Hali halisi ya Umasikini Kimkoa Tanzania 2018

kisinja

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
241
295
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Imetoa taarifa kama inavyoonekana

Screenshot_20190629-183621~2.png

7A2DC4BC-DDE3-493E-803A-1D75F7DD771F.jpeg

Na chini ni TAKWIMU RASMI ZA HALI YA UCHUMI TANZANIA BARA 2012-2018
Screenshot 2019-06-30 at 06.55.25.png

KWA UJUMLA:

Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2015, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017.

Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli, na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo.

Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na:
Sanaa na Burudani iliyokua kwa asilimia 13.7;
Ujenzi (asilimia 12.9);
Uchukuzi na Uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na
Habari na Mawasiliano (asilimia 9.1).
 
Attachments

  • KITABU CHA HALI YA UCHUMI WA TAIFA KATIKA MWAKA 2018.pdf
    3.2 MB · Views: 71
Wasukuma wanaongoza kwa umasikini. Walichokijua ni kuzaana badala ya kuzalisha. Wabadilike. Mwanza, Simiyu, Geita ni maeneo yanayotia huzuni.
Ila pongezi nyingi ziende kwa Magufuli. Inaonekana kiwango cha umasikini (Adject poverty) kimepungua sana hasa kwa mikoa kama ya Kigoma ambayo kwa takwimu zilizopita umasikini ulikuwa kwenye 45%. Mikoa mingi yenye 35% kwenye riport iliyopita ilikuwa kwenye 40 something. Riport hii inatia matumaini kama ni ya kweli.
 
Rating ya umasikini hi focus katika viashiria 3 kiashiria cha kwanza ni shelter je wananchi wana makazi ya aina gani hasa vuiijini,wanalala vipi nyumba zao ni imara,2 chakula je wakazi hao wanao uwezo wa kula milo 3 kifungua kinywa,mchana na chakula cha usiku 3 social services muhimu kama maji,shule na afya ,Lakini tukifanya rating kwa kuangalia pato la sehemyu husika GDP TU gross domestic product tutabaki kudanganyana resources kama madini,gas,mafuta vyaweza kupatikana sehemu husika lakini wananchi wa sehemu hizo wanabaki masikini hawanufaiki na rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Imetoa taarifa kama inavyoonekana

Ebwana eeh hawa ndugu zetu wa Kagera na kujisifu kote huko Bado mkoa wao ni maskini kiasi hichi ?

Mkoa wa kagera unapata mvua za kutosha, wapo karibu na nchi kama Rwanda na Burundi plus kuna Ziwa victoria na mto kagera hivyo shughuli za uvuvi , kilimo n.k zinashamiri kwa urahisi!!

Hawa ni wavivu au kuna shida gani ?

Wanapitwa na mikoa yenye ukame kama Singida na Dodoma kweli?

Sasa kwa hali hiyo hao wenyeji wa Kagera wangekuwa mikoa mikame nusu jangwa si ingekuwa aibu zaidi....
 
Kwa mujibu wa hizi takwimu Kilimanjaro inaifuatia Dsm licha ya kutokuwa Jiji ni mkoa wa pili kwa ukwasi.

Halafu unakuta nyuzi humu ndani wenyeji wa Kagera ambao ni miongoni mwa mikoa mitano maskini zaidi wakijipambanisha na Kilimanjaro ili hali hata Dodoma hawaifikii...

Hizi ni aibu hizi...
 
1. Vita ya Kagera
2. Mv Bukoba
3. Virusi vya ukimwi
4. Kuanguka kwa Bei ya kahawa
5. Wakimbizi
6. Uhalifu uliokithiri haswa pori la biharamulo
7. Mnyauko wa migomba ambacho ni chakula kikuu
8. Tetemeko la ardhi
9. Vikwazo vya kielimu na kimiundombinu

And the list is endless

Nitajie mkoa hata mmoja Tanzania ambao umepitia yote haya na bado wakazi wake wakaendelea na maisha yao pasipo utegemezi kwa serikali. Kagera is a home of survivals
 
Kwa mujibu wa hizi takwimu Kilimanjaro inaifuatia Dsm licha ya kutokuwa Jiji ni mkoa wa pili kwa ukwasi.

Halafu unakuta nyuzi humu ndani wenyeji wa Kagera ambao ni miongoni mwa mikoa mitano maskini zaidi wakijipambanisha na Kilimanjaro ili hali hata Dodoma hawaifikii...

Hizi ni aibu hizi...
Kilimanjaro ilitakiwa iwe CITY.. Mji mdogo ambao haujawahi pata misukosuko ya aina yoyote , una rasilimali kibao na fursa za utalii zilizopo nje nje. Rasilimali watu iliyopo exposed ya kutosha and yet unaishi katika shadow ya Arusha.

Mji ambao una population density ya kutosha, Hali ya hewa nzuri na ardhi yenye rutba na bado Ni beautiful residential town ambayo inacheza na league za Moro. What a shame
 
Back
Top Bottom