Njombe bado sana, nimeishi huko, watu Wa Njombe bado wapo nyuma sana kifikra, elimu, kimtazamo na pia hawana maji ya kutosha, vijijini nyumba nyingi Njombe zina funza bado, wanalisi wanawake, na kufuata mila na desturi za ajabu. Faida ya Njombe Ni Mkoa unafikika kwa urahisi kila pande kwa kuwa ni mdogo, hari ya hewa inawarahisishia kulima mazao ya biashara na idadi ndogo ya watu, ambayo ni rahisi kupanga mipango. Njombe itaipita Kilimanjaro Kiuchumi, ila haitakaa muda mrefu, maana Mikoa kama Morogoro, Mwanza siku ikichanganya itakua juu kwa fursa nyingi. Njombe na Kilimanjaro ni kama Qatar, Brunei, na Equatorial Guinea zinafaidika na udogo na uwepo wa fursa.