Hakuna Mgao wa Umeme Tanzania...

Hakuna Mgao wa Umeme Tanzania...

duuuh!!!!! kweli nimeamini duh!!!

Watanzania wamezoea matatizo hivyo hata matatizo kama haya ya mgao wa umeme tunachukulia kama misiba mingine tu!

Hakuna mgao wa umeme Tanzania na mgao utabaki historia.

But seriously, hivi kuna mtu aliamini kweli mgao sasa utakuwa historia?

hongera sie siku ya 4 hatujauona

Peofesa muhongo muongo, aka mjivuni, mjua kila kitu, jeuri, mwenye dharau, mwenye ghiliba na mzalendo kwa wawekezaji wa kizungu....ni maneno gani utakayotumia kufuta maneno yako kuwa hakutakuwa na mgao tena? Wahenga walisema usiwatukane mamba kabla hujavuka mto
Katuni%2BNov%2B23.jpg

Katuni.jpg

katuni+majir+27.7.11.jpg
 
Mambo ya kizembe kama haya yapo Tanzania tu duniani kama yalivyo madini ya Tanzanite. Ni jambo ambalo linajulikana kabisa kila baada ya muda fulani visima vya Songosongo vitafanyiwa matengenezo lakini hatujipangi kwa hilo.

Na safari hii wameua nyani kabisa kitu kinapigwa 24hrs. Ni Tanzania tu mgao kama huu unawezekana na watu wakawa wanacheka au kunung'unika bila kuchukua hatua.

Yaani acha kabisa inakera sana vile kwao wanao hawajui adha tunayopata......haitoshi juzi kwenye PB wanatangaza wanataka kuongeza gharama unit 1 =198 mpya 1= 336 watapandisha kwa 67% kubinafsisha hawataki huku hawana mipango thabiti ya kuondokana na matatizo......najiuliza wataendelea kutunyonya kwa kutumia hili shirika hadi lini
 
Mgawo huu wa umeme ni wa ufisadi wa kimikataba Songosongo/PAT na udhaifu wa Mpango wa Dharura wa Umeme; Bungeni Muhongo alinijibu uongo.

Mgawo wa Umeme ufisadi wa PAT na udhaifu wa ukarabati wa visima ulijulikana toka Julai na Novemba 2011; Prof Muhongo alisema uongo kuficha.

Trilioni 1 ilitumika kuficha uongo wa Prof Muhongo Mgawo wa Umeme kwenye manunuzi ya mafuta mazito; Ufisadi, PAT, visima, gesi umemshinda.

MgawowaUmeme Prof Muhongo alisema uongo mara 2 bungeni; 1. 28 Julai 2012 baada ya kumhoji kwenye hotuba 27 JulJOHN MNYIKA: HOTUBA YA KAMBI RASMI YA UPINZANI; WIZARA YA NISHATI NA MADINI


Uongo wa mara ya 2 wa Prof Muhongo bungeni kuhusu MgawowaUmeme ni wa Mei 23 nilipohoji baada ya hotuba ya 22 Mei:JOHN MNYIKA: HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI JOHN JOHN MNYIKA (MB) KUHUSU MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA

Halafu kwa maagizo ya IMF/WB wanataka kupandisha bei ya umeme kufidia ufisadi kukodi mitambo ya dharura/ununuzi mafuta na mikataba mibovu.

Source; John Mnyika facebook account

Kuna jamaa wa Tanesco katutonya kuwa wanadaiwa na makampuni yanayozalisha umeme, kama Tanesco hawalipi jiandaeni kununua vibatari.
 
Mi nilidhani baada ya Profesa kuteuliwa kuwa waziri tatizo lingekwisha.

Manake huyo Profesa ni msomi, ni kichwa, mwenye kipaji maalum, na mengineyo mengi.

Sasa iweje tena leo kuna mgao? Profesa msomi atashindwaje kuleta umeme wa uhakika bana?

Haiwezekani kabisa. Hakuna mgao wa umeme Tanzania.
Nyani Ngabu, bandiko lako zuri sana kama mleta mada.
Huu ni ushahidi ulio wazi kuwa kwenye sayari ya dunia kipande kinachoitwa 'Tanzania' tatizo sio elimu bali tatizo ni watu wanaoishi sehemu hiyo. Isije kuwa mazingira ya eneo hili ndiyo yametuathiri au ni uumbaji wa Mungu.
 
hakuna mgao wa umeme tz. naapa hakuna na haijawahi kutokea tz mgao wa umeme prof muongo yuko sawa kabisa na mh. rais pia alikuwa sawa kusema mgao wa umeme utakuwa historia tanzania kuna mgao wa giza na si umeme......
 
yaani acha kabisa inakera sana vile kwao wanao hawajui adha tunayopata......haitoshi juzi kwenye PB wanatangaza wanataka kuongeza gharama unit 1 =198 mpya 1= 336 watapandisha kwa 67% kubinafsisha hawataka huku hawana mipango thabiti ya kuondokana na matatizo......najiuliza wataendelea kutunyonya kwa kutumia hili shirika hadi lini
Wadaiwa wakubwa wa TANESCO ni taasisi za Serikali sasa najiuliza kupandisha bei hizo ni sawa na kujipandishia serikaki yenyewe gharama bila msingi wowote.
 
The best thing he (representing the failing govt and falling political party) can offer to the Wananchi. Mwache aendelee kutukana. Hao hao anaowatukana ndiyo anataka awaongoze na 'kesho' wamwelewe aendelee kuwa kiongozi.

Wakati wengine wanatukana live, wengine wanatukana kirejareja kwa kujifanya wanawajali waalimu na wakulima leo, wakati masuala yote yanapitia kwenye vikao wanavyoviandaa, kuviendesha na kusimamia utekelezaji wake.

Wengine wanatishia kuua raia, wanakiri kuhujumu uchumi kwa shughuli haramu na kutamba serikali haiwezi kufanya lolote dhidi yao. A good sign of

Hasaa mkuu umenena ... yaani hakuna kitu kinanikera kama huu unafiki na uongo wa akina nape na kinana kujifanya kutoa mapovu kwenye majukwaa kuwahadaa watz maskini na wasio na uelewa eti wanawakoromea mawaziri ili hali wakijua kuwa wao ndo wenye serikali na walipaswa wawajibike ... yaani ikijengwa barabara wanawahadaa wananchi kuwa imejenga ccm kumbe ni kodi zetu ila serikali ikiharibu ccm wanajifanya wao hawahusiki .... UNAFIKI UNAFIKI UNAFIKI ... TZ TUZINDUKE
 
Tungelikuwa nchi makini inayosisitiza katika UWAJIBIKAJI, huyu 'bwana umeme' wa sasa, alipaswa kuwa ameshawajibika au kuwajibishwa siku nyingi sana, hasa kwa UONGO! Huyu mtu ni muongo muongo muongo unakuwa muongo kisha unaongezea na 'intellectual arrogance'.

Kama usingekuwa uongo, basi angeshawajibika kwa mambo kama haya. Anyway, acha watu kama hawa wazidi kuonesha na kudhihirisha kuwa sera za CCM zimeshindwa na zinazidi kushindwa. Wacha wazidi kuwaonesha Watanzania kuwa mabadiliko yako nje ya CCM na wakati wenyewe ni huu.

Hakuna tatizo hata moja linalosumbua Watanzania sasa hivi ambalo halina uhusiano na UFISADI wa status quo!

Matatizo nyeti kama haya yanapoingiliwa na wanasiasa huonekana siasa tu.
Sikutegemea chama changu kukaa kimnya na kutolitolea tamko kali swala hili la ukosefu wa umeme wa zaidi ya masaa 30 mfululizo na mgao wa masaa manane tu kwa siku tatu sasa.

Vinyozi, salun wapika vitumbua wauza maji na barafu ndio wanaojua machungu ya kukosekana umeme. Na sio nyie wanasiasa mabwenyenye wenye mishahara mikubwa msiolia sahani moja na masikini wa nchi hii
 
Hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme. Kama huamini rudia tena mawazo haya hadi ujishawishi kuwa unachoshuhudia ni kitu kingine zaidi ya mgao wa umeme. Kwanini hakuna mgao wa umeme? Kwa sababu walisema hakutakuwepo mgao wa umeme tena, mgao wa umeme utakuwa historia. Kwa hiyo kinachotokea ni historia tu ya mgao wa umeme ulivyokuwa; wanatumia nafasi hii kuwakumbusha historia ya mgao wa umeme msije mkasahau.

Na hakuna namna nzuri ya kuwakumbusha watu kuhusu tukio la nyuma kama kwa kutumia 'mfano halisi'. Kwa hiyo, wale waliokuwa wamesahau au ambao hawajui mgao basi hii ni namna nzuri ya kukumbuka. Hiki ndicho alichokisema Waziri Yule kuwa mgao wa umeme utakuwa ni "historia".
Nape Nnauye yuko wapi, si amwambie aachie ngazi kama alivyowaambia wengine wale watatu! Jana wamenilaza giza usiku kucha.
 
Last edited by a moderator:
Historia hii inapatikana only Tanzania, hii ndio historia tunaisoma sasa, tunameza vya watu wamevipa grade, tunatunukiwa mawazo ya watu tunasifiwa ila havina mchango wowote katika jamii za watu weusi, Profesor katulazimisha kusoma historia only in Tanzania..
 
Hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme. Kama huamini rudia tena mawazo haya hadi ujishawishi kuwa unachoshuhudia ni kitu kingine zaidi ya mgao wa umeme. Kwanini hakuna mgao wa umeme? Kwa sababu walisema hakutakuwepo mgao wa umeme tena, mgao wa umeme utakuwa historia. Kwa hiyo kinachotokea ni historia tu ya mgao wa umeme ulivyokuwa; wanatumia nafasi hii kuwakumbusha historia ya mgao wa umeme msije mkasahau.

Na hakuna namna nzuri ya kuwakumbusha watu kuhusu tukio la nyuma kama kwa kutumia 'mfano halisi'. Kwa hiyo, wale waliokuwa wamesahau au ambao hawajui mgao basi hii ni namna nzuri ya kukumbuka. Hiki ndicho alichokisema Waziri Yule kuwa mgao wa umeme utakuwa ni "historia".

Mzee mwanakijiji, mbona huyu jamaa anajitahidi sana kutenda kazi, suala la mgao wa umeme ni bahati mbaya tu imetokea kwenye uzalishaji wa gas, mbona kipindi chake hiki mambo yamekuwa mazuri tu au kwakuwa anaongea ukweli sana?? Huyu jamaa kwa nchi kama hii anafaa sana, tatizo tumezea maneno matamu matamu kwa wanasiasa waongo,mwacheni huyu jamaa afanye kazi yake. Kama uzima upo, mtaona jinsi watu watakavyokuja kumsifia
 
Kinachoendelea sio mgao wa umeme, ni economic sabotage. Songosongo/PAT wanahujumu uchumi.

Kuzima mitambo ya umeme kwa siku 10 kwa kisingizio cha kusafisha visima ni uhuni uliopitiliza na inaonesha ni jinsi gani Songosongo/PAT wanavyodharau Tanzania.

Ingekuwa ni huko kwao, hawa wawekezaji wamezima mitambo kwa dakika 10 (sio siku 10) kuna watu wangepoteza kazi, na wangetozwa faini kwa kila dakika ambayo mitambo itakuwa imezimwa.

Lakini hapa Tanzania, kwa sababu wanaona ni nchi wa wendawazimu wanazima kwa siku 10 na bado wanaendelea kunywa whisky zao bila shida! Biashara za watu zimesimama, nani atawafidia?

Tanesco nao walivyobobea kwenye uzembe, hata ratiba ya mgao hawajatoa.

Hivi Baraza la mawaziri wakikutana huwa wanaongea nini maana mambo kama haya yanayotekea sasa hivi yanatia aibu na yanagharimu uchumi wa nchi. Wabunge nao ndio hivyo tunaambiwa wanazunguka dunia kwa kodi ya watu hawa hawa ambao wamekaa kwenye giza! Dhulma!
 
Hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme, hakuna mgao wa umeme. Kama huamini rudia tena mawazo haya hadi ujishawishi kuwa unachoshuhudia ni kitu kingine zaidi ya mgao wa umeme. Kwanini hakuna mgao wa umeme? Kwa sababu walisema hakutakuwepo mgao wa umeme tena, mgao wa umeme utakuwa historia. Kwa hiyo kinachotokea ni historia tu ya mgao wa umeme ulivyokuwa; wanatumia nafasi hii kuwakumbusha historia ya mgao wa umeme msije mkasahau.

Na hakuna namna nzuri ya kuwakumbusha watu kuhusu tukio la nyuma kama kwa kutumia 'mfano halisi'. Kwa hiyo, wale waliokuwa wamesahau au ambao hawajui mgao basi hii ni namna nzuri ya kukumbuka. Hiki ndicho alichokisema Waziri Yule kuwa mgao wa umeme utakuwa ni "historia".
Karibuni Fursa imejileta
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    22.3 KB · Views: 64

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1385046370.516187.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1385046370.516187.jpg
    30.2 KB · Views: 56
Serikali inayoendeshwa kwa matukio inasababisha umaskini kwa watu wake
 
Ifike mahali tuandamane kama zambia.Tusiendelee kuwa wapole kwa mgongo wa woga wa amani inayohubiriwa na ccm
 
Back
Top Bottom