X men
Member
- Dec 26, 2021
- 11
- 23
MUHIMBILI NA URASIMU WA MEDICAL REPORT.
Nimekuwa nikiuguza mgonjwa wodini pale Jengo la Watoto Hospitali ya Muhimbili kwa vipindi tofauti tofauti, ilikuwa kuomba Medical Report ni bure, lakini kuanzia Prof. Janabi alipoingia kupata Medical report ya mgonjwa ni lazima ulipie Laki moja (Tsh. 100,000/=)
Hilo sio tatizo sana, tatizo linakuja kwamba hata baada ya kulipia hizo gharama inakupasa tena kuanza kuzunguka kuwatafuta madaktari kuwaomba waandike hiyo report, usumbufu zaidi ni kwetu sisi ambao tunatoka mkoani ukiwasiliana na watu wa masjala/PS wanakwambia mtafute daktari wake ama mpigie simu mwambie akuandikie sisi tumeshapeleka file kwake!!
Nina zaidi ya wiki 2 sasa, niko mkoani report inahitajika ofisini ila kila nikiwasiliana na wanaopaswa kuifuatilia report wananizungusha tu, sasa wameweka vipi gharama ya huduma kama hawawezi kuitoa hiyo huduma vizuri?
Hili jambo linatakiwa kushughulikiwa haraka, ni usumbufu sana!!
Majibu ya Muhimbili, soma hapa: Hospitali ya Muhimbili yatoa ufafanuzi kuhusu keri ya ucheleweshwaji wa utoaji wa Medical Report