Jamani wakati ni huu, Vijana wa vyuo hawana mikopo, pia wamachinga wanaonewa, wanateswa
Watanzania tuungane, tuwasaidie hawa wamachinga. Hawa wamachinga ni vijana wenzetu, ni dada zetu, kaka zetu na watoto wetu.
Hawa wamachinga wamekuwa wabunifu, wanajishughulisha, jamani mnataka wawe majambazi?
Ardhi ya kulima iko wapi? wawekezaji, mafisadi na vig o go wamegawana ardhi kubwa kubwa. Vijana wametelekezwa, wafanye kazi gani?
Wanaharakati, watetea haki za binadamu na watanzania wote tunaopenda haki. Tuungane ili tutoe matamko, tuikemee serikali na tufanye maandamano ya amani.
Vijana wa Vyuo vikuu nao wanateswa, vijana wanataka elimu iwakomboe ila serikali inawatesa. Hela za dowans, sherehe za uhuru ila hela za kuwaendeleza vijana wetu hakuna?
Kweli hakuna haja ya amani ya kinafiki wakati haki tanzania haipo tena.
Sasa cha kufanya ni kuungana mikoa yote, Arusha, Mwanza, Moshi, Mbeya, shinyanga, Bukoba ili tuandamane bila kujali dini, siasa au kipato.
Tuhamasishane kwa kutumia simu, kila mtu amtumie rafiki, ndugu ujumbe huu hapa chini.
-- Pinga uonevu, tetea vijana wa Tanzania, tuunganishe nguvu katika maandamano ya amani ili serikali isikie. Sasa kila mmoja wetu afike katika uwanja wetu wa mikutano. Wote tunataka tanzania yenye vijana wanaostawi, hatutaki wezi, na machangu doa--