Halima Mdee: Bold and Beautiful!

Halima Mdee: Bold and Beautiful!

ila sauti yake inanitia mashaka:

huenda anavuta bangi

au mtu wa zantel to zantel

Wewe unajiita mtu-wa-pwani JF senior Expert member halafu busara ndiyo hiyo imemomonyoka, kuwa mstaarabu kusema mwenzako anavuta bangi usifikiri ni hekima,(No reseach no right to say) kuwa muungwana na mwadilifu kame expert senior. Ushauri wa bure huu.
 
masaki huyu rais wake ni jk na mbuge ni Mnyika
 
05-novemba-2010: feed back

Hatimaye mpaka leo hii, halima mdee ni mbunge mteule wa jimbo la kawe.
 
mnyika1.jpg
Mbunge mteule wa Jimbo la Ubungo,John Mnyika

Na Ramadhan Semtawa
TOFAUTI na muongo mmoja uliopita ambao CCM imeweza kuwa na ngome imara ya kisiasa mkoani Dar es Salaam, safari hii kambi ya upinzani imeweza kuiteka baada ya kupata kura za ubunge 395,157 ikilinganishwa na 345,101 za chama tawala.

Pigo hilo la ngome ya CCM limekwenda sambamba na ushindi wa upinzani kwa kupata viti viwili vya ubunge majimbo ya Kawe na Ubungo.

Kwa mujibu wa mchanganuo wa kura za ubunge zilizotangazwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), zinaonyesha jimbo la Kinondoni CCM ililinda ngome yake, lakini kwa ushindi mdogo wa kura 51,372 sawa na asilimia 50 dhidi ya 51,150 za Chadema huku jumla ya kura zikiwa ni 102,522.
Jimbo hilo limekuwa likiongozwa na Iddi Azzan wa CCM limeweza kuangukia tena mikononi mwa chama hicho kikongwe barani Afrika.

Katika Jimbo la Ukonga, CCM pia iliweza kutetea ngome yake kwa kura 28,000 sawa na asilimia 40 dhidi ya 18,819 za Chadema na jumla ya kura zilikuwa 46,891, jimbo hilo pia limeangukia mikononi mwa chama tawala.



:smile-big: Hata hivyo, katika Jimbo la Kawe ngome ya CCM ilitikiswa baada ya Chadema kupata kura 65,619 sawa na asilimia 66 dhidi ya 34,412 za CCM, jumla ya kura ni 100,031.

Jimbo la Ubungo, ngome ya CCM ilitikiswa tena baada ya Chadema kupata kura 81,346 sawa na asilimia 62, ikilinganishwa na kura 50,544, huku jumla ya kura zikiwa ni 131,890.



Kwa mara ya kwanza baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, jimbo hilo lilichukuliwa mwaka 1995 na Dk Masumbuko Lamwai kipindi hicho akiwa NCCR-Mageuzi, lakini mahakama ilibatilisha ushindi huo na CCM kupitia kwa Venance Ngulla ikalinyakua tena.

CCM pamoja na kwamba iliweza kushinda Jimbo la Segerea, lakini iliweza kupata upinzani mkubwa baada ya kushinda kwa kura 43,5557 sawa na asilimia 57 dhidi ya 39,150 za Chadema na 18,737 za CUF.

Temeke, jimbo hilo ambalo liliwahi kunyakuliwa na Augustine Mrema akiwa NCRR-Mageuzi, limeangukia tena CCM lakini kwa ushindi mwembamba wa kura 59,886 sawa na asilimia 51 dhidi ya kura 58,339.

Katika jimbo la Kigamboni, CCM pia iliweza kutetea ngome yake lakini kwa nguvu kubwa baada ya kushinda kwa kura 53,389 sawa na asilimia 49 dhidi ya kura 51,370 za Chadema, huku jumla ya kura 104,759.
Hata hivyo, katika Jimbo la Ilala, CCM imeweza kutetea ngome yake kwa kishindo baada ya kupata kura 25,490 sawa na asilimia 26 dhidi ya kura 9,008 katika kura jumla 34,498.


comment:
soma hapo kwenye blue
 
Hongera Halima. You are really bold And beautiful. I am travelling to Dodoma to come and shake your hand and congratulate you after you are sworn in as an Elected Member of Parliment.
 
Hongera sana, mdee mi binafisi na vutiwa na kujiamini kwako, endeleza mapambanoooooooooooo
 
wakuu wenye habari za mhe huyu atupatie yanayojiri kumhusu yeye.
 
hatimaye mhe halima mdee na wabunge wenzake wameamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge katika habari maarufu ya kutoyatambua matokeo ya urais kufuatia harakati za uchakachuaji.
 
wabunge wa chadema wametoka nje ya ukumbi wa bunge kumsusia jk kama vyombo vya habari vilivyoripoti uvumi; mhe mdee naye yumo katika tukio hili la kihistoria.
 
HalimaMdee.jpg

Namuita iron lady!!! huyu mheshimiwa anayemaliza muda wake kama mbuge wa kuteuliwa, sasa anagombea kupitia chadema kwenye jimbo ambalo yule anayemalizia kaamua kulikimbia (kwa kumwogopa halima???) na kugombea kupitia nafasi ya NGOs.
3.jpg

kihistoria ametoka kwenye familia ya ccm lakini akaamua kutoka kivyake; akiweka 'historia' kisogoni (kwanini asiitwe bold/iron lady?)
halima+mdee.jpg
11311.png
12-mdee.jpg

akiwa mjengoni amefanikiwa kutoa mchango wa mawazo kwa ujasiri wa hali ya juu kiasi cha kufikia kukwaruzana na kigogo wa ccm ambaye aliamua kumpeleka 'nusu-mahakama' (kwa 6) lakini kwa ujasiri wake mhe. mdee (as she then was), ilibidi mzee wa bumbuli alazimike ku 'drop charges'



my take:
huyu mdada anafaa kupewa nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi la kawe; she is bold and yet beautiful!!!
(huo mtazamo wangu tu usijali sana!!!)


05-novemba-2010: feed back

Hatimaye mpaka leo hii, halima mdee ni mbunge mteule wa jimbo la kawe.


Basi leteni picha zake akiwa kwenye uniform za mgambo kama wenzake wa CHADEMA.
 
Basi leteni picha zake akiwa kwenye uniform za mgambo kama wenzake wa CHADEMA.





nakushauri we ndo umlete kwenye hizo uniform tajwa. hizo ambazo unaonekana hupendi ni picha kutoka vyanzo mbalimbali ikiwepo global publishers.
 
je halima mdee na wenzake wa cdm wako tayari kukubaliana na matokeo ya kususia ufunguzi wa bunge la 10 hapo juzi; kama wenzao wa ccm walivyotishia juzi?
 
Kuna kipindi alikomaa na uuzwaji wa eneo moja wazi kule kawe ambapo Makamba na sijui meya wa jiji yule walihusika.
Wote walislim amri kwa uyu mdada
 
Wewe unajiita mtu-wa-pwani JF senior Expert member halafu busara ndiyo hiyo imemomonyoka, kuwa mstaarabu kusema mwenzako anavuta bangi usifikiri ni hekima,(No reseach no right to say) kuwa muungwana na mwadilifu kame expert senior. Ushauri wa bure huu.


mkuu nisamehe huenda j=hujamsikia huyu dada akiongea kwa kweli sauti yake sio nyepesi kama wanawake wa kawaida na ndio nikasema nna wasi wasi na sina hakika kama havuti bangi ila kwa kumkubali nnamkubali, wako wachache ndani ya chadema nnawakubali akiwemo huyu dada
 
Back
Top Bottom