenye makao yake Qatar kuwa tishio kwa usalama wa taifa.

"Kulenga waandishi wa habari kwa njia hii kila mara kunalenga kufuta ukweli na kuzuia watu kusikia ukweli," Omari alisema katika maoni yaliyoripotiwa na mwajiri wake.

Wanajeshi hao walichukua maikrofoni na kamera ya mwisho nje ya barabara ya ofisi hizo na kumlazimisha Omari kutoka nje ya ofisi, mwandishi wa habari wa Al Jazeera Mohammad Alsaafin alisema.

Akichapisha kuhusu uvamizi huo kwenye mitandao ya kijamii, Alsaafin alisema wanajeshi hao pia waling'oa bango la Shireen Abu Aqla - ripota wa Al Jazeera ambaye aliuawa wakati akiripoti uvamizi wa vikosi vya Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Aljazeera na mashuhuda wa wakati huo walisema mwandishi huyo wa habari Mpalestina mwenye uraia wa Marekani alipigwa risasi na wanajeshi wa Israel. Hapo awali Israel ilidai kuwa alipigwa risasi na Mpalestina, hata hivyo miezi kadhaa baadaye ilihitimisha kuwa kulikuwa na "uwezekano mkubwa" kwamba mmoja wa askari wake alimuua.View attachment 3102932
Kilikuwa ni kituo cha propaganda cha magaidi kwa hiyo israel wapo sahihi kukifunga
 
Back
Top Bottom