Halima Mdee amwita Dk. Magufuli Jembe

Halima Mdee amwita Dk. Magufuli Jembe

Lema na Mbowe pamoja na Dr.Slaa sijui watamchukulia hatua yeyote Halima Mdee au kwa sababu ni wa nyumbani.

ni ccm tu ndiyo mtu huchukuliwa hatua anapo pongeza mema yanayofanywa na upinzani, ndiyo maana nawew upo mtandaoni kupnga chchte toka kwa wapinzan na kuunga mkono ujinga wowote toka kwa mafisadi wa ccm. kifupi n kwamba wapinza wanaufahamu kamili but wewe na wajinga wenzio akili zenu mmeshikiwa na Nape! mnawaza buku7 tu.
 
Jembe la CHATO, tumekumis mbunge wetu. Soon tutafungua bendi maana unavyochanganya ngoma DR wa ukweli upo juu
 
Hii show ya kustaajabisha sana, yaani madabida anachangia madawati kwa Mnyika, Mdee anamsifia Magufuli, haya tuambieni tril moja kujenga km 55.5 hizi barabara zina njia 16 kama gear za eveco ya msomali? flyover ziko ngapi? nawajenzi ni wachina au struburg? yaani bil18.8/km nasema hapana.
 
Katika hali isiyotarajiwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee amemtaja Dk.Magufuli kuwa ni Jembe kwenye mkutano Goba katika uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi barabara ya Mbezi Mwisho kwenda Goba mpaka Tangi Bovu.

Aidha, wananchi wa Goba (Wote CHADEMA na CCM) wamempokea Dk.Magufuli kwa shangwe wakimwita "JEMBE JEMBE" Clip ya video inakuja.

Pia alikuwepo Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika na wote kwa pamoja wamesema "MAENDELEO HAYANA CHAMA"






View attachment 221823
Dk.Magufuli (W/Ujenzi), Halima Mdee(MB-Kawe) na Madabida(M/Kiti CCM -Dsm)
View attachment 221825
Kutoka Kushoto Mkuu wa Mkoa Dsm, Dk.Magufuli, Madabida na Mh.Mnyika.​




Haaaaa....ndio hii hafla niliyoiona kwa gazet la mwananchi. Ambayo magufur amekosea kufunga vifungo vya shati?
 
Last edited by a moderator:
Kweli magufuli anakubalika kila kona za tanzania na kila nyumba na kila chumba cha nchi hii. msikilize halima mdee anakiri kuwa kabla ya magufuli hali ilikuwa ngumu ingawa wabunge wa jimbo walikuwa ccm, ila magufuli kaingia maendeleo mpaka upinzani na wanamkubali.

sikiliza mwenyewe.

https://www.youtube.com/watch?v=0jgWKjndS10
 
Penye ukweli tuseme Hongera mdee kuwa not biased na mihemko ya kichama
 
Mdee anataka rais akiingia amkumbuke ata ubunge wa kuteuliwa maana hana uakika wa kurud bungeni
 
Halima ameenda shule,anaelewa,sio ushabiki tuu wa kijinga,kusema hivyo wasio elewa lazima wataleta longolongo
 
Kwa kile kilichofanyika jimboni mwake kizuri juwa kakipigania bungeni lazima afurahi
 
Kwani ni magufuri au ni wananchi kupitia kwa mtumishi magufuri? Hizo ni kodi za wananchi wali si hela magufuri. Kingine, hapo ametimiza majukumu yake anayoripiwa mshahara.
 
Kwani ni magufuri au ni wananchi kupitia kwa mtumishi magufuri? Hizo ni kodi za wananchi wali si hela magufuri. Kingine, hapo ametimiza majukumu yake anayoripiwa mshahara.

Tuambie ni kiongozi gani atatoa fedha yake mfukoni kuleta maendeleo.Acha siasa za upepo.
 
Magufuli ni Jembe ndani ya mfumo mchafu. Lengo ni kuondoa mfumo
 
Back
Top Bottom