Hapo mwanzo mtu alimuumba Mungu kwa mfano wake

Hapo mwanzo mtu alimuumba Mungu kwa mfano wake

Wasioamini Uwepo wa Mungu,hawana utofauti na wanaoamini uwepo wa Mungu,inatakiwa wajitofautishe na wanaoamini uwepo wa Mungu.
1.Ikiwa wanaomini uwepo wa Mungu wanaoa na kuolewa,wasioamini uwepo wa Mungu wasioe wala kuolewa.
2.Wanaoamini uwepo wa Mungu,wanatafuta elimu kwa watoto wao,wasioamini uwepo wa Mungu,wasitafutw elimu kwa watoto wao.
3.Wanaoamini uwepo wa Mungu wanavaa nguo,wasioamini wasivae nguo
4.Wasioamini uwepo wa Mungu,wawe kinyume kwa kila analofanya anayeamini uwepo wa Mungu,kwa maana wanaomini uwepo wa Mungu wanafuata maamrisho ya Mungu,kupitia vitabu wanavyoamini ni vya Mungu.Kwa hiyo asiyeamini uwepo wa Mungu akifanya kama anavyofanya anayeamini uwepo wa Mungu,atakuwa na yeye anamuamini Mungu kivitendo,huku anasema kimaneno haamini uwepo wa Mungu.
Nikikuita kilaza ama kihiyo nitakuwa nimekukweza sana.........nasubiri lipatikane neno sahihi nikuite kwalo.
 
Mungu yupo Na usipokiri dhambi hii itakuandama,fikiria binadamu tumetokea wapi Na mwisho wetu ni upi
 
Utakapolala kitandani, haja ndogo na kubwa zote unamalizia hapo,mwili umepooza na huwezi kutumia vidole vyako kuandika upuuzi kama huu ulioandika leo,ndipo utakapojua kama Mungu yupo au la.
kwa kumuona au kwa kusikia sauti yake au kwa kuamini kama ilivyo desturi
 
Sasa kama uwezo wetu wa kumjua Mungu ni mdogo, ilikuwaje watu wanafahamu sheria, sifa pamoja na mapenzi ya Mungu?
Kama hujui maana ya tafiti itakuwa ngumu kukuelezea.........lakini kama vitabu vya dini vingekuwa na tafiti basi Mungu angechunguzika bila shida.
Sifa, sheria na mapenzi ya Mungu ni vitu vichache tunavyovijua wanadamu kuhusu Mungu.
Nataka kujua tafsiri yako kwa neno tafiti. Mfano vitabu vinavyounda biblia ni secondary source ya data. Na je hujui kuwa vitabu vya matukio mengi vinavyounda bible ni sehemu ya tafiti za kuprove uwepo wa Mungu? Na je hujui kuwa wanadamu (respondents) mathalani mitume waliotumwa na kumshuhudia Mungu na matendo yake ni primary data za kuelezea uwepo wa Mungu? Leo nikienda kufanya historical research Middle East kuyajua matendo ya Mussa kutumiwa na Mungu hadi kutengeneza njia katikati ya bahari watu wakapita na askari wa farao wakapigwa na moto Je utanishauri nitumie njia gani ya kupata data kama siyo written records and archives za utawala wa farao na wayahudi? Na nikiprove hayo ni mwanasayansi gani atanieleza hizo natural forces ni zipi?
 
Mungu yupo Na usipokiri dhambi hii itakuandama,fikiria binadamu tumetokea wapi Na mwisho wetu ni upi
Ndo maana nimesema mtu ali imagine uwepo wa kitu chenye uwezo zaidi yake ili kiwe kielelezo cha mambo yasiyoeleweka.

Swala la chanzo cha wa au nini kinafuata baada ya kifo, hakuna anayejua.

Kwa kutokujua huko, ndio watu waka imagine uwepo wa Mungu atakayejua yote.
 
Mtoa mada kuna vitu vyakutolea stress za Anko magu JF ila cyo MUNGU,
Nikupe siri MUNGU(supernatural being) hadhihakiwi at a siku moja, hii thread inafanyiwa kaz unless utubu
unaelewa maana ya dhihaka?
 
Sifa, sheria na mapenzi ya Mungu ni vitu vichache tunavyovijua wanadamu kuhusu Mungu.
Nataka kujua tafsiri yako kwa neno tafiti. Mfano vitabu vinavyounda biblia ni secondary source ya data. Na je hujui kuwa vitabu vya matukio mengi vinavyounda bible ni sehemu ya tafiti za kuprove uwepo wa Mungu? Na je hujui kuwa wanadamu (respondents) mathalani mitume waliotumwa na kumshuhudia Mungu na matendo yake ni primary data za kuelezea uwepo wa Mungu? Leo nikienda kufanya historical research Middle East kuyajua matendo ya Mussa kutumiwa na Mungu hadi kutengeneza njia katikati ya bahari watu wakapita na askari wa farao wakapigwa na moto Je utanishauri nitumie njia gani ya kupata data kama siyo written records and archives za utawala wa farao na wayahudi? Na nikiprove hayo ni mwanasayansi gani atanieleza hizo natural forces ni zipi?
Kwanini Mungu ajitambulishe kwa watu wake indirect kwa kutumia mitume?

Kwanini mitume na manabii wote ni watu wa middle east?

Je kama hao watu waliabudu mizimu yao sisi tutajuaje?
 
Mtu alimuumba Mungu katika fikra zake ili awe kielelezo cha mambo yote yaliyokosa majibu kwa upeo wa watu.
Mungu alipewa sifa zote za kiutu kama vile huruma, chuki, upendo, ukatili, hasira, wivu, majuto, ushindani n.k.
Kutokana na sifa ya ushindani kuwa ni kipimo cha nguvu za Mungu, mtu alimuumbia Mungu mshindani, naye ameitwa Shetani.Mtu akajijengea imani kuwa matendo yote anayoyatenda anongozwa na Mungu iwapo ni mema au na Shetani iwapo ni mabaya.

Mungu na Shetani sii vitu halisi bali ni 'Idea' za watu.Mungu na Shetani hawajawahi kuonekana, kusikika, kuhisika, ama kushikika popote.
Idea ya uwepo wa Mungu imekuwa ikirithishwa kwa watu [Theists] wakiwa kwenye umri mdogo zaidi na kwa vitisho vya ya kwamba kama wasipomwamini Mungu basi wataishi maisha ya tabu pamoja na kuingia kwenye moto wa milele watakapokufa[Hakuna uthibitisho hata chembe wa kuwepo kwa hivyo vitisho].

Kutokana na watu mbalimbali kujitengenezea picha tofauti kwenye fikra zao juu ya Mungu, yameibuka makundi mbalimbali ya watu wenye mitazamo tofauti juu ya sifa za Mungu, sheria zake pamoja na mapenzi yake kwa watu. Makundi hayo ni dini na madhehebu yasiyo na idadi yanayodai kumwamini Mungu mmoja lakini jambo la kushangaza huyo Mungu ana waongoza watu kwa utofauti mkubwa sana.Hizo dini na madhehebu yake zimekuwa zikihubiri sifa chanya za Mungu na hasi za Shetani ambazo haziendani na uhalisia.

Idea ya uwepo wa Mungu na Shetani imekuwa ikiaminishwa kwa watu badala ya kueleweshwa hivyo kukosekana kwa ushahidi juu ya kuwepo kwa Mungu pamoja na mpinzani wake Shetani.
Pindi mahojiano juu ya uwepo wa Mungu yanapoibuka, Mungu hutetewa na watu badala ya kujitetea mwenyewe.

Mungu na Shetani sii halisi[kweli] bali ni fikra za watu ambazo hazina uhalisia wowote.
Nje ya fikra za watu hakuna Mungu wala Shetani..........Hapo mwanzo mtu alimuumba Mungu kwa mfano wake.
Labda nikuulize kitu.kabla ya wewe kuja duniani ulikuwa wapi?
 
Wasioamini uwepo wa Mungu,hawajiamini kauli yao ya kutokuwepo kwa Mungu,kwa maana ili hoja yao ya kutokuwapo Mungu,haina nguvu mpaka wamtaje Mungu.
kumtaja lowasa hakumaanishi kumwamini fikiria vizuri hapo,
ukizingatia ni jina lipo dahari
 
Nothing called God exists!

God is an imaginary imagination depending on the imaginator!
My husband can be better than that God
Cause my hub exist, but God doesnt

John 3:18-19
"He who believes in Him is not judged; he who does not believe has been judged already, because he has not believed in the name of the only begotten Son of God. "This is the judgment, that the Light has come into the world, and men loved the darkness rather than the Light, for their deeds were evil.
 
Kwanini Mungu ajitambulishe kwa watu wake indirect kwa kutumia mitume?

Kwanini mitume na manabii wote ni watu wa middle east?

Je kama hao watu waliabudu mizimu yao sisi tutajuaje?
Ulitaka ajitambulishe vipi kwa watu wake? Hata sisi wanadamu tukipewa utawala kila mtu atatumia akili zake ingawa tunabanwa na katiba sasa Mungu hacccccccccccccccccccna Latina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom