Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,325
- 11,193
Master Sergeant Gal Meir Eisenkot, mwenye umri wa miaka 25 ameuliwa na wapiganaji wa Hamas hapo jana kaskazini ya Gaza.
Gal ni mtoto wa Gadi Einsenkot ambaye ni mmoja wa mawaziri wa baraza la vita la kupambana na Hamas linaloongozwa na waziri mkuu Benjamini Netanyahu.
Maumivu kutokana na habari za kifo cha mtoto wake huko Gaza waziri Gadi alizipata akiwa kwenye chumba cha kuongozea vita huko Israel.
Taarifa za kuongezeka kwa vifo vya maafisa wa juu wa jeshi la IDF zinakuja wakati ambapo jeshi hilo limetoa indhari kuwa vita vimekuwa vikali zaidi mara baada ya kumalizika usitishaji wa muda mfupi uliofanyika mwishoni mwa mwezi ulipitata mwezi uliopita.
Malalamiko hayo ya Israel yanakwenda sambamba na ahadi ya ushindi iliyotolewa na kiongozi wa Hamas hapo tarehe 6 kuadhimisha miezi miwili ya vita na sambamba na Marekani kulalamika juu ya kushambuliwa kwa kambi zake za jeshi nchini Iraq na Syria.
Kutokana na kile anachokiona katibu mkuu wa UN ametumia rungu lake la kanuni ya 99 ya jumuiya hiyo kutoa tahadhari kuwa vita vya Gaz bila kusitishwa haraka kuna uwezekano mkubwa kuwa vita eneo lote la mashariki ya kati.
Yahoo News