Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,608
- 12,818
Mtu alimuumba Mungu katika fikra zake ili awe kielelezo cha mambo yote yaliyokosa majibu kwa upeo wa watu.
Mungu alipewa sifa zote za kiutu kama vile huruma, chuki, upendo, ukatili, hasira, wivu, majuto, ushindani n.k.
Kutokana na sifa ya ushindani kuwa ni kipimo cha nguvu za Mungu, mtu alimuumbia Mungu mshindani, naye ameitwa Shetani.Mtu akajijengea imani kuwa matendo yote anayoyatenda anongozwa na Mungu iwapo ni mema au na Shetani iwapo ni mabaya.
Mungu na Shetani sii vitu halisi bali ni 'Idea' za watu.Mungu na Shetani hawajawahi kuonekana, kusikika, kuhisika, ama kushikika popote.
Idea ya uwepo wa Mungu imekuwa ikirithishwa kwa watu [Theists] wakiwa kwenye umri mdogo zaidi na kwa vitisho vya ya kwamba kama wasipomwamini Mungu basi wataishi maisha ya tabu pamoja na kuingia kwenye moto wa milele watakapokufa[Hakuna uthibitisho hata chembe wa kuwepo kwa hivyo vitisho].
Kutokana na watu mbalimbali kujitengenezea picha tofauti kwenye fikra zao juu ya Mungu, yameibuka makundi mbalimbali ya watu wenye mitazamo tofauti juu ya sifa za Mungu, sheria zake pamoja na mapenzi yake kwa watu. Makundi hayo ni dini na madhehebu yasiyo na idadi yanayodai kumwamini Mungu mmoja lakini jambo la kushangaza huyo Mungu ana waongoza watu kwa utofauti mkubwa sana.Hizo dini na madhehebu yake zimekuwa zikihubiri sifa chanya za Mungu na hasi za Shetani ambazo haziendani na uhalisia.
Idea ya uwepo wa Mungu na Shetani imekuwa ikiaminishwa kwa watu badala ya kueleweshwa hivyo kukosekana kwa ushahidi juu ya kuwepo kwa Mungu pamoja na mpinzani wake Shetani.
Pindi mahojiano juu ya uwepo wa Mungu yanapoibuka, Mungu hutetewa na watu badala ya kujitetea mwenyewe.
Mungu na Shetani sii halisi[kweli] bali ni fikra za watu ambazo hazina uhalisia wowote.
Nje ya fikra za watu hakuna Mungu wala Shetani..........Hapo mwanzo mtu alimuumba Mungu kwa mfano wake.