Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 17,856
- 33,578
Mkuu hapa hatuzungumzii fikra za watu,mitazamo,elimu wala destri bali uwezo wa uchumi wa wananchi kama data za NBS zinavyo elekeza.Njombe bado sana, nimeishi huko, watu Wa Njombe bado wapo nyuma sana kifikra, elimu, kimtazamo na pia hawana maji ya kutosha, vijijini nyumba nyingi Njombe zina funza bado, wanalisi wanawake, na kufuata mila na desturi za ajabu. Faida ya Njombe Ni Mkoa unafikika kwa urahisi kila pande kwa kuwa ni mdogo, hari ya hewa inawarahisishia kulima mazao ya biashara na idadi ndogo ya watu, ambayo ni rahisi kupanga mipango. Njombe itaipita Kilimanjaro Kiuchumi, ila haitakaa muda mrefu, maana Mikoa kama Morogoro, Mwanza siku ikichanganya itakua juu kwa fursa nyingi. Njombe na Kilimanjaro ni kama Qatar, Brunei, na Equatorial Guinea zinafaidika na udogo na uwepo wa fursa.
Pia insu sio udogo wa eneo la kimkoa wala idadi ya watu sababu kuna mkoa kama katavi ni mdogo na ina watu wachache kuliko njombe but bado ni wa mwisho.
Alafu usidhani ninatetea as if mimi ni mwenyeji wa njombe la hasha,nimekaa tu miaka 5 ninachokiongea ninakijua.huko kilimanjaro nimekaa pia kwa mwaka 2 ndio maana bado ninapata ugumu wa kulinganisha kati ya kilimanjaro na njombe.