Hakuna pesa rahisi wakuu

Hakuna pesa rahisi wakuu

650

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
200
Reaction score
291
Wakuu habari Zenu

Dah wimbi kubwa la vijana tumekuwa tunapenda matokeo ya haraka sanaaa yaan boom baah 💥

Manoti hayooo

Hii kitu inapelekea baadhi ya vijana 😂 kutumia fursa hii ya vijana tupendao matokeo overnight kupiga pesa

Wanafungua platform wanaipromote mitandaon kwamba ukijiunga unapata kiasi fulan kila siku

Kijana ukipiga hesabu
Niwape 14,500/- kwa siku napata 2000/- nikifanya task fulan kwenye platform yao

By wiki moja Hela yangu hiyoo

Siku zinazofuatia nakula faida tuuu 😂

Bila kujua ww ndo unayelengwa especially hiyo pesa yako ya kuanzia (kianzio)

Wengi wao masharti na vigezo vyao vinakua havipo clear yaan unakuja kujiunga ushwapa Hela ndo unaambiwa ukitaka kutoa mpaka ufikishe kiasi fulan

Tena mchakato wa kutoa unakua mgumuuu kuliko hata kudeposit pesa

Haya na Ili upate pesa nyingii ualike wengine wengiiii


vijana wenzabgu wa jf tuwe makini hakuna pesa rahisi kiiivyo.
 
Na mara nyingii zinakua sio guarantee mda wowote zinazimwaaaaaa

Yalinikutaaa Hela yangu ilienda yote sikuambulia hata miaaaaa
 
wanabadili tu mbinu ila utapeli ni uleule miaka nenda rudi! tutafute namna ya kuelekeza hizi nguvu zetu kwingine tunaonekana ndio wajinga, wakitaka kutupiga wanaanza na sisi! Africa!🙁
 
wanabadili tu mbinu ila utapeli ni uleule miaka nenda rudi! tutafute namna ya kuelekeza hizi nguvu zetu kwingine tunaonekana ndio wajinga, wakitaka kutupiga wanaanza na sisi! Africa!🙁
Yaan
 
Wanyabi tunafanya hivi...

Unamshawishi yule anaekushawishi akulipie pesa ya kiingilio na wewe utamlipa baadae maana uko vibaya ila onesha interest ya kuingia hiyo platform.

Nishakula pesa za bure kwa ishu za namna hiyo mara 3, wale walionishawishi walinipa mtaji na nikala faida kabla hazijafungwa.
 
Back
Top Bottom