Mabibi na mabwana kama nchi tumepwelewa sana katika hili la maridhiano. Kwa hakika matatizo yetu kama nchi yako hapo na ndiyo maana tuko hapa tulipo na sasa kama mazuzu tu.
Mbowe ameonyesha kwa vitendo kuwa kinachohitajika katika migogoro ukiwamo huu ni maridhiano. Jibu la Bi. Halima kwenye hili kuwa wapo tayari "kuyajenga" mbona ni la kupongezwa mno?
Ikumbukwe pana wenye kupenda kuukaanga mbuyu vilivyo ili kuwaachia wenye meno kutafuna.
Hebu wasipewe nafasi hao. Wakaanga mbuyu na wakajifunze kwa vitendo.
Kwa maneno ya bi Tshala Mwana, "bibi na bwana wakigombana nyumbani waache wataelewana wenyewe. Ukiyaingilia utabaki na aibu"
Muda wa kuwafahamisha wasiohusika bila ya kujali vyeo vyao au vyama vyao - kuufyata! Ipewe sasa nafasi ya hoja kutamalaki katika mazingira yenye kufaa. Kusamehe 7x70 ni sehemu ya maisha ya binadamu wenye utu. Wanasema waungwana, "we can live and let live!"
Nini taabu kama maridhiano yakatufikisha kwenye:
1. Kuwajua waasisi wa ghushi?
2. Kuwashugulikia waasisi wa ghushi?
3. Kuwaumbua waasisi wa ghushi?
4. Kuwapa funzo la kudumu waasisi wa ghushi?
5. Kuufunga mjadala wa ghushi hii katika namna inayokubalika?
Kamanda Mbowe na makamanda wote kwa kauli ya bi dada leo, kukaa nao rasmi au hata kivinginevyo lengo kuyajenga itakuwa ni sahihi sana. Ikumbukwe kuwa kuhitajika kuyajenga kwanza kabla ya mengine limo kwenye sehemu ya hukumu.
Walionyeshwa mlango wa kutokea ila haukupigwa kufuli. Bi Halima hakukunja ngumi. Kwa hekima amenyoosha mkono. Ni busara kuupokea.
Kwa maneno ya Jabali la Muziki: "Tukamsake mbaya wetu anaye tuchonganisha." Siku tukimpata zikawe zetu ama zake!
Mungu ibariki CHADEMA.