Hali halisi ya Umasikini Kimkoa Tanzania 2018

Hali halisi ya Umasikini Kimkoa Tanzania 2018

Ebwana eeh hawa ndugu zetu wa Kagera na kujisifu kote huko Bado mkoa wao ni maskini kiasi hichi ?

Mkoa wa kagera unapata mvua za kutosha, wapo karibu na nchi kama Rwanda na Burundi plus kuna Ziwa victoria na mto kagera hivyo shughuli za uvuvi , kilimo n.k zinashamiri kwa urahisi!!

Hawa ni wavivu au kuna shida gani ?

Wanapitwa na mikoa yenye ukame kama Singida na Dodoma kweli?

Sasa kwa hali hiyo hao wenyeji wa Kagera wangekuwa mikoa mikame nusu jangwa si ingekuwa aibu zaidi....
asilimia kubwa ya sisi watanzania ni "wavivu" hilo halina ubishi, kagera hakuna njaa, ndizi kibaao singida kuna njaa ndo maana wanajibiidisha otherwise unaweza kufa njaa - ila watu hao hao wanaotokea kwenye ukame ukiwapeleka kwenye ardhi zenye rutuba na mvua za kutosha kunakuwa na comfort zone kwao so hawatajibidiisha sana, kingine ni mifumo, huko kagera (na kilimanjaro) walikuwa wakulima wazuri sana wa zao la buni (kahawa) zamani sio kama sasa hivi viwango vimepungua, enzi hizo ukienda kilimanjaro familia kibao miti ya kahawa tu raha sana, ukienda pia kagera na mbeya ilikuwa hivyo ila naona watu walichoshwa na vuta nikuvute ya vyama vya ushirika, hizo ndo sababu zimewachosha wakulima wakageukia mazao mengine, mfano angalia pamba ilivyosuasua
 
1. Vita vya kagera vinaizuiaje kagera kuendelea ili hali vita Vimepiganwa miaka 40 iliyopita, isitoshe athari zilikuwa kwa nchi nzima!!

2. Mv Bukoba??... Mv Bukoba imeizuiaje kagera kuendelea ni Sawa na watu wa Dodoma wakwambie ajali ya treni ya Dodoma inazorotesha mkoa kuendelea au kufika mbali zaidi.

3. Kagera sio mkoa unaongoza kwa maambukizi ya ukimwi, mkoa wa njombe zamani iringa Ndio vinara wa maambukizi na wamekuwa wakishikilia hii title kwa muda mrefu Hata kama ukimwi ulitokea huko, hivyo kisingizio hakina maa hiko

4. Sasa kama hii Ndio sababu na mkoa wa Kilimanjaro usingekuwa wa pili kwa ukwasi isitoshe moja ya mazao tegemezi kilimanjaro ni kahawa tokea enzi za ukoloni.

5. Kigoma wasemaje Sasa kama mnalalamikia wakimbizi, isitoshe wakimbizi ni fursa

6. Haina mashiko, uhalifu unafanyika sana Arusha kushinda hapo Kagera

7. Mnyauko haupo kagera tuu Bali hata Kilimanjaro Ila kagera imebaki kuwa maskini

8. Acha utani mkuu kile kitetemeko cha juzi ndicho kifanye kagera kuwa miongoni mwa mikoa 5 maskini zaidi .. umesahau kuwa kabla ya hilo tetemeko kagera ilikuwa ya pili kwa umaskini.

9. Vikwazo vya kielimu kivipi ili hali wahaya wenyeji wa kagera ni moja ya jamii zilizoelimika zaidi TANZANIA!!

Kimsingi hizi sababu zote hazina mashiko uzijumlishe zote kwa pamoja au moja moja hazishawishi kabisa eti mkoa uko karibu na nchi 3 , mvua za kutosha, wasomi kibao ziwa kubwa , mto mkubwa n.k bado uwe miongoni mwa mikoa maskini zaidi TANZANIA...
hahaha takwimu zimepikwa...
 
Na sisi wa Njombe ni wa 3 baada ya Kilimanjaro. Hiyo naamini. Njombe hata ukienda vijijini ni nadra sana kuona nyumba za tope, miti au zilizoezekwa kwa nyasi. Ni maeneno machache sana. Hakuna matajiri wa kupindukia lakini pia hakuna maskini wa kupindukia.

Arfhi nzuri, mvua za kutosha na bidii kubwa ya watu ya kufanya kazi, vinachamgia sana. Tumeharibiwa uchumi katika awamu hii. Soko la mbao zetu nchini Kenya limekuwa la kusuasua kutokana na yale matendo ya kishetani yankuchoma vifaranga na kupora ng'ombe wa Wakenya.

Soko la mahindi nchini Zambia liliharibiwa na watawala baada ya kutangaza kuwa yasipelekwe nje. Kwa ujumla kwa wananchi wa Njombe, utawala wa awamu hii umekuwa wa kuharibu maendeleo badala ya kuwezesha maendeleo.

Awamu hii, kumbukumbu kubwa kwetu ni ya mabaya kuliko mema.
na bado 2020 mtawapigia kura wale wale
 
Hivi kagera kuna mmbunge kutoka upinzani ?
kwani Wilfred Lwakatare ni wa chama gani kama sio CHADEMA - haya mavyama yenu yanatuletea gozi gozi tu badala ya kuadili mambo ya maana watu wamekalia vyama vyama vyama
 
Mkoa wa Kagera sio masikini pamoja kuwa isolated hasa katika miondombinu hasa ya usafiri wa majini.Ukosefu wa meli za MV victoria ya Abiria na MV Umoja YA MIZIGO umesababisha maisha ya mkoa huu kuwa ghali.

Msafiri wa barabara uwanufaisha wale wenye magari ya matera na mabasi huku bei za vitu vinapanda kila kukicha kutokana usafirishaji wa bidhaa mbali mbali.Hata hivyo wananchi wa Kagera wanazikabili changa moto mbali mbali ni nadara sana kuona mwananchi wa Kagera analala kwenye nyumba iliyoezekwa na nyasi au tope wengi wananchi wa Kagera wana makazi mazuri.

Walio wengi wanamudu kula milo 3 ya chakula hata mavazi yao yanapendeza ingawa wengi wao Mitumba ndio mkombozi wao.

Rating ya Umaskini kwa kuangalia GDP YA MKOA haitoshi maana mugawanyo wa mapato yanayopatikana na rasilimali za mikoa mara nyingi unufaisha wale wenye kumiliki resources hizo sio mwananchi wa kawaida mmoja mmoja
Ninaafikiana na maoni yako. Mojawapo ya vyanzo vikubwa vya mapato ya kagera ni diaspora remittances. Wazawa wengi wa mkoa huu hutuma pesa nyingi kwao ambazo husaidia kuboresha standard of living za wakazi ingawaje kwa bahati mbaya si kwa viwango vikubwa vya uwekezaji ktk ujenzi wa vitega uchumi. Ukuaji wa maendeleo ya kagera ktk kipindi cha miaka michache ijayo utakuwa wa haraka zaidi baada ya ujenzi wa meli ktk ziwa victoria kukamilika, bomba la mafuta toka uganda, na muhimu zaidi ukamilishaji wa miradi ya stendi ya mabasi, soko kuu na chuo cha veta kinachojengwa kwa msaada wa china. Kagera ipo strategically located kwa maendeleo kwa hiyo wenyeji wasijione dhaifu na kwa msukumo wa serikali ya awamu ya 5 yajayo yanafurahisha.
 
Ebwana eeh hawa ndugu zetu wa Kagera na kujisifu kote huko Bado mkoa wao ni maskini kiasi hichi ?

Mkoa wa kagera unapata mvua za kutosha, wapo karibu na nchi kama Rwanda na Burundi plus kuna Ziwa victoria na mto kagera hivyo shughuli za uvuvi , kilimo n.k zinashamiri kwa urahisi!!

Hawa ni wavivu au kuna shida gani ?

Wanapitwa na mikoa yenye ukame kama Singida na Dodoma kweli?

Sasa kwa hali hiyo hao wenyeji wa Kagera wangekuwa mikoa mikame nusu jangwa si ingekuwa aibu zaidi....
Hata Mimi nimeshangazwa Sana duu! Dodoma imeipita RUKWA, KAGERA Mhhhh!
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Imetoa taarifa kama inavyoonekana

View attachment 1142323

View attachment 1143342

Na chini ni TAKWIMU RASMI ZA HALI YA UCHUMI TANZANIA BARA 2012-2018
View attachment 1142638

KWA UJUMLA:

Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2015, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017.

Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli, na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo.

Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na:
Sanaa na Burudani iliyokua kwa asilimia 13.7;
Ujenzi (asilimia 12.9);
Uchukuzi na Uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na
Habari na Mawasiliano (asilimia 9.1).
1. Vita ya Kagera
2. Mv Bukoba
3. Virusi vya ukimwi
4. Kuanguka kwa Bei ya kahawa
5. Wakimbizi
6. Uhalifu uliokithiri haswa pori la biharamulo
7. Mnyauko wa migomba ambacho ni chakula kikuu
8. Tetemeko la ardhi
9. Vikwazo vya kielimu na kimiundombinu

And the list is endless

Nitajie mkoa hata mmoja Tanzania ambao umepitia yote haya na bado wakazi wake wakaendelea na maisha yao pasipo utegemezi kwa serikali. Kagera is a home of survivals

Politix tuuu, mambo yote iko Kilimanjaro kwa kina Mangi ambao ni ATM ya Nchi. Na hata hiyo Dar es Salaam zaidi ya 50% utakuta ni importation ya utajiri kutoka Kilimanjaro kwa kina Massawe. Hakuna kutafuta sababu za ajabu ajabu.
 
Mikoa mingine muige mfano wa njombe hawana maneno ya kwenye kanga wanapiga kazi tu.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Imetoa taarifa kama inavyoonekana

View attachment 1142323

View attachment 1143342

Na chini ni TAKWIMU RASMI ZA HALI YA UCHUMI TANZANIA BARA 2012-2018
View attachment 1142638

KWA UJUMLA:

Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2015, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017.

Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli, na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo.

Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na:
Sanaa na Burudani iliyokua kwa asilimia 13.7;
Ujenzi (asilimia 12.9);
Uchukuzi na Uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na
Habari na Mawasiliano (asilimia 9.1).
 
Usiangalie Arusha mjini na Arumeru tu.
Huko Arusha vijijini hali mbaya ktk wilaya zake zingine.
Ndio hivyo watu wanafikiria mini badala ya mikoa. Kimaendeleo ya makazi sio ajabu Tanga kuizidi Arusha.

Kama ulivyosema ukiacha Arusha na Arumeru kwingine hali sio kutokana na jamii za ufugaji.
 
Wabunge wa upinzani wamezidi kuiongezea umaskini Arusha.
 
Ninaafikiana na maoni yako. Mojawapo ya vyanzo vikubwa vya mapato ya kagera ni diaspora remittances. Wazawa wengi wa mkoa huu hutuma pesa nyingi kwao ambazo husaidia kuboresha standard of living za wakazi ingawaje kwa bahati mbaya si kwa viwango vikubwa vya uwekezaji ktk ujenzi wa vitega uchumi. Ukuaji wa maendeleo ya kagera ktk kipindi cha miaka michache ijayo utakuwa wa haraka zaidi baada ya ujenzi wa meli ktk ziwa victoria kukamilika, bomba la mafuta toka uganda, na muhimu zaidi ukamilishaji wa miradi ya stendi ya mabasi, soko kuu na chuo cha veta kinachojengwa kwa msaada wa china. Kagera ipo strategically located kwa maendeleo kwa hiyo wenyeji wasijione dhaifu na kwa msukumo wa serikali ya awamu ya 5 yajayo yanafurahisha.
Labda ndo maana umetoka top three na kuwa wa kumi na moja sasa
 
Watu wengi kumbe hawajui kuchambua takwimu na kuzingatia jinsi taarifa zilivyopatikana na kutathmini uhalisia.
 
Mikoa mitano?

Hebu tazama takwimu vzr Kwanza.

Asilimia ni 31.

Hata haipo top ten Acha kukurupuka mkuu

Lakini pia Kagera ndo mkoa wa tatu Kwa idadi ya watu nchini vip mbona watu wanapenda kukaa kwenye mkoa wa maskini? Kama unavyoainisha wew.

Kimpangilio sasa mikoa maskini ni

1.Rukwa 45%
2.simiyu 39%
3.lindi37%
4.Geita37%
5.mwanza36%
6.kigoma35%
7.Tabora34%
8nk

Kagera ya 11 huko

Tulia usome takwimu vzrView attachment 1142522
Doesnt matter,.. Kagera ni POOR/Masikini . Period**
 
Wachagga wapo humu wanapiga kelele eti wahaya masikini, nani kawaambia kagera ni kwa wahaya tu?? Pamoja na hizi data niseme kwamba wilaya za wahaya zipo juu kimaendeleo. Ukizunguka bukoba, muleba, misenyi na huko karagwe watu wana maisha mazuri. Kagera kama mkoa una kazi kubwa ya kufanya kwa wilaya za biharamulo na ngara maana huku ndo umaskini umejikita
Niwapongeza wahaya wanavyojenga kwao sasa hivi wilaya kama karagwe na misenyi hazikamatiki aisee
MMM Kwa Muleba nooo please ,sehemu kubwa ni visiwa na zipo familia za wavuvi wanaishi Maisha ya kimaskini sana .Nilishiriki na halmashauri kutambua watoto wanaoishi mazingira magumu (Muleba DC) was among council with Most vulnerable children(MVC) na hii ni moja ya indicator ya umaskini
 
Singidani itabaki kuwa juu vuna magunia yako 5 ya mahindi ambayo yanakuwa sawa na gunia 1 la vitunguu vya Singida vyenye viwango vya dunia!
 
Jamani hizi takwimu sio za kupambana nani maskini nani Tajiri.Tuangalia kwa fursa Zaidi.Mkoa wenye hali nzuri it means ukiwekeza mzunguko wa hela uko vizuri Zaidi na hata miundombinu iko vizuri kulinganisha na labda na hizo zilizokuwa za mwisho.Mikoa iliyo mwisho ,nazo kuna ffursa zinazopatikana kama maeneo mampya ya uwekezaji,kupata rasilimali watukwa uraisi ukianzisha kitu kama kiwanda au uzalishaji na kupeleka kuuza mikoa iliyokaa vizuri.Mi bado nachambua report kwa minajili ya ku invest na kuangalia fursa kwa mapana.Labda kwa sababu mimi mchagga aisee hizi takwimu ni muhimu naendelea kuzichambua kwa ajili ya fursa.Uzuri nimeshafika mikoa yote bara na visiwani isipokuwa rukwa tu.
 
Back
Top Bottom