Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Tax ukikatwa hakuna uwezekano wa kuipata tena in-person. Inawasafirisha kina JK nje, wanatumbua wabunge n.k

Mchango wako wa Pension una uhakika wa kuupata, hata kama ukifa hauliwi.. we huna wanaokutegemea? Kama huna watoto, huna wazazi? kama huna wazazi huna watu ambao ungependa warithi? Kama sivyo we mbinafsi na unapaswa uwaishwe motoni.
Maana ya pension hasa ni security for the days you can't/don't work
Hawawezi kunilazimisha kuchangia miradi fake ya serikali!
Ingekua kuna market study wangejenga jengo la machinga?
Ukitrace source ya hizo pesa ni moja kwa moja pesa yetu!
link: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ga-nssf-imekula-hasara-ya-bilioni-30-a-2.html

Sasa baada ya kufirisika wanatafuta njia ya kutupotezea
na katika kutupotezea kwenyewe lazima wahakikishe kua
the amount of money that goes back to members is
inferior to the amount they actually contributed.

Nimesema hapo kama sio double taxation (part of the money will not come back)
Basi ni waajiriwa wanao changia kukopesha serikali indirectly
in this case lazima waajiriwa wawe treated like shareholders
and the risk should be discussed with them openly and beforehand

hii ndio nini sasa ya kuamua kua watu hapokei hadi 55?
watoe basi a window period ya watu kujipanga (kama 15 years hivi)
 
Mabadiliko ya pension sidhani kama NSSF na pension funds zingine zilaumiwe

wa kulaumiwa ni SSRA ambao kwa kiasi kukubwa ndio waliopendekeza haya mabadiliko mnayoyaona leo hii

wana JF kuweni GREAT THINKERS na angalieni mambo kwa marefu na mapana badala ya kulaumu bila kuchunguza chanzo cha haya mabadiliko.
 
sSRC ndo nini mkuu? Cz ninahasira sana na hawa jamaa. Hope wengi wao watakuwa wameiba na kuwekeza vya kutosha so hawahitaji hizo hela. Tanzania yetu inaongonzwa na wendawazimu na wengi wao wameforge vyeti
 
Lakini kampuni binafsi ziliingia mkataba na mahsirika binafsi na wakachagua aina ya savings hivyo hiyo itakuwa kwa wale wa serikali ambao ukipata kazi ni for life. Mimi leo nikikosa kazi kama nimeajiriwa na mtu binafsi nife umeshikilia pesa zangu si unatafuta vita?
Lastname mie niko kampuni binafsi hii kitu ipo haha tumeambiwa tuanze kujiandaa kisaikolojia walikuja NSSF na PPF pamoja wakaongea hii kitu
Wanadhani na sisi ni kama serikali ajili za till death..
Kwetu sisi ni wewe na mwajiri ..Kampuni ikiondoka ...?
Ukikosana na Boss ...haha No job
Na mengineyo..
 
Last edited by a moderator:
Tax ukikatwa hakuna uwezekano wa kuipata tena in-person. Inawasafirisha kina JK nje, wanatumbua wabunge n.k

Mchango wako wa Pension una uhakika wa kuupata, hata kama ukifa hauliwi.. we huna wanaokutegemea? Kama huna watoto, huna wazazi? kama huna wazazi huna watu ambao ungependa warithi? Kama sivyo we mbinafsi na unapaswa uwaishwe motoni.

Yaani wewe kama si Meneja wa NSSF basi PPF duh am kidding but niko serious
Hivi unadhani mie ninayefanya kazi kampuni binafsi niko kama wewe mfanyakazi wa Serikali..?
 
SSRA kwanza imeanzishwa mwaka gani?..........na hii mifuko imeanza miaka gani? nadhani tukijua hapo tunaweza kupata majibu angalau ya kuridhisha kidogo.
 
Afu trendy ya maisha imebadilika
Zamani pension ilikuwa dili, sasa hivi nawaza nikifika 38 niache kazi nivute NSSF nijiajiri maana itakuwa inatosha.

Pension yenyewe waweza kuwa unachangia 300,000 kwa mwezi kwa sasa halafu baada ya mfano miaka 25 ukawa na miaka 55, unaweza jikuta kila mwezi unapewa 350,000 ambazo wakati huo zitakuwa kama elfu ishirini labda.
 
hivi ni NSSF tu au na wengine watafuata huu upuuzi?
 
SSRA nako utata mtupu hata ajira zao pale ni za kimagumashi ni vyeo vya kupeana aka kuteuliwa so lazima wasikilize watawala wanataka nini.
 
Yaani wewe kama si Meneja wa NSSF basi PPF duh am kidding but niko serious
Hivi unadhani mie ninayefanya kazi kampuni binafsi niko kama wewe mfanyakazi wa Serikali..?

FirstLady..kwanza nikane kwamba mm ni meneja wa both funds ulizozisema, I hold a freemind, thats all! Mimi nilishapata experience ya kuwithdraw hela mara kadhaa baada ya kuacha kazi katika sehemu tofauti kama ninyi mnavyotaka lakini baada ya kukaa na kuuchambua vizuri mfumo wa pension niliona ni kiasi gani tunaoksea kuchukua hizi withdrawals. Kimsingi, sheria ya pension scheme popote duniani hairuhusu withdrawal. Hii inafanyika TZ kwa sababu mifuko ilikuwa ipo katika Provident Fund Scheme na ile transition kutoka huko ikachukua muda mrefu!

Mfumo pekee unaoweza kufanya withdrawal ni Provident Fund kama ilivyokuwa NPF sasa NSSF na kama ilivyo sasa GEPF na LAPF. With provident fund, ni kama unafanya savings bank..tofauti yake na bank ni kwamba huna direct access/control na cash yako. Ila Baada ya muda wako kuisha aidha kwa kuacha kazi au kustaafu unachukua hela yako yote uliyotunza kipindi hicho chote.Mifuko ya namna hii huwa bado ni immature kuweza kumeet uwezo wa kumpa member wake special lumpsum (i.e kianzio cha pesa anapostaafu) na kumpa pensheni mpaka anapofariki baada ya kustaafu.

Lakini pia experience ikaja kuonesha kwamba watu baada ya kuchukua pesa zile walizoweka kwenye provident Fund wanazi-missuse na kisha kubaki hawana kitu. Wengi hujikuta wakiziweka kwenye biashara , starehe, kujenga nyumba etc. Baada ya kufanya investments hizi, mara nyingi biashara zinazowekewa pesa hizi zinakuwa siyo viable, akijenga nyumba hela yote inaisha, bierre, wake etc zote zinaisha..! Swali linakuja.. je? Baada ya kuisha hizi hela huyu mtu pamoja na kuitumikia serikali, nchi yake (don't dispute the fact kwamba wafanyakazi wote wawe wa private au govt wana-lengo moja tu....kusogeza mbele uchumi wa nchi husika, dirrectly or indirect) anaishije maisha yaliyobaki?

Ndio hapo sasa penshen sheme inapo-mata, mwanzoni kabisa unapostaafu i.e at age of 55-60 unapata hiyo special lumsum ambayo ni kiasi kikubwa cha hela ambayo unaweza kuazisha biashara au kuongeza mtaji ili kuendeleza bishara uliyokuwa nayo awali, kujenga nyumba n.k n.k KISHA ukawa unapata mafao ya kila mwisho wa mwezi kwa asilimia kati ya 60-87% ya GROSS SALARY (i.e Basic + any other renumerations i.e transport,nyumba,comm. etc na ndiyo maana wanakata kwenye gross ) ili kukurudisha katika at least same position uliyokuwa nayo kipindi upo kazini na kuondoa social distress.

Lakini pia pension schemes zote zina directive kutoka ILO kuhusiana na addition products kama Invalidity, Employment Injury benefits, maternity, survivors, heathcare etc ili MEMBERS wake wafaidike kabla ya muda ule wa kustaafu. Sasa hii ndiyo pension scheme.. SASA kama huitaki basi inabidi ujitoe ukajiunge na mifuko ya provident i.e GEPF ambayo nayo ikishakuwa matured wanapaswa kufanya kama wanavyofanya wengine..sijui utakimbilia wapi mwishoni.

Alafu, hili jambo la kusema oh nani anataka kuajiriwa milele, tuchukue hela zetu tufanye biashara etc etc. Let me tell you, As far as wewe ni muajiriwa iwe wa serikali au private inabidi utayarishe maisha baada ya kustaafu. Hii mifuko hai-intend kucover wafanyabiashara, ni added product tu ili na wao waingie kwani hata wao wanaweza kupatwa na social distress i.e kuumwa, ajali, kuzeeka na watoto/ndugu/waajiriwa kufuja mali etc etc. YOU HAVE NO WAY OUT, kama sheria ikianza..ukitaka kujitoa kabla ya 55-60 years, basi, unachukua 30% ya kilichomo unaendelea na mambo wako, kingine kinasubiri legal retirement age. Hata huko first world wanalilia pensheni nzuri baada ya kustaafu au kwa ajili ya survivors nyie mnapinga..

Kinachopaswa ni kuwa karibu na Mifuko yetu na kufuatilia ACTUARIAL VALUATIONS ili tuweze kujua solvency ya Fund zetu.The WORLD is moving fast guys..!

Alamsyk.
Donyongijape
 
SSRA kwanza imeanzishwa mwaka gani?..........na hii mifuko imeanza miaka gani? nadhani tukijua hapo tunaweza kupata majibu angalau ya kuridhisha kidogo.

Jisumbue japo kidogo basi eh dada..SSRA imeanzishwa 2008.. go to ssra.go.tz Mifuko pia utapata link humo humo.. Usipende kutafuniwa kila kitu.. nway NSSF 1964 as NPF and reborn in 1997 as NSSF, PSPF 1998, PPF 1978, LAPF 1944, GEPF 1942, NHIF 1999, ZSSF 2005.

So hapo majibu ya kuridhisha yatakujaje baada ya kujua miaka? what is the point?. Nisaidie
 
It is always nice to visit Jamii Forums and once in a while finding posts that use statisitics,references,common sense and most important the technical know how of exactly what one is posting about.Even though I am might be inclined towards the FirstLady views like many others who are not well informed I must admit that your post was REALLY EXCELLENT in the way you have represented your views. Keep them coming
 
Jisumbue japo kidogo basi eh dada..SSRA imeanzishwa 2008.. go to ssra.go.tz Mifuko pia utapata link humo humo.. Usipende kutafuniwa kila kitu.. nway NSSF 1964 as NPF and reborn in 1997 as NSSF, PSPF 1998, PPF 1978, LAPF 1944, GEPF 1942, NHIF 1999, ZSSF 2005.

So hapo majibu ya kuridhisha yatakujaje baada ya kujua miaka? what is the point?. Nisaidie
ahsante kwa kunielewesha ila loh mpaka uniseme kidogo........anyway point ni kwamba hiyo SSRA imeundwa ije iwasaidie hawa wakubwa mana wana madeni makubwa inawadai serikali ukizingatia NSSF ina miradi mingi ambayo imeifanya kwa niaba ya serikali ikiwa wana maana serikali irudishe baadhi ya fedha hizo kwa NSSF ...........sasa baadhi ya miradi imesimama mana hela akuna tena na NSSF................wamepata hasara kwa baadhi ya miradi kama Machinga complex.............so nahisi wanataka kufidia hizo hasara indirect...............
 
Manina.. wallah eti mnasemaje? mmeshaniharibia siku yangu hapa, nina bonge la plan na huu mpunga wangu aiseee..

Plz tell me its not true!~!! hii nadhani itanipeleka barabarani na bango langu iweje hela yangu watu wajipangie tu jinsi ya mimi kuipata? tuukatae huu ushoga

Kwanza mimi hata hili suala la kunikata kila mwisho wa mwezi sikubaliani nalo kabisa.. wanipe hela yangu nijitunzie mwenyewe
 
ahsante kwa kunielewesha ila loh mpaka uniseme kidogo........anyway point ni kwamba hiyo SSRA imeundwa ije iwasaidie hawa wakubwa mana wana madeni makubwa inawadai serikali ukizingatia NSSF ina miradi mingi ambayo imeifanya kwa niaba ya serikali ikiwa wana maana serikali irudishe baadhi ya fedha hizo kwa NSSF ...........sasa baadhi ya miradi imesimama mana hela akuna tena na NSSF................wamepata hasara kwa baadhi ya miradi kama Machinga complex.............so nahisi wanataka kufidia hizo hasara indirect...............

Si kweli kwamba SSRA imeundwa ije kusaidia kudai madeni..WRONG. Imeundwa ku-regulate hz Funds ili kuwepo na equal playing ground. Mengineyo soma SSRA Act ya 2008.

Alafu watu tunachanganya mradi uliojengwa na NSSF,PPF etc na mkopo uliotolewa na NSSF,PPF kwa serikali. Mfano,UDOM,Machinga, TPDF houses, MABIBO hostel ambayo mkopo umesharejeshwa wote, hii miradi imejengwa kwa mkopo wa NSSF..hii mikopo lazima irudishwe!. Kama una ufahamu mzuri, kukopesha serikali is among a low risk business (Go and learn more about this).Na Funds lazima zifanye investments km hizi na nyinginezo ambazo ni miradi inayoiendesha yenyewe directly ili kusaidia jamii , kucreate more jobs (ambapo zitapata members infuture), kutunza Value for Money ili ww uliyetunza leo next 10,20-50yrs upate fedha yenye thamani sawa na kipindi hicho na mwisho ili kupata faida/profit ambayo itatumika kuboresha mafao ya wanachama wake na kuendesha shughuli zake za kila siku.
 
Wafanyakazi tulioko migodini hasa GGM tumepatwa na ugonjwa wa NSSF Syndrome baada ya kuambiwa kwamba kuna utaratibu unakuja ambao mtu hataweze kuchukua mafao yake mpaka afikie umri wa kusitahafu.Jamani wanajamiii wenzangu mtusaidie michango yenu ya mawazo
 
Acha uzushi,
Ulisikia wapi na ktk forum ipi ili tuchangie kikamilifu.
 
Back
Top Bottom