Halima Mdee kamtukana Rais kwa tusi gani?

Halima Mdee kamtukana Rais kwa tusi gani?

Kitu cha kwanza ni kukomesha upinzani kwanza maendeleo baadae!
Ndio maana wenzetu wanatuita tunakaa bara la Giza!
Sasa maendeleo yatatoka wapi?
.....Imani yao ni kwamba adui wa maendeleo ya nchi hii since independence ni opposition, maajabu ni kwamba hawataki pia kufuta multiparty system from the constitution kwa kuogopa kunyimwa misaada.

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama alimtukana Rais ila kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa wilaya ya kinondoni Halima katika hotuba yake alisema ni vema Rais Magufuli akafungwa break..! so anawasaidia polisi kujua ni aina gani ya break ambayo anategemea kuitumia kumfunga rais.
hivyo sidhani kama anatarajiwa kutoka hivi karibuni..
ni mpaka pale polisi watakaporidhika kuwa hiyo aina ya break aliyoisema ndio aliyo ikusudia..
kuna watu wanasumbua Kibiti ni vizuri tukafahamu pia huenda wana mahusiano.
....Endeleeni kutanua magoli from kutukana na sasa Kibiti...

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Uzuri kuna kitu kimoja watu wanajisahau sana,aliyemuweka ndani kwa kujipendekeza hicho cheo amepewa kama mtu unvyopewa gazeti usome,dakika yeyote mwenye nalo anaweza kulichukua na ukabakia mikono mitupu
....Mfano Nape, Muhongo, yule chapombe Kitwa....

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Kuhoji huku jf kuwa huyo mama alitukana tusi gani haimsaidii chochote. Cha msingi nenda central ukamshauri ale chakula maana jumanne anaweza akafunguliwa kesi ya suicide attempt.
....Aliyekuambia kwamba amekuhoji wewe hapa JF ni nani? Mbona una kimbele mbele sana? Hili ni jukwaa huru kama huna la kuchangia piga kimya tuu.

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama umezaliwa kawaida. Itakuwa umedondoshwa ndio maana ubongo wako umejaa rohau.
....Rubbish as usual. Halafu kama unaamini mtu anadondoshwa kuna kingine ambacho akili yako is capable of? Nyinyi ndiyo mtaji wa Lumumba as Twaweza correctly said.

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Maneno aliyosema Halima, anaweza kumwambia baba yake? Au mumewe?
Neno mshikaji si tusi, wewe unaweza kumwita baba au mama yako msikaji wako? Tuliitwa mafara na mabwege mbona polisi hawakumkamata aliyesema hayo licha yalilengwa kwa baadhi ya watu wenye umri wa baba take! Simama, fikiri, tafakari usiwe kama chura.
 
Kuhoji huku jf kuwa huyo mama alitukana tusi gani haimsaidii chochote. Cha msingi nenda central ukamshauri ale chakula maana jumanne anaweza akafunguliwa kesi ya suicide attempt.
Mkuu Halima hajafanya jaribio lolote la kutaka kujiua. Kuna tofauti kati ya "suicide attempt" na "hunger srike". Halima yuko kwenye hunger strike, hakuna suicide attempt hapo. Kwa maana hiyo hawezi kufunguliwa kesi kwa kugoma kula.
 
Maneno aliyosema Halima, anaweza kumwambia baba yake? Au mumewe?
Halima ni Upinzani, hawezi kuchaguliwa maneno dhidi ya Upinzani wake. Hapa walisema kuna mtu anajinyea tusi baya na la kunyanyapaa mtu kuliko yote duniani! Hakuna aliyeswekwa ndani, ohhoo white house si wodi ya wagonjwa hakuna aliyewekwa Lupango. One day Yes Haki itasimama
 
Kitu cha kwanza ni kukomesha upinzani kwanza maendeleo baadae!
Ndio maana wenzetu wanatuita tunakaa bara la Giza!
Sasa maendeleo yatatoka wapi?
Mi nadhani upinzani sio kama wanakomeshwa ila wanatafuta kiki ili ionekane wanaonewa. Kwa sababu kauli zingine hazina tija kwa taifa wala kwa mtu binafsi. Ila kwa upinzani wa kipuuzi baada ya kuhimiza maendeleo ya wananchi wao wanang'ang'ania mambo yasio na tija. Lema amekaa gerezani zaidi ya miezi 4 tumepata tija gani? Je ndoto aliyoiota Lema ilikuwa na tija gani kwa taifa. Mi naona ni sawa tu wasweke lumande ili wapate kiki vizuri.
 
kama hayana tija unaonaje wangepuuzwa tu tuendelee kujenga taifa letu kuliko kuwapa kiki kama unavyosema?
 
kama hayana tija unaonaje wangepuuzwa tu tuendelee kujenga taifa letu kuliko kuwapa kiki kama unavyosema?
Kama wao hawako tayari kuyapuuza kwa nini nao wapuuzwi, dawa ya moto ni moto, kama mbwai ni mbwai tu barida. Tatizo upinzani wetu hauna njia mbadala za kuwasaidia wananchi bali ni political gain tu. Kwani ukiangalia maauala yote yanayowapeleka hatiani si ya kutetea wananchi.
 
Na hawata lipata ng'o , ndio sababu ya kuendelea kumshikilia kwa kisingizio cha 'Uchunguzi bado hauja kamilika'...
Kama hatutopenda kutumia busara basi itakuwa shida sana, kwani Lema alivyokaa mahubusu siku zote ulifnya nini. Tusishadadie wenzetu kukaa mahabusu wakati wewe unakula maisha uraiani
 
Back
Top Bottom