Halima umeonesha mwanzo mzuri, maridhiano

Halima umeonesha mwanzo mzuri, maridhiano

Kwanini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010, 2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
2010 chama kilipata na wabunge wa majimbo,kilikalamika kuhusu rafu,2015pia kilipata na wabunge wa majimbo ndio maana walikwenda mjengoni.

2020 chama kimelalamika kuhusu rafu mbaya haijawahi kutokea tangu1995,na mdee ni miongoni mwa waathirika na hizo rafu,halina ubishi Hilo.

Kwa kauli moja ya chama wakiamua walivyoamua na mdee lazima alikua mmoja wa waliyofanya maamuzi hayo,nafikiri jibiu linakutosha au....

Na hata Kama ingekua hivyo,yeye Kama mwwnyekiti bawacha asingejichagua yeye Wala yeyote aliyekua mbunge mwakilishi kabda labda angeeleweka.

Na Kama ni lazima,vitu maalum wapewe wamama wengine kabisa ni haki Yao,mdee na baadhi wamehudumu kwa vipindii vitatu,inatosha.

Mdee amechemka sio sawa kabisa,Safari hii wamama walipewa nafasi Sana kugombea majimboni,ni Nani aliuliza haki hizo wamepewa na Nani?
 
Sasa Kamati kuu iliharakisha nini kutoa maamuzi ya kuwafukuza?
Joto lilikuwa kubwa mno. Hamna mtu ambae angewaelewa kama wangeahirisha kikao. Wahasimu wao wangepata nafasi ya kusema wameogopa kuumbuliwa kwa sababu wana mkono wao katika mchakato mzima.

Sasa hivi kazi iliyoko mbele ni namna ya kutatua mgogoro bila kuacha madhara makubwa kwenye chama. Halima katika press yake ameonyesha kuwa yuko tayari kushirikiana kufanya hivyo.

Kwangu mimi kilichodhihirisha kwangu ni mapenzi yake makubwa kwa chama chake na hasa Mwenyekiti wake ambae anamuona kama mzazi wake. Na Mwenyekiti wake hata alipokuwa anasoma hukumu alionekana kusikitishwa zaidi kuliko kukasirika kwa hiki kitendo cha watu aliokuwa na imani nao. Tukumbuke, hawa wamefungwa pamoja nae, wamepigwa na wamenyanyaswa sana kutokana na misimamo yao kutetea maslahi ya chama chao. Ndio maana Mbowe hakutumia maneno ya shombo dhidi yao na alisisitiza kuwa bado kuna njia ya wao kurudi kundini.

Ni wajibu wetu sisi tulio nje tuwape nafasi ya kukaa pamoja na kutibia vidonda vyao wakiwa wenyewe.

Amandla...
 
Ameshidwa kujibu maswaii mwishowe kaishia kumsifu Mbowe kawaeea, waiokuwa wanasema mbowe ana mfumo dume wameshidwa, maji yamemfika shingoni mpaka anakwenda na wazazi wake, wameshidwa vibaya hao Covid 19.
 
Mabibi na mabwana kama nchi tumepwelewa sana katika hili la maridhiano. Kwa hakika matatizo yetu kama nchi yako hapo na ndiyo maana tuko hapa tulipo na sasa kama mazuzu tu...
Ili arudi ni aachane na ubunge yeye na wenzake akubali maamuzi ya kamati kuu, akifanya hivyo tunampa kadi za uwanachama arudi upya lakini akijaribu kuweka sharti sijui 2010, 2015 hatukutambua matokeo ya uchaguzi lakini tulienda bungeni hatutaelewana, na lazima afahamu 2020 matokeo ya kura yalipikwa kwa kiwango kikubwa zaidi hivyo hatuna mpango wa kushirikiana na bunge kwa kupeleka viti maalum.
 
2010 chama kilipata na wabunge wa majimbo,kilikalamika kuhusu rafu,2015pia kilipata na wabunge wa majimbo ndio maana walikwenda mjengoni...

Hoja yako iko wazi.

Hata hivyo mkuu, kosa ni kurudia kosa. Wanasema "let's give it a try."
 
Mabibi na mabwana kama nchi tumepwelewa sana katika hili la maridhiano. Kwa hakika matatizo yetu kama nchi yako hapo na ndiyo maana tuko hapa tulipo na sasa kama mazuzu tu...
Hwawa COVID 19 dawa yao ni kupukutishwa kabsaaaa mazima wavuliwe magwanda mpaka bikini zao wakafie mbele
 
2010 na 2015 CHADEMA iligoma kutambua matokeo ya Urais pekee. 2020 imegoma kutambua matokeo yote ya uchaguzi mkuu. Elewa tofauti hapo.
Ulimsikiliza Mdee alichosema lakini?
 
Hwawa COVID 19 dawa yao ni kupukutishwa kabsaaaa mazima wavuliwe magwanda mpaka bikini zao wakafie mbele

Art ya vita iko tofauti. Katika vita cha msingi ni ushindi.

Ushindi wa CHADEMA ni mwiba kwa mboga mboga. Soma comments za mboga mboga hata kwenye uzi huu kutambua wangependelea nini kwenye mgogoro huu.

Wasipokuwa tayari kuyajenga wanapukutiswa huo ndiyo msimamo. Wako tayari kuyajenga kama sisi si mboga mboga tusiende na matakwa ya mboga mboga!
 
Joto lilikuwa kubwa mno. Hamna mtu ambae angewaelewa kama wangeahirisha kikao. Wahasimu wao wangepata nafasi ya kusema wameogopa kuumbuliwa kwa sababu wana mkono wao katika mchakato mzima...

Mkuu umenena vyema sana. Halima kaonyesha kuumia kwa yaliyotokea.

"Kuyajenga" - neno hili ni zito sana.

Wapewe nafasi. Nakazia, wanapoyajenga huwa ni busara kwa wasiohusika kuufyata.

"Ni furaha iliyo je mbinguni kwa mwenye dhambi mmoja akitubu?"
 
huyo muasi na wenzake tumeshawatimua kwenye Chama.
amekua wabariiidi ameshindwa kujibu maswali kwasababu ni wazi ni muasi.

Mkuu heshima kwako.

Ni kweli kuwa amefukuzwa. Pia ni kweli kuwa maswali hakuyajibu pale. Ni kweli kuwa sababu ni za wazi. Lakini waswahili wanasema, kosa moja lisifukuze mke - hasa kama huko tayari kuyajenga.

La maana katika aliyosema ni nia yake ya dhati kuona mtafaruku huu una malizika kwa maslahi ya CHADEMA.

Maslahi ya CHADEMA yanajulikana. Tuwape muda makamanda Mbowe Lissu na wote wanaohesabika.

Watatuvusha.
 
Kwanini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010, 2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
Kwasababu huko nyuma walipewa nafasi hata kuhesabu kura kwenye kata na kubaki na documents zilizowasaidia kwenda mahakani kupinga matokeo tofauti na Sasa hata mawakala wao walishindwa kuingia vituoni.
 
Kwanini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010, 2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
Mdee nae naona hajawajibu Chadema, majina yao yalipelekwa na nani NEC, kikao gani kilitoa baraka za wao(tena kwa kujipendelea, kwa sababu wote ni viongozi wa BAWACHA) za majina yao kupewa uteuzi? Nadhani Mdee ajibu maswali hayo kwanza kabla ya janja janja
 
Mabibi na mabwana kama nchi tumepwelewa sana katika hili la maridhiano. Kwa hakika matatizo yetu kama nchi yako hapo na ndiyo maana tuko hapa tulipo na sasa kama mazuzu tu.

Mbowe ameonyesha kwa vitendo kuwa kinachohitajika katika migogoro ukiwamo huu ni maridhiano. Jibu la Bi. Halima kwenye hili kuwa wapo tayari "kuyajenga" mbona ni la kupongezwa mno?

Ikumbukwe pana wenye kupenda kuukaanga mbuyu vilivyo ili kuwaachia wenye meno kutafuna.

Hebu wasipewe nafasi hao.

Wakaanga mbuyu na wakajifunze kwa vitendo.

Kwa maneno ya bi Tshala Mwana, "bibi na bwana wakigombana nyumbani waache wataelewana wenyewe. Ukiyaingilia utabaki na aibu"

Muda wa kuwafahamisha wasiohusika bila ya kujali vyeo vyao au vyama vyao - kuufyata!

Ipewe sasa nafasi ya hoja kutamalaki katika mazingira yenye kufaa. Kusamehe 7x70 ni sehemu ya maisha ya binadamu wenye utu. Wanasema waungwana, "we can live and let live!"

Nini taabu kama maridhiano yakatufikisha kwenye:

1. Kuwajua waasisi wa ghushi?
2. Kuwashugulikia waasisi wa ghushi?
3. Kuwaumbua waasisi wa ghushi?
4. Kuwapa funzo la kudumu waasisi wa ghushi?
5. Kuufunga mjadala wa ghushi hii katika namna inayokubalika?

Kamanda Mbowe na makamanda wote kwa kauli ya bi dada leo, kukaa nao rasmi au hata kivinginevyo lengo kuyajenga itakuwa ni sahihi sana. Ikumbukwe kuwa kuhitajika kuyajenga kwanza kabla ya mengine limo kwenye sehemu ya hukumu.

Walionyeshwa mlango wa kutokea ila haukupigwa kufuli. Bi Halima hakukunja ngumi. Kwa hekima amenyoosha mkono. Ni busara kuupokea.

Kwa maneno ya Jabali la Muziki: "Tukamsake mbaya wetu anaye tuchonganisha." Siku tukimpata zikawe zetu ama zake!

Mungu ibariki CHADEMA.
Hakuna Cha maridhiano hapa,mtu unasemaje kwamba eti uchaguzi tangu 2010 uchaguzi usio ridhisha na wabunge walikua wanaenda ebo
So what
Aliesema jana na leo ni siku zinazofanana nani?
Ok hata Kama walienda wabunge si ni bahada ya makubaliano ya chama kwani yalikua mahamuzi ya kakundi la watu ? Inakuaje uwe ndani ya tahasisi alafu utake uende Kama unavyotaka, nini maana ya mamlaka ya tahasis,katiba n.k kwamba kila mtu aweze hamua kile akitakacho
Mpaka mda huu, hata kwenye press mmetia huruma, mpaka mnakwepa jibu ya maswali mfano
Swali zuri kauliza mhandishi Kati ya maswali mengine, kwamba Kama chama chenu hakitambui serikali iliyo madarakani je nyie kuendelea kuwa wabunge mnahitambua, ? Umelikimbia mazima
Niseme mmezidi jishushia hadhi ,Sana, hata elim zenu hamjazitendea haki,hivyo hata kukataa rufaa halmashauri kuu, hakutobadilisha lolote,na huko mahamuzi yatakua hata zaidi ya kamati kuu,
Endeleeni na Mambo yenu ya chadema yaache, KWA press ya leo mngeongea maneno TUSAMEHENI CHADEMA NA WANACHADEMA kidogo mgerudisha heshima iliyokua imebaki
Wananchi Wana hasira Sana na nyinyi achilia mbali wanachama
 
Hiyo miaka ya 2010 walienda kwa sababu mbowe alishinda uchaguzi

Na 2020 hawaendi kwa sababu Mbowe ameshindwa uchaguzi
Miaka hiyo, hata walioteuliwa, Waliteuliwa na Kikao halali cha chama chao, siyo usanii walioufanya. Hata kama CDM wanamapungufu yao, lakini kama wamesimamia taratibu, hao wadada walistahili KUFUKUZWA. Naamini hata ingekua CCM wangefukuzwa.
 
Kwanini hamjibu swali la Mdee?

Kwa nini 2010, 2015 wabunge wa viti maalum waende bungeni na 2020 wasiende?
Kwasababu 2010,2015 mwenye chama alikuwa na nafasi ya kuingia bungeni.
ilo ndo jibu bwashee.
 
Hakuna Cha maridhiano hapa,mtu unasemaje kwamba eti uchaguzi tangu 2010 uchaguzi usio ridhisha na wabunge walikua wanaenda ebo
So what
Aliesema jana na leo ni siku zinazofanana nani?
Ok hata Kama walienda wabunge si ni bahada ya makubaliano ya chama kwani yalikua mahamuzi ya kakundi la watu ? Inakuaje uwe ndani ya tahasisi alafu utake uende Kama unavyotaka, nini maana ya mamlaka ya tahasis,katiba n.k kwamba kila mtu aweze hamua kile akitakacho
Mpaka mda huu, hata kwenye press mmetia huruma, mpaka mnakwepa jibu ya maswali mfano
Swali zuri kauliza mhandishi Kati ya maswali mengine, kwamba Kama chama chenu hakitambui serikali iliyo madarakani je nyie kuendelea kuwa wabunge mnahitambua, ? Umelikimbia mazima
Niseme mmezidi jishushia hadhi ,Sana, hata elim zenu hamjazitendea haki,hivyo hata kukataa rufaa halmashauri kuu, hakutobadilisha lolote,na huko mahamuzi yatakua hata zaidi ya kamati kuu,
Endeleeni na Mambo yenu ya chadema yaache, KWA press ya leo mngeongea maneno TUSAMEHENI CHADEMA NA WANACHADEMA kidogo mgerudisha heshima iliyokua imebaki
Wananchi Wana hasira Sana na nyinyi achilia mbali wanachama

Machungu ya CHADEMA yeyote kwenye hili yanajulikana.

Hata hivyo kama nia ya kuweka mambo sawa ipo. Haipo shaka kamanda Mbowe, Lissu na wote wanaohesabika wanaweza kuweka kila kitu sawa tukafika hapa kwenye kuwajua wabaya wetu. Yaani:

1. Kuwajua waasisi wa ghushi.
2. Kuwashugulikia waasisi wa ghushi.
3. Kuwaumbua waasisi wa ghushi.
4. Kuwapa funzo la kudumu waasisi wa ghushi.
5. Kuufunga mjadala wa ghushi hii katika namna inayokubalika.

Bottom line ya requirements za chama ziko wazi.
 
Back
Top Bottom