Halima umeonesha mwanzo mzuri, maridhiano

Halima umeonesha mwanzo mzuri, maridhiano

Hivi hawa 19 watakuwa tayari kama sharti kuu la kuyajenga ni Halima na wenzie kuachia Ubunge kwanza na kurudi chamani kama wanachama wa kawaida bila nafasi yoyote ya uongozi harafu CHADEMA kipeleke akina mama wengine 19 bungeni?

Come to think of it, most likely dhahama hii ilianza chini kwa chini pale lilipokuja suala la nani na nani wateuliwe kwenda Bungeni

Yote yanawezekana chini ya jua. Nakazia tuwape muda makamanda wetu wanapoyaweka maslahi ya chama mbele.

Kinachotakikana mbona kinajulikana?
 
Machungu ya CHADEMA yeyote kwenye hili yanajulikana.

Hata hivyo kama nia ya kuweka mambo sawa ipo. Haipo shaka kamanda Mbowe, Lissu na wote wanaohesabika wanaweza kuweka kila kitu sawa tukafika hapa kwenye kuwajua wabaya wetu. Yaani:

1. Kuwajua waasisi wa ghushi.
2. Kuwashugulikia waasisi wa ghushi.
3. Kuwaumbua waasisi wa ghushi.
4. Kuwapa funzo la kudumu waasisi wa ghushi.
5. Kuufunga mjadala wa ghushi hii katika namna inayokubalika.

Bottom line ya requirements za chama ziko wazi.
Alafu unasikia uzalendo,uzalendo gani huu,taifa linapitia kipindi kigumu,kwa baadhi kufanya majaribu ambayo hayakua na sababu
Vyovyote vile itakavyo kua juu ya taifa hili kwa yoyote anehusika au aliehusika kulifikisha taifa mahali pabaya, zambi hii itatafuna ukoo wake mzima
Inauma Sana Yani, mkuu
 
Alafu unasikia uzalendo,uzalendo gani huu,taifa linapitia kipindi kigumu,kwa baadhi kufanya majaribu ambayo hayakua na sababu
Vyovyote vile itakavyo kua juu ya taifa hili kwa yoyote anehusika au aliehusika kulifikisha taifa mahali pabaya, zambi hii itatafuna ukoo wake mzima
Inauma Sana Yani, mkuu

Nina kusoma mkuu. Sala zako na zikawe hivyo inshallah.
 
Mabibi na mabwana kama nchi tumepwelewa sana katika hili la maridhiano. Kwa hakika matatizo yetu kama nchi yako hapo na ndiyo maana tuko hapa tulipo na sasa kama mazuzu tu.

Mbowe ameonyesha kwa vitendo kuwa kinachohitajika katika migogoro ukiwamo huu ni maridhiano. Jibu la Bi. Halima kwenye hili kuwa wapo tayari "kuyajenga" mbona ni la kupongezwa mno?

Ikumbukwe pana wenye kupenda kuukaanga mbuyu vilivyo ili kuwaachia wenye meno kutafuna.

Hebu wasipewe nafasi hao.

Wakaanga mbuyu na wakajifunze kwa vitendo.

Kwa maneno ya bi Tshala Mwana, "bibi na bwana wakigombana nyumbani waache wataelewana wenyewe. Ukiyaingilia utabaki na aibu"

Muda wa kuwafahamisha wasiohusika bila ya kujali vyeo vyao au vyama vyao - kuufyata!

Ipewe sasa nafasi ya hoja kutamalaki katika mazingira yenye kufaa. Kusamehe 7x70 ni sehemu ya maisha ya binadamu wenye utu. Wanasema waungwana, "we can live and let live!"

Nini taabu kama maridhiano yakatufikisha kwenye:

1. Kuwajua waasisi wa ghushi?
2. Kuwashugulikia waasisi wa ghushi?
3. Kuwaumbua waasisi wa ghushi?
4. Kuwapa funzo la kudumu waasisi wa ghushi?
5. Kuufunga mjadala wa ghushi hii katika namna inayokubalika?

Kamanda Mbowe na makamanda wote kwa kauli ya bi dada leo, kukaa nao rasmi au hata kivinginevyo lengo kuyajenga itakuwa ni sahihi sana. Ikumbukwe kuwa kuhitajika kuyajenga kwanza kabla ya mengine limo kwenye sehemu ya hukumu.

Walionyeshwa mlango wa kutokea ila haukupigwa kufuli. Bi Halima hakukunja ngumi. Kwa hekima amenyoosha mkono. Ni busara kuupokea.

Kwa maneno ya Jabali la Muziki: "Tukamsake mbaya wetu anaye tuchonganisha." Siku tukimpata zikawe zetu ama zake!

Mungu ibariki CHADEMA.
Siku zote kuna gharama zisizoonekana za usaliti. Moja ya gharama hizo ni kukosa kibali cha muunganiko wa akili,mwili na matukio. Kwa Halima Mdee yote hayo yametokea.
 
Kwanini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010, 2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
KWANI WEWE INAKUHUSU HIYO? KWANI HIYO MIAKA WALIYOENDA WALIAPISHWA VICHOCHORONI KAMA SASA? JE, HIYO MIAKA WALIYOENDA WALIKWENDA BILA KUPELEKWA NA CHAMA? WALIPITA NJIA ZA PANYA KAMA HAWA COVID-19?
 
Siku zote kuna gharama zisizoonekana za usaliti. Moja ya gharama hizo ni kukosa kibali cha muunganiko wa akili,mwili na matukio. Kwa Halima Mdee yote hayo yametokea.

La maana kabisa kwenye yote - kuyajenga. Hilo ametamka. Kwa hilo kumpongeza japo kwa hapo si haba.
 
Joto lilikuwa kubwa mno. Hamna mtu ambae angewaelewa kama wangeahirisha kikao. Wahasimu wao wangepata nafasi ya kusema wameogopa kuumbuliwa kwa sababu wana mkono wao katika mchakato mzima.

Sasa hivi kazi iliyoko mbele ni namna ya kutatua mgogoro bila kuacha madhara makubwa kwenye chama. Halima katika press yake ameonyesha kuwa yuko tayari kushirikiana kufanya hivyo.

Kwangu mimi kilichodhihirisha kwangu ni mapenzi yake makubwa kwa chama chake na hasa Mwenyekiti wake ambae anamuona kama mzazi wake. Na Mwenyekiti wake hata alipokuwa anasoma hukumu alionekana kusikitishwa zaidi kuliko kukasirika kwa hiki kitendo cha watu aliokuwa na imani nao. Tukumbuke, hawa wamefungwa pamoja nae, wamepigwa na wamenyanyaswa sana kutokana na misimamo yao kutetea maslahi ya chama chao. Ndio maana Mbowe hakutumia maneno ya shombo dhidi yao na alisisitiza kuwa bado kuna njia ya wao kurudi kundini.

Ni wajibu wetu sisi tulio nje tuwape nafasi ya kukaa pamoja na kutibia vidonda vyao wakiwa wenyewe.

Amandla...
Kwa haya maelezo yako ni sawa na kusema kwamba Kamati kuu ilifanya maamuzi kwa mihemuko kutokana na hilo joto lililokuwepo,ndiyo maana Mdee aliona atulie kwanza ili watu hasira zishuke na sasa ndio ameona muda sahihi kwa watu washatukana kadri wawezavyo na kuwamalizia hasira zote.
 
Amecheza karata vizuri, ila angeleta ujeuri wa kutishia kuhama chama basi ndio ulikua mwisho wake kisiasa.

Ange danganyika kwenda CCM kisa Dk. Bashiru amemkaribisha au kinga walioahidiwa na Speaker pamoja na A.G, angekutana na fitna nyingi sana za wana CCM kindaki ndaki.

ILA BADO ninaamini serikali ndio imemshinikiza aongee hayo kwenye hii press ya leo. Baada ya kuona dunia na taifa zima limepokea "NEGATIVELY" kulazimishwa kwa Covid-19 kuapishwa bila ridhaa ya chama chao na Mwanasheria Mkuu Wa Serikali na Speaker kujigamba kuwatetea kwa nguvu zote.

Pia Covid-19 walishagawanyika, kuna waliotaka kurudi na kuomba msamaha, na kuna waliotaka waendelee na ukauzu wao.

CHADEMA NINGEPENDA KUONA wanatumia karata zao vizuri kukubali maridhiano ya kina Halima Mdee & Co LTD. Kwa kuwapa mashart umiza;

1) Ili kupokea baraka na msamaha wa chama, basi Covid-19 wafanye press kutoa muongozo wa nani alieshinikiza wao kuapishwa. Na vikao vilifanyika vipi na wapi.

2) Covid-19 waandike barua za kujivua ubunge wa kuteuliwa kwa NEC na SPEAKER (Japo kisheria baada ya kufukuzwa uwanachama wameshaondolewa).

3) Katika press hio Covid-19 watoe tamko la kuungana na wanachama wenzao sambamba na vyama vingine vya upinzani kutotambua uchaguzi mkuu 2020 pamoja na bunge hili.

4) Pia katika press hio "WAOMBE MSAMAHA CHAMA NA WANACHAMA" kwa kukubali kufanya hayo waliofanya ya kuapishwa bila ridhaa ya chama. Na wakiri walikosea sana.
Wanirudishie pesa yangu, niliyochangia kipindi wapo magereza, waache ujinga
 
Back
Top Bottom