SoC04 Serikali ianzishe shule za msingi za kata nchini ili kuwa na nguvu kazi tosherezi ya walimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mustafa James

New Member
May 22, 2024
2
0
Serikali imekuwa ikiboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari hapa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya za msingi na sekondari katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Pamoja na jitihada hizo bado kumekuwa na changamoto kubwa katika utoaji wa vifaa tosherezi na ugawaji wa walimu katika shule zetu nchini. Jambo hili limekuwa likififisha na kudhaifisha ubora wa utoaji elimu nchini.

Changamoto hii inaweza kuondolewa kwa serikali kufanya mambo yafuatayo;
1 Serikali iweke bajeti kupitia wizara ya tamisemi zijengwe shule kubwa za kata zenye miundombinu ya madarasa vyoo maktaba na nyumba za walimu tosherezi. Kwa mfano serikali ikijenga madarasa ya ghorofa yenye rosha kuanzia tatu zenye vumba vya madarasa 30 unaweza kukusanya wanafunzi wanaotokea katika vijiji kuanzia nane ambao wanaanzia darasa la tatu mpaka darasa la 6 kulinngana na mtaala mpya halafu hao wanafunzi wote wakae bweni wazazi wachangie chakula.

2. Wanafunzia wa darasa la awali mpaka darasa la pili wao wabaki katika shule zile za msingi zilizokuwepo tangu mwanzo halafu wasome wakirudi nyumbani.

Faida zake
1. Walimu wengi watakuwa katika kituo kimoja cha kazi jambo ambalo litafanya kuwa na nguvukazi kubwa ya ufundishaji na hata uelewa wa watoto utakuwa mkubwa na ufaulishaji utaongezeka. Kwa sababu walimu wapo mfano ukichukua walimu 8 kutoka kila shule ukawaweka shule moja kama kata ilikuwa na shule 10 maana yake shule hii maalumu ya kata itakuwa na walimu 80 hapa ufaulishaji na ufundishaji lazima uwe mkubwa

2. Uanzishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali utakuwa mkubwa kwa sababu kule walikokuwa wanasomea wanafunzi wa madarasa ya tatu mpaka sita madarasa yamebaki wazi na yapo ya kutosha na kule kwenye shule za awali unaweka walimu wanne mpaka watano kwa kila shule.

3 Itasaidia kuwa na mazingira yanayofanana kwa shule zote nchini Tanzania katika ufundishaji vifaa na nguvu kazi ya ufundishaji.

Itawaondoa wanafunzi wa kuanzia darasa la tatu mpaka darasa la sita kuwa katika mazingira ya mtaani ambapo shule hizi za msingi za kata zitapaswa kuwa za bweni hivyo watoto watakaa eneo moja na kupata muda wa kutosha wa kujisomea na kufundishwa tofauti na ilivyo sasa ambapo mazingira wanayotokea kwenda na kurudi nyumbani kila siku wengine yamekuwa changamoto hasa maeneo ya vijijini kutokana na umbali, kutumwa kazi za nyumbani na kushindwa kupata muda tosherezi wa kujisomea.

4. Itaisaidia serikali kuwa mgawanyo sawa wa vifaa vya ufundishaji na walimu wa kutosha kwa kuwa shule zitakuwa chache.

Hivyo ombi langu serikali ipunguze ujenzi wa kila siku wa shule nyingi kila mtaa na kijiji badala yake iweke shule moja kubwa ya kata yenye miundombinu mikubwa ya mabweni na madarasa ya ghorofa na nyumba za kutosha za walimu ili wazazi wao wachangie chakula na mahitaji mengine ya msingi ili elimu yetu iwe bora zaidi na yenye ufanisi na kuweza kumudu upatikanaji wa walimu tosherezi shuleni.

Mustafa James katole
0782593170
 
Mkuu Maendeleo ya sayansi kwa sasa inabidi hata baadhi ya shule zifungwe, Kinacho takiwa ni uwekezaji kwenye Sayansi, MWalimu mmoja anaweza kaaa Dodoma akatoa mafunzo kwa shule zote nchi nzima. Binafisi hata shule za secondary za Kata naona ni kuharibu Aridhi
 
kukusanya wanafunzi wanaotokea katika vijiji kuanzia nane ambao wanaanzia darasa la tatu mpaka darasa la 6 kulinngana na mtaala mpya halafu hao wanafunzi wote wakae bweni wazazi wachangie chakula.
Je katika hiyo shule hawatakuwa wengi kiasi cha kuishinda miundombinu ya shule hizo za kata?

Na kama miundombinu itawatosha unaonaje kama wakisambaza tu katika mashule yaliyopo ili iwatoshee hukohuko makwao?

. Kwa sababu walimu wapo mfano ukichukua walimu 8 kutoka kila shule ukawaweka shule moja kama kata ilikuwa na shule 10 maana yake shule hii maalumu ya kata itakuwa na walimu 80 hapa ufaulishaji na ufundishaji lazima uwe mkubwa
Nimeanza kuliwazia kiundani kiasi wazo lako naona linaweza kujenga uzalendo kiasi fulani. Maana kwa idadi hizo itakuwa ni kama watoto tumewapeleka kambi za jeshi au skauti.
Na nchi zote zenye mshikamano utakuta wananchi wake wengi ni lazima wawe wameishi muda wa kutosha katika mazingira ya kijeshi. Israeli, Marekani, Urusi.... naona imewasaidia. Unapokuta karibu nusu ya wananchi wanasema 'I was with the marine for five years, went on a few tours'.......
 
Back
Top Bottom