Hali halisi ya Umasikini Kimkoa Tanzania 2018

Hali halisi ya Umasikini Kimkoa Tanzania 2018

View attachment 1142378
Sijui hawa wanaangukia kwenye fungu gani hapo
Tanzania ya viwanda ifikapo 2025.

1143553
 
Mkuu ukiangalia watu humu wanaandika kishabiki wanaacha uhalisia, mkoa wa Kagera una shida kwenye hizi wilaya za biharamulo na ngara na kwa kwel zipo isolated na wilaya nyingine ndo maana na maendeleo ni duni

Uko isolated vipi?
(i). Wilaya ipi imetengwa na imetengwaje ilhali barabara zipo, umeme upo nk ulitaka nini kifanyike?
 
Uko isolated vipi?
(i). Wilaya ipi imetengwa na imetengwaje ilhali barabara zipo, umeme upo nk ulitaka nini kifanyike?
Ila kuna ukweli Fulani wilaya za biharamulo na ngara zipo nyuma Sana ukilinganisha na wilaya kama Bukoba, misenyi,karagwe na muleba.

Ripoti ya 2012 inaitaja wilaya ya biharamulo kama ya pili Kwa umaskini nchini baada ya kakonko.hivyo inauangusha mkoa wa kagera Kwa ujumla.

Anyway naskia zitaunganika na chato kutengeneza mkoa wa rubondo ndo maana hata na mbuga zimekuwa national park
 
Mkuu hili suala la wilaya moja kuzidi nyingine ni la kawaida hata USA Mississippi iko nyuma ukilinganisha na New York, hapa Dar Ilala inatofautiana na Kinondoni - utofauti huu hausababishwi na eneo kuwa isolated kama mzungumzaji alivyotolea mfano Biharamulo na Ngara bali ni geographic
 
HTujazungumzia wilaya kuzidiana mkuu, hapa tumezungumza wilaya nyingine kuwa kwenye umaskini mkubwa na hivyo kufanya average ya mkoa kuwa mbaya. Kama ni suala la kuzidiana ilo liko wazi maana hata hizo Wilaya zenye hali nzuri bado haziko sawa
 
Uko isolated vipi?
(i). Wilaya ipi imetengwa na imetengwaje ilhali barabara zipo, umeme upo nk ulitaka nini kifanyike?
Mkuu labda huijui jiografia ya mkoa wa Kagera. Shughuli nyingi zinazotajwa katika kuinua mkoa wa Kagera biharamulo na ngara zinahusika kidogo sana, mfano ni shughuli za uvuvi. Ukiangalia biharamulo haina zao maalum la kibiashara kama wilaya nyingine ambazo kuna kahawa, ndizi, miti ya mbao, vanilla n, k
 
wimbi la wageni ndio wanaofanya mkuoa huu kuwa maskini...

na wenyeji ndio wanaofanya mikoa mengine kupata neema ya ukwasi
 
Kwa mujibu wa hizi takwimu Kilimanjaro inaifuatia Dsm licha ya kutokuwa Jiji ni mkoa wa pili kwa ukwasi.

Halafu unakuta nyuzi humu ndani wenyeji wa Kagera ambao ni miongoni mwa mikoa mitano maskini zaidi wakijipambanisha na Kilimanjaro ili hali hata Dodoma hawaifikii...

Hizi ni aibu hizi...
Kilimanjaro hakuna CCM ndio maana kuna maendeleo. Sehemu yeyote ilipojikita CCM basi na umasikini upo wa kutosha!
 
Ukisema unaishi katika shadow ya Arusha ni uongo mkuu! Kumbuka kuna moshi(wilaya) na kilimanjaro (mkoa) sehemu kama rombo, same, mwanga, siha, hai na moshi vijijini hizi zote ni rural areas..... Moshi mjini ina kilometa za mraba 59 tu[emoji23][emoji23] mkuu 59 tu wakati mkoa mzima una kilomita za mraba zaidi ya 17000

Ungepasawa kusema Moshi na sio kilimanjaro
Rural za kilimanjaro eg himo, marangu, mwika kuelekea huko rombo usipime. Ni kuzuri sana, hali ya hewa ni nzuri, watu wake wanajituma sana. Nilikaa marangu wiki moja life la pale nililifurahia sana. Rural nyingine sijui tulikwama wapi
 
Takwimu mbona kama vile zimekaa kimkakati...!! Kilimanjaro hakuna umasikini kwa hiyo hakuna haha ya kufikiriwa katika miradi ya kimaendeleo (developed region). Kwa upande mungine Mkoa wa Lindi (kwa WM), Kanda ya Ziwa (kwa Rais) na Magharibi (kwa waziri wa fedha) kuna umasikini mno na miradi mingi ipelekwe huko.
Hili nalo ni neno.
 
1. Vita ya Kagera
2. Mv Bukoba
3. Virusi vya ukimwi
4. Kuanguka kwa Bei ya kahawa
5. Wakimbizi
6. Uhalifu uliokithiri haswa pori la biharamulo
7. Mnyauko wa migomba ambacho ni chakula kikuu
8. Tetemeko la ardhi
9. Vikwazo vya kielimu na kimiundombinu

And the list is endless

Nitajie mkoa hata mmoja Tanzania ambao umepitia yote haya na bado wakazi wake wakaendelea na maisha yao pasipo utegemezi kwa serikali. Kagera is a home of survivals
acha kujibweteka kwani hao majirani zenu rwanda hawajaguswa na nusu tajwa hapo juu.
vikwazo gani vya kielimu ikiwa karibia kila offisi mkoa wa kagera upo fresh? wanafunzi bora kitaifa wanatokaga kwenu acha siasa kijana
 
Tafadhali mkuu naomba uipitie hiyo comment yako upya; comment yangu iliulizia utaje mkoa mwingine wa Tanzania ambao unaongozwa na serikali yetu na si nchi nyingine. Kwa mantiki hii,ingekuwa ni mtihani bhasi ungepata zero.

Kingine Rwanda ni nchi iliyokumbwa na Genocide ambayo ni mbaya sana lakini ile ni nchi yenye mamlaka kamili na huwezi ukalinganisha na Kagera ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea allocation kutokea serikali Kuu. Pia Rwanda sio Kigali na usiamini sana ile polished angle ya Kigali ambayo mnaruhusiwa kuiona. There's more to see mkuu

Kingine jitahidi kutokukurupuka au kupenda kubisha pasipo kuelewa mkuu,
 
wazungu wanasema "what doesn't kill you makes you stronger".

hongereni sana wahaya kwa kupitia vipindi vigumu na bado mnaendelea ku survive.

Shukrani kwa niaba mkuu.
 
Back
Top Bottom