DOKEZO Hali ya Huduma na Mazingira katika Wodi No. 11 Jengo la Kibasila, Hospitali ya Taifa -Muhimbili hairidhishi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wodi namba 11 ni miongoni mwa wodi za wanaume zilizopo jengo la Kibasila katika Hospitali ya taifa Muhimbili (Upanga)

Hali ya mazingira katika wodi hiyo sio nzuri
1. Sakafu ni chafu
2. Mashuka yamepauka
3. Vitanda vimechoka na vimepangwa kwa kusongamana
4. Vyandarua licha ya kuwa na rangi nyeupe lakni ni vichafu

Ukilinganisha na wodi nyingine katika hospitali ya taifa Muhimbili, wodi namba 11 itazamwe kwa jicho la pekee na ikiwezekana mamlaka zinazohusika zifanye maboresha ya wodi hii ukizingatia inatoa huduma kwa wagonjwa mara nyingi wenye majeraha ya upasuaji.

Hali ya huduma ni duni

1.Ni kawaida kukuta mwili wa mgonjwa aliyekata roho unaandaliwa katika mazingira ya wazi na wagonjwa wengine wakiwa wanapita huku na kule na wakati mwingine bila hata kuzungusha pazia la kijani.

2. Mgonjwa aliyelazwa Cubic ya tatu ya wodi hii atatakiwa kutumia nguvu kubwa mwita muuguzi anapopata changamoto na wakati mwingine muuguzi (wauguzi) uchelewa kufika kwa mgonjwa husika au kutofika kabsa.

Ni muhimu kuboresha huduma tunayo toa kwa watanzania wenzetu.
 
Wodi ya wanawake namba nne gorofa ya kwanza mwaisela muhimbili huduma ni za kuomba, mgonjwa anahitaji huduma kama kipimo inabidi asubiri mpaka ratiba ya kipimo hicho ifike mgonjwa anaumwa kweli unasubiri siku ya hicho kipimo, wagonjwa wanang'atwa na mbu balaa, ukilazwa unapata na maralia, kingine hii bima mbona siielewi? Kuna vipimo inalipa na vingine hailipi inakuaje hapo?
 
Back
Top Bottom