Hakuna Mgao wa Umeme Tanzania...

Hakuna Mgao wa Umeme Tanzania...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,188
Reaction score
44,142
Hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme. Kama huamini rudia tena mawazo haya hadi ujishawishi kuwa unachoshuhudia ni kitu kingine zaidi ya mgao wa umeme. Kwanini hakuna mgao wa umeme? Kwa sababu walisema hakutakuwepo mgao wa umeme tena, mgao wa umeme utakuwa historia. Kwa hiyo kinachotokea ni historia tu ya mgao wa umeme ulivyokuwa; wanatumia nafasi hii kuwakumbusha historia ya mgao wa umeme msije mkasahau.

Na hakuna namna nzuri ya kuwakumbusha watu kuhusu tukio la nyuma kama kwa kutumia 'mfano halisi'. Kwa hiyo, wale waliokuwa wamesahau au ambao hawajui mgao basi hii ni namna nzuri ya kukumbuka. Hiki ndicho alichokisema Waziri Yule kuwa mgao wa umeme utakuwa ni "historia".

SICHO HICHO

Hiki kilichoko sicho, hiki sicho kilichoko,
Ndicho hiki hichohicho, ndicho hiki hakiko,
Hiki ni kile si hicho, kile kisichokuwako
Hakuna cha mgao, kilichoko ni historia;
Ya mgao!

Aliyesema hakiko, kwamba hakitakuwapo,
Yeye mwenyewe hayuko, alichosema hakipo,
Huyu bwana yuko yuko, kama popo mwenye pepo,
Hakuna cha mgao, kilichoko ni historia;
Ya mgao!

Wanachogawa hakipo, kwani kisingekuwepo,
Ugawe vipi hakipo, hakipo huko mlipo,
Kama wafuata upepo, ndugu zangu mpo mpo,
Hakuna cha mgao, kilichoko ni historia;
Ya Mgao!

Cha nini hki cha nani, kwanini tena ni nini?
Tutamuuliza nani, kinaendelea nini?
Tunakuwa kama nyani, kujenga nyumba mtini!
Hakuna cha mgao, kilichoko ni historia;
Ya Mgao!

Tukubalini watani, janja ya jiwe ya nini?
Hili jambo siyo geni, linarudia kwa nini?
Ahadi zao jamani, twaamini kama dini!
Hakuna cha mgao, kilichoko ni historia;
Ya Mgao!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Mi nilidhani baada ya Profesa kuteuliwa kuwa waziri tatizo lingekwisha.

Manake huyo Profesa ni msomi, ni kichwa, mwenye kipaji maalum, na mengineyo mengi.

Sasa iweje tena leo kuna mgao? Profesa msomi atashindwaje kuleta umeme wa uhakika bana?

Haiwezekani kabisa. Hakuna mgao wa umeme Tanzania.
 
CCM ni washari wametufinyanga kiakili wanatumia propaganda kwenye maisha ya watu mgao upooooooooooooooo tena kwa nguvu zote kuna maeneo hawajaona umeme hata tone kwa siku nne mfululizo ndio waisema hata wakiongopa wanajali hakuna wakuwawajibisha
 
Huyu professor simkubali kabisa.. Ni muongo

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Mambo ya kizembe kama haya yapo Tanzania tu duniani kama yalivyo madini ya Tanzanite. Ni jambo ambalo linajulikana kabisa kila baada ya muda fulani visima vya Songosongo vitafanyiwa matengenezo lakini hatujipangi kwa hilo.

Na safari hii wameua nyani kabisa kitu kinapigwa 24hrs. Ni Tanzania tu mgao kama huu unawezekana na watu wakawa wanacheka au kunung'unika bila kuchukua hatua.
 
Huyu professor mwenye kutukana watu tu, hata tuliomuajiri?
 
Tungelikuwa nchi makini inayosisitiza katika UWAJIBIKAJI, huyu 'bwana umeme' wa sasa, alipaswa kuwa ameshawajibika au kuwajibishwa siku nyingi sana, hasa kwa UONGO! Huyu mtu ni muongo muongo muongo unakuwa muongo kisha unaongezea na 'intellectual arrogance'.

Kama usingekuwa uongo, basi angeshawajibika kwa mambo kama haya. Anyway, acha watu kama hawa wazidi kuonesha na kudhihirisha kuwa sera za CCM zimeshindwa na zinazidi kushindwa. Wacha wazidi kuwaonesha Watanzania kuwa mabadiliko yako nje ya CCM na wakati wenyewe ni huu.

Hakuna tatizo hata moja linalosumbua Watanzania sasa hivi ambalo halina uhusiano na UFISADI wa status quo!
 
Hakika wema na fadhili zitatufwata siku zote za maisha yetu siku tukianza kudai watekeleze yale wayasemayo.
 
Watanzania wamezoea matatizo hivyo hata matatizo kama haya ya mgao wa umeme tunachukulia kama misiba mingine tu!

Hakuna mgao wa umeme Tanzania na mgao utabaki historia.
 
Huyu professor mwenye kutukana watu tu, hata tuliomuajiri?

The best thing he (representing the failing govt and falling political party) can offer to the Wananchi. Mwache aendelee kutukana. Hao hao anaowatukana ndiyo anataka awaongoze na 'kesho' wamwelewe aendelee kuwa kiongozi.

Wakati wengine wanatukana live, wengine wanatukana kirejareja kwa kujifanya wanawajali waalimu na wakulima leo, wakati masuala yote yanapitia kwenye vikao wanavyoviandaa, kuviendesha na kusimamia utekelezaji wake.

Wengine wanatishia kuua raia, wanakiri kuhujumu uchumi kwa shughuli haramu na kutamba serikali haiwezi kufanya lolote dhidi yao. A good sign of
 
Profesa Muhongo muongo, aka mjivuni, mjua kila kitu, jeuri, mwenye dharau, mwenye ghiliba na mzalendo kwa wawekezaji wa kizungu....ni maneno gani utakayotumia kufuta maneno yako kuwa hakutakuwa na mgao tena? Wahenga walisema usiwatukane mamba kabla hujavuka mto
 
But seriously, hivi kuna mtu aliamini kweli mgao sasa utakuwa historia?
 
Tunavuna matunda ya Serikali ya CCM kwa kuwa madarakani kwa miaka hamsini halafu wanazunguka nchi nzima eti Chadema hawajafanya uchaguzi, Katiba ya Chadema ina matatizo, eti Mbowe hafai kuwa M/Kiti wa Chadema na kuendela...

Ukiwauza Mambo ya Umeme na Rasilimali za Nchi wanatokwa na Povu, na kuna makada wao kila siku utasikia jitambue eti kwa kuishabikia chama ambacho kimetufikisha hapa, Miaka saba ijayo hatutakuwa na dhahabu, Tembo watakuwa wameisha kwenye hifadhi maana ndugu zao waachina wamewapa sumu ambayo akipewa tembo penzo zinanyofoka tu bila kutumia nguvu sana.

Bado wanasema tujitambue, kuna mavuvuzela kibao yanazunguka nchi nzima eti kuelimisha wananchi waichague CCM kwa lipi???

Elimu wameiuwa, Afya hakuna Kitu, Nishati na Umeme tabu huku Gesi inachukuliwa bure.
 
Mgawo huu wa umeme ni wa ufisadi wa kimikataba Songosongo/PAT na udhaifu wa Mpango wa Dharura wa Umeme; Bungeni Muhongo alinijibu uongo.

Mgawo wa Umeme ufisadi wa PAT na udhaifu wa ukarabati wa visima ulijulikana toka Julai na Novemba 2011; Prof Muhongo alisema uongo kuficha.

Trilioni 1 ilitumika kuficha uongo wa Prof Muhongo Mgawo wa Umeme kwenye manunuzi ya mafuta mazito; Ufisadi, PAT, visima, gesi umemshinda.

MgawowaUmeme Prof Muhongo alisema uongo mara 2 bungeni; 1. 28 Julai 2012 baada ya kumhoji kwenye hotuba 27 JulJOHN MNYIKA: HOTUBA YA KAMBI RASMI YA UPINZANI; WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Uongo wa mara ya 2 wa Prof Muhongo bungeni kuhusu MgawowaUmeme ni wa Mei 23 nilipohoji baada ya hotuba ya 22 Mei:JOHN MNYIKA: HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI JOHN JOHN MNYIKA (MB) KUHUSU MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA

Halafu kwa maagizo ya IMF/WB wanataka kupandisha bei ya umeme kufidia ufisadi kukodi mitambo ya dharura/ununuzi mafuta na mikataba mibovu.

Source; John Mnyika facebook account

 
Zamani nikisikia mtu ni Profesa huwa namchukulia sio mtu wa kawaida.
Nilikuwa naamini upeo wao ni hali ya juu sana. Kamwe hawafanyi upuuzi puuzi.
Lakini tangu huyu Waziri atumikie hii nafasi na kauli zake alizokuwa anazitoa, na hivi karibuni yule mbunge wa Urambo wamefanya niwe na mtazamo tofauti kabisa na ule niliokuwa nao.
 
Back
Top Bottom