Diwani
JF-Expert Member
- Oct 25, 2014
- 2,903
- 3,139
Yes, now you sound like an Engineer, God bless, suala hapa ni kwamba, elimu katika vinchi vyetu vinavyoendelea bado liko politicized, kwa mfano, dhana ya elimu bure ni dhana duni kuwahi kutokea, elimu ina uhusiano wa moja kwa moja na kila mtu katika jamii, najua kila mkakati una faida na hasara, ila hili la elimu bure ni udumavu. Elimu inapaswa ipokee public fund, yaani kila mtu anapaswa kuchangia elimu, kwenye nchi masikini wenye hela ni masikini wenyewe, sio serikali, people need to fund education. Raia na mataasisi yote, pamoja na wadau mbali mbali wa elimu, ndani na nje ya nchi, kwa sababu ni suala sensitive sana.Upo sahihi teacher kuna usemi mmoja unasema hivi "jamii isiyofundishwa na mwalimu basi itafundishwa na wapumbavu" naelewa jitihada zenu kwenye kupigania future ya Taifa kwani leo hii nimekua mhandisi kwa kupitia mikononi mwa walimu ila kinachonitafakarisha ni kwa namna gani tutaipandisha hadhi hii kada ili iheshimike katika jamii hasa ya kitanzania, sikatai kua ualimu ni wito na hata kama tukisema serikali ikae chini imlipe huyu mtumishi anayeitwa mwalimu sidhani kama kuna kiasi ambacho kitafanana na kile anachokizalisha, isispikua kufanya yale yatakayomkomboa huyu mwalimu ili atoke kwenye lile wimbi la kudharaulika katika jamii kupitia kile anachokiingiza baada ya elimu aitoayo.
Mwisho wote tunajenga Taifa moja na hakuna haja ya kutofautiana.
Nilishawahi kwenda kijiji, fulani pale Mafinga, nikakutana na wana kijiji wanawazungumzia walimu as watu duni, imagine watu ambao walishindwa kulipa 20k kwa ajili ya ada, ati nao wana mshipa wa kusema kuhusu umasikini wa elimu, walimu tunalipwa na serikali kupitia kodi za wananchi, suala ni kwamba, kama kodi hazitoshi kutunza walimu, there must be direct cost, unasomaje bure? Elimu ni product na ni service.
Jambo lingine ni kwamba, walimu huenda wanawekwa nyuma kimaslahi ili watumike kisiasa, kwenye ku propagate agenda za kisiasa, walimu ambao ndio kundi kubwa la watumishi wa uma ni mtaji mkubwa sana; so tumegawanywa na tunatawalika, wapo walimu wanaohitaji mabadiliko, but they are politically nothing, hawawezi ku air hayo mabadiliko kwa sababu hawana nafasi ama platforms za kufanya hayo mabadiliko.
Yapo mengi, we just need time.
Sent from my OPPO A57 using JamiiForums mobile app