DOKEZO Ruvuma: Hali ya Vyoo vya Wanafunzi Shule ya Sekondari NGWILIZI Wilaya ya MBINGA ni mbaya sana

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mkurugenzi mtendaji wa Mbinga mji hali ya vyoo vya shule ya sekondari Ngwilizi ni mbaya sana.

Imefika wakati wanafunzi walio wengi wanaenda kujisaidia vichakani.

Hebu wasaidieni Hawa wanafunzi waweze kusoma kwa raha na waweze kutimiza ndoto zao.

IMG_20230517_182639_270.jpg
IMG_20230517_182632_444.jpg
IMG_20230517_182627_578.jpg
 
Huko kati kati ya miji pambio za "nani kama mama" zinaendelea kurindima kwa kasi kubwa, na kwa bahati mbaya zaidi kwa wananchi viongozi walioteuliwa kwenye nafasi mbali mbali wameamua kua machawa na waimba mapambio badala ya kufanya kazi
 
Yaani ukiangalia mazingira ya vyoo katika ofisi au mazingira ya serikali ni kero tupu, achilia mbali vyuo na hospitali.
Siku moja uongozi wa ARUSHA DC walikuja kukagua usafi shule moja Private. Walipokosa cha kuandika, wakazunguka wee baadaye wakasema Karo la kuoshea linaelekeza maji kwenye open space, hivyo tulipe faini. Walitusumbua, na kuandika faini. Siku moja nikafika kwenye ofisi zinazowatuma hao wapiga faini, nilitamani niwaone niwahoji juu ya fedha waliyochukua. Ofisi zao zilikuwa ni JALALA. Kuanzia nje, mapokezi, Vyoo, ilikuwa uchafu kipeo cha pili. Shame on them.
 
Back
Top Bottom