FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,802
Hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme. Kama huamini rudia tena mawazo haya hadi ujishawishi kuwa unachoshuhudia ni kitu kingine zaidi ya mgao wa umeme. Kwanini hakuna mgao wa umeme? Kwa sababu walisema hakutakuwepo mgao wa umeme tena, mgao wa umeme utakuwa historia. Kwa hiyo kinachotokea ni historia tu ya mgao wa umeme ulivyokuwa; wanatumia nafasi hii kuwakumbusha historia ya mgao wa umeme msije mkasahau.
Na hakuna namna nzuri ya kuwakumbusha watu kuhusu tukio la nyuma kama kwa kutumia 'mfano halisi'. Kwa hiyo, wale waliokuwa wamesahau au ambao hawajui mgao basi hii ni namna nzuri ya kukumbuka. Hiki ndicho alichokisema Waziri Yule kuwa mgao wa umeme utakuwa ni "historia".
Unajitekenya mwenyewe unacheka mwenyewe.
Unajuwa maana ya utakuwa? unajuwa miradi mingapi ya umeme ambayo inatekelezwa kwa sasa?
Nilikwambia wewe huku hapakufai wewe panakufaa kwenye udaku na ufataani.