Hamas walimkuta Joshua amevaa bulletproof

Hulijui jeshi la israel na pia hujui maana ya siri za kijeshi. Mwanajeshi anapoitwa kwenda kwenye operation yoyote, hiyo already ni siri ya kijeshi ambayo inaweza kwenda kwa walengwa wa operation hiyo na kuivuruga. Mnapoambiwa siri za kijeshi wengi wenu hukimbilia kudhani kuwa ni mambo mepesi mepesi kama zilipo kambi za jeshi na silah zao badala ya kujua kuwa siri ni yale mambo ambayo askari anajua kuhus daily operations za kijeshi.

Huwezi kuingia jeshi la israeli kirahisi trahisi kama ilivyo kwa nchi kama marekani.
 
Ukisikia mtu anasema, kifo cha mtanzania mwenzetu, ujuwe huyo mnafiki muogope kama ukoma...
Kabisa mkuu...yan watu wa Hivi wana unafiki wa hali ya juu,hv kma ni kweli jamaa alikuwa anatumikia jeshi la wazayuni hv atakuwa ameuA waoalestina wangapi? Hv wale palestines ni mawe?
Watu wamekaza tu "mtanzania mwenzetu" unafiki mkubwa
 
Alikuwa mpiganaji ambaye hana mafunzo.

Tunatamani kujua mengi zaidi pia.
 
Haha foolish mwenyewe na pia hamna wa kuniamulia kitu humu J. F na kamwe hatatokea
Have a nice day you brother
 
Sasa kitakachokukuta huko usilaumu,ni Ajali kazini
we jamaa ni mjuvi wa mambo nyeti, unajua tuna ushirikiano wa ulinzi na usala na israel? Kwa kuwa wame advance kimedani tukipeleka vijana wetu wakafundishwe huko kuna ubaya? Unaenda mafunzoni mara unakutana na kitu halisi ulichoenda kujifunza itabidi uingie mzigoni kufa na kupona. Je kama alikuwa anajifunza ukomando?
 
Israel ni role model wa medani duniani, hiyo ndiyo nchi ya kupeleka vijana kwa wingi kupata mafunzo ya kijeshi/kikomando huko
 
Unavyoniambia silijui jeshi la Isael kama vile wewe peke yako ndo unalijua kumbe unaleta stori za vijiweni mwisho wake ndo huu
 
Sakala la Joshua Molel kuuawa na HAMAS lilileta mfadhahiko na tafrani kwenye jamii.

Binafsi niliona taarifa zake kuna walakini kwani Joshua tulitangaziwa na mwenzie mmoja kua walitekwa na HAMAS mnamo tarehe 7 October ila video ya mauaji ya Molel ilikuja kuachiwa mwezi December baada ya balozi wa Palestine kuanza kuelezea baadhi ya mambo kwenye media (haswa clouds tv)

Serikali ilijitokeza na kusema familia ya Molel itasafirishwa kwenda Israel kwa ajili ya taarifa zaidi,well jambo jema familia kusafirishwa kwa ajili ya briefing ila kwa mtu anaeweza kuwaza mbali inatosha kuleta maswali kua kuna taarifa zaidi za ndani haziko wazi na binafsi ilipelekea kuandika andiko hili, Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

Baba mzazi wa Molel amerejea kutoka Israel na kwenye mahojiano na vyombo vya habari ameeleza bayana kua mwanae alikua amevaa bullet proof na aliuawa pamoja na askari watano wa Israel walipokuja sehemu moja. Hizo ni taarifa za mzazi ambae ametoka Israel kukutana na jeshi la Israel.

Watanzania wengi wamesahau kabisa kua bado Molel iliripotiwa alikua na Mtanzania mwenzie walipotekwa na HAMAS,mbona hadi leo hatutajiwi jina lake?!! Hali yake ikoje?!! Nae alikamatwa akiwa kavaa bullet proof ama akiwa chuoni?!!.

Tumsikilize Mzee Molel mwenyewe.

View: https://www.instagram.com/reel/C1crB_6KGs0/?igsh=MzRlODBiNWFlZA==
 
Kuliko kupeleka vijana congo na afrika ya kati si bora kupeleka vijana huko israel na urusi/ukraine wakaive kimedani? Kufa kupo kila mtu atakufa
 
Aliuawa na wenzie ila video ndio kwanza inaonyesha yupo barabara na pale ndio wanaanza kumpiga ...Kiufupi ndugu yetu Mtanzania kauliwa ila maelezo ya mzee na video ni vitu tofauti kabisa.

Tukubali amekufa kuchambua hakuna maana kwa vile naona uongo ni mwingi, huyu mzee kapewa story ila haiendani na clip iliyosambaa mwanzoni.

Wanasema kauliwa ila taarifa za awali walisema katekwa yeye na mwenzie.
 
Ninavyojua mimi ni kuwa Israel nyumba nyingi hasa zile zilizo karibu na Gaza zina vyumba vinavyoitwa ''safe room'' kwa ajili ya kujificha wakati wa mashambulizi na ndani ya hivyo vyumba kuna vifaa vya kujikinga na mashambulizi kama bullet proof.
 
Unavyoniambia silijui jeshi la Isael kama vile wewe peke yako ndo unalijua kumbe unaleta stori za vijiweni mwisho wake ndo huu
Wewe huna background ya kijeshi ndiyo maana unachukulia neno siri za kijeshi kirahisi sana. Halafu pia hujui mfumo wa jeshi la Israel ambalo kubwa ni jeshi la akiba kwa hiyo unadhani wanawaweza wakachukua mtu yeyote kuhudumu jeshini. Ugaidi unaoizunguka Israel miaka yote tangu taifa hilo liunde umewafanya wawe makini sana katika security system yao. Kama huamini na unadhani hayo ni mambo ya kijiweni hilo siyo tatizo lakini usitake kuwa mmoja wa wanaotaka kumchafua marehemu kuwa alikuwa mwanajeshi wa israel hivyo alikuwa na haki kuuwawa na hamas kama combatant.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…