Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

itabidi wafanyakazi tushawishi waajiri watuandikie barua kama tumeacha kazi kwa ajili ya kuchukua pesa zetu tu.

Afu tunaanza upya.

Yaani napata hasira nikiwaza, kwanza PAYE kubwa mno, afu bado na NSSF wachukue?

Msimu huu ntamwaga damu hata kama ni kwa kuua mbu.

Si kweli kwamba SSRA imeundwa ije kusaidia kudai madeni..WRONG. Imeundwa ku-regulate hz Funds ili kuwepo na equal playing ground. Mengineyo soma SSRA Act ya 2008.

Alafu watu tunachanganya mradi uliojengwa na NSSF,PPF etc na mkopo uliotolewa na NSSF,PPF kwa serikali. Mfano,UDOM,Machinga, TPDF houses, MABIBO hostel ambayo mkopo umesharejeshwa wote, hii miradi imejengwa kwa mkopo wa NSSF..hii mikopo lazima irudishwe!. Kama una ufahamu mzuri, kukopesha serikali is among a low risk business (Go and learn more about this).Na Funds lazima zifanye investments km hizi na nyinginezo ambazo ni miradi inayoiendesha yenyewe directly ili kusaidia jamii , kucreate more jobs (ambapo zitapata members infuture), kutunza Value for Money ili ww uliyetunza leo next 10,20-50yrs upate fedha yenye thamani sawa na kipindi hicho na mwisho ili kupata faida/profit ambayo itatumika kuboresha mafao ya wanachama wake na kuendesha shughuli zake za kila siku.

mkuu unanifungua naona uelewa wangu kuhusu Lakini kubali usikubali si kweli kwamba hii inawasidia wafanyakazi wote as one.

mfano: mfanyakazi mgodini;
1. job security almost zero nothing iz done by the government to solve uonevu huu. Leo hii naandika watu karibu 80% wameenda kurisign ili wapate chao bahati baya tumechelewa fungu lilishafungiwa. No one wishes to work in these areas but sometimes in life circle you find in places you did not intend to be.

hebu fikiri mtu kufukuzwa kazi kisa kagonga post parking or any accident (kuna kitu kinaitwa zero torelence) even sleeping at work iz zero torelence which iz equal to no job.

2. mazingira ni hatarishi ukitoa sumu, radiations and rock dusts which may lead to lungs failure ukiachilia kwamba wengi (though there are some who take risk of leaving and secure a knew job) wa waajiriwa ni vijana ambao that is their own area of proffession no other option apart from mining life except you take your NSSF as add up with saved amount unakua mjasiliamali. It is the only place we are not recommended to work more than seven years. A place where a coordinator (tanznian iz paid 2mill) while a southafrican white doing the same job tought by this tanzanian (is paid up to 15000usd with more than 400000tsh every weekend for beers and snacks).
who do you think benefits when it comes for ZERO TORELENCE policy.
3. Umewahi kujiuliza kwa nini kila kukicha matangazo mapya 50 ya kazi 30 ni migodini these people are fired, resigning and wagonjwa (unfit to work) at their young ages na wengine wakienda likizo ndio kimoja while their hopes lies on social security fund. so how can you judge these guys in these bloody working area with civil servants who have guarantee with their work.

I suggest considerations bust be done.

these were my views
 
Hivi kama contributions zitatumika kama collateral kukopea benki nk. sifa ya collateral ni liquidity yani mkopeshaji kuweza kurejesha hela zake mtu akidefault, kwahiyo ina maana hizo hela zinaweza kutolewa huko nssf nk. Kwa maana hiyo sheria hii imetoa direct right ya mwanachama kuvuta mafao yake na badala yake wamepewa mabenk nk. Akili za kusubiri kustaafu ndo utengeneze maisha kizazi cha dotcom hakina hizo, hela zangu nazizalisha na kuzitunza kwenye investment zangu. Hawa wazee wanatuletea sheria gani hizi?
 
Jamani mafao sahihi ya mtu wa mgodini au kazi za muda ni yeye kuchukua pension yake na kununua nyumba ili zimsaidie baadae maana hii ni investment inayoendana na thamani ya pesa na ndiyo maana hata hao NSSF na PPF wao pia wanawekeza kwenye majengo. Hii ya kutunziwa pesa hadi uzeeke miaka zaidi ya 30 mbele ni wizi.

Ok mimi nimeachishwa kazi nina miaka 26 nikiwa na VVU, utanihakikishiaje kufikia hiyo miaka 55? Hawa wabunge waliopitisha hii sheria naona wanashida ya kuitikia ndiyooooooooo tu kwa kila kitu kinacholetwa na serikali ya chama chao. Mungu mmoja hawa watu wanaofanya kazi underground wakifukuzwa kazi alafu eti hao NSSF n.k eti wawanyime pesa yao basi hao wapangaji katika majengo yao marefu wahame maana yatakuwa hatarini.
 
FirstLady..kwanza nikane kwamba mm ni meneja wa both funds ulizozisema, I hold a freemind, thats all! Mimi nilishapata experience ya kuwithdraw hela mara kadhaa baada ya kuacha kazi katika sehemu tofauti kama ninyi mnavyotaka lakini baada ya kukaa na kuuchambua vizuri mfumo wa pension niliona ni kiasi gani tunaoksea kuchukua hizi withdrawals. Kimsingi, sheria ya pension scheme popote duniani hairuhusu withdrawal. Hii inafanyika TZ kwa sababu mifuko ilikuwa ipo katika Provident Fund Scheme na ile transition kutoka huko ikachukua muda mrefu!

Mfumo pekee unaoweza kufanya withdrawal ni Provident Fund kama ilivyokuwa NPF sasa NSSF na kama ilivyo sasa GEPF na LAPF. With provident fund, ni kama unafanya savings bank..tofauti yake na bank ni kwamba huna direct access/control na cash yako. Ila Baada ya muda wako kuisha aidha kwa kuacha kazi au kustaafu unachukua hela yako yote uliyotunza kipindi hicho chote.Mifuko ya namna hii huwa bado ni immature kuweza kumeet uwezo wa kumpa member wake special lumpsum (i.e kianzio cha pesa anapostaafu) na kumpa pensheni mpaka anapofariki baada ya kustaafu.

Lakini pia experience ikaja kuonesha kwamba watu baada ya kuchukua pesa zile walizoweka kwenye provident Fund wanazi-missuse na kisha kubaki hawana kitu. Wengi hujikuta wakiziweka kwenye biashara , starehe, kujenga nyumba etc. Baada ya kufanya investments hizi, mara nyingi biashara zinazowekewa pesa hizi zinakuwa siyo viable, akijenga nyumba hela yote inaisha, bierre, wake etc zote zinaisha..! Swali linakuja.. je? Baada ya kuisha hizi hela huyu mtu pamoja na kuitumikia serikali, nchi yake (don't dispute the fact kwamba wafanyakazi wote wawe wa private au govt wana-lengo moja tu....kusogeza mbele uchumi wa nchi husika, dirrectly or indirect) anaishije maisha yaliyobaki?

Ndio hapo sasa penshen sheme inapo-mata, mwanzoni kabisa unapostaafu i.e at age of 55-60 unapata hiyo special lumsum ambayo ni kiasi kikubwa cha hela ambayo unaweza kuazisha biashara au kuongeza mtaji ili kuendeleza bishara uliyokuwa nayo awali, kujenga nyumba n.k n.k KISHA ukawa unapata mafao ya kila mwisho wa mwezi kwa asilimia kati ya 60-87% ya GROSS SALARY (i.e Basic + any other renumerations i.e transport,nyumba,comm. etc na ndiyo maana wanakata kwenye gross ) ili kukurudisha katika at least same position uliyokuwa nayo kipindi upo kazini na kuondoa social distress.

Lakini pia pension schemes zote zina directive kutoka ILO kuhusiana na addition products kama Invalidity, Employment Injury benefits, maternity, survivors, heathcare etc ili MEMBERS wake wafaidike kabla ya muda ule wa kustaafu. Sasa hii ndiyo pension scheme.. SASA kama huitaki basi inabidi ujitoe ukajiunge na mifuko ya provident i.e GEPF ambayo nayo ikishakuwa matured wanapaswa kufanya kama wanavyofanya wengine..sijui utakimbilia wapi mwishoni.

Alafu, hili jambo la kusema oh nani anataka kuajiriwa milele, tuchukue hela zetu tufanye biashara etc etc. Let me tell you, As far as wewe ni muajiriwa iwe wa serikali au private inabidi utayarishe maisha baada ya kustaafu. Hii mifuko hai-intend kucover wafanyabiashara, ni added product tu ili na wao waingie kwani hata wao wanaweza kupatwa na social distress i.e kuumwa, ajali, kuzeeka na watoto/ndugu/waajiriwa kufuja mali etc etc. YOU HAVE NO WAY OUT, kama sheria ikianza..ukitaka kujitoa kabla ya 55-60 years, basi, unachukua 30% ya kilichomo unaendelea na mambo wako, kingine kinasubiri legal retirement age. Hata huko first world wanalilia pensheni nzuri baada ya kustaafu au kwa ajili ya survivors nyie mnapinga..

Kinachopaswa ni kuwa karibu na Mifuko yetu na kufuatilia ACTUARIAL VALUATIONS ili tuweze kujua solvency ya Fund zetu.The WORLD is moving fast guys..!

Alamsyk.
Donyongijape

Mkuu umenitoa gizan nilikuwa sielewi kabisa hii mifuko ya jamii.Shukran
 
Ni wakati wa TUCTA kukunjua makucha yake. Maamuzi ya kijinga sana. Hivi watatupa na guarantee ya kuishi tufikie hiyo miaka ya kustaafu. Afya za watanzania wenyewe siku hizi ziko kimtego mtego tu


Wangeweka kuwa mtu akifanya kazi 10 yrs, aruhusiwe kustaafu nA kuchukua mafao......

Hata hivyo, coz nna 6 yrs now, nitachukua mkopo wa nyumba!! Then, ikitokea ishu nakimbia kibarua!!!!
 
Tena nasikia ukistaafu hulipwi pesa zote kinachofanyika utalipwa mshahara wako uliostaafia hadi ufe. Hii inamaana utajilipa mwenyewe na chenji utawaachia kwani kama umekatwa miaka 42 hiyo fedha si ndo unjilipa mwenyewe tu!
 
Kuna walaka toka serikalin umesambazwa kuanzia tar 20 july, kwenye mifuko ya jamii, ikiwataka kusitisha kutoa michango (malipo) ya kujitoa uanachama.

Na kuanzia sasa malipo yote yatatolewe mpaka mwanachama amefikisha miaka 55 au 60, walaka huo unasema umepitishwa na bunge na umetiwa sahin na rais mwezi wa 4.

Swali
1. Mimi kama mwanachama mbona sijasilikishwa?
2. Mbona vyama vya wafanyakaz wamesema hawajui
3. Limejadiliwa bunge gani? Mi mbona la mwezi wa nne sijasikia hili mkisemea pale bungeni au lilipita kwa mlango wa nyuma ya bunge au ndio hile wanaohafiki waseme NDIO?

Mimi nina miaka 29, nikiache kazi kesho siwezi kuchukua mafao yangu NSSF mpaka nisubiri miaka 31 ijayo, hii ni haki? Wengine tulikuwa na plan, michango yetu ikifika mil. Kadhaa tunaache kazi tunadraw tuanzishe miradi yetu wenyewe. Life span ya mtanzania average ni 44, sasa wanapotuambia kusubiri mpaka utimize 60yrs mliliangalia hilo?

Nyie wabunge wetu kazi yenu nini? Hili hamkuliona? Au kwa vile haliwausu.

Tatizo langu ni kuwa Hela zetu wanafaidi wengine, ingekuwa na sisi wanachama tunamanufaa nayo wala nisingepiga kelele. Hata mkopo hawatupi, zaidi wanafaid wakina manji etc. Shame on you...!

CPA(T)
 
watoe majibu ya kuridhisha,kama wamepitisha ni kwa manufaa ya nani? Hapa hatuna mchezo au na wao ni Dhaifu? Tunawasubiri....
 
Ni hoja nzuri...sema mtiririko wako wa maneno na spelling zinanitia shaka kama ww ni proffessional accountant.
 
Ni hoja nzuri...sema mtiririko wako wa maneno na spelling zinanitia shaka kama ww ni proffessional accountant.

cha msingi umelewa, sikuja kuonyesha ujuzi wa kuandika, mimi nimewauliza wabunge wetu
 
Mi sijalewa labda ww badala ya kwenda church umeamkia konyagi

kama haujaelewa umejuaje kama ni hoja nzur? Ok ila sio lazima wewe uelewe wapo walioelewa. Nimeshindwa kwenda kanisan nawazia michango yangu ya NSSF. Karibu tupate supu ya mbuzi hapa USESI BAR
CPA(T)
 
Urgent public call for @J.Mnyika, Zitto HKigwangalla, @Tundi Lisu (Sijui kama yupo humu)

Tunaomba ufafanuzi hii sheria ya kuzuia withdraw benefit imepitishwa lini imekuwaje na nyie
mkakubali hii sheria ipitishe?

Wabunge wetu wakishidwa kutoa ufafanuzi wa kusadia wananchi wake napendekeza MASS STRIKE

hii mbona ni kinyume na ILO conversion minimum benefit standard N0.102???


[h=4]ILO Social Security (Minimum Standards) Convention, 1952 (No. 102
Article 19[/h]Each Member for which this Part of this Convention is in force shall secure to the persons protected the provision of
unemployment benefit in accordance with the following Articles of this Part

Article 20
The contingency covered shall include suspension of earnings, as defined by national laws or regulations, due to inability to obtain suitable employment in the case of a person protected who is capable of, and available for, work


[h=4]Article 21[/h]The persons protected shall comprise--
(a) prescribed classes of employees, constituting not less than 50 per cent. of all employees; or
(b) all residents whose means during the contingency do not exceed limits prescribed in such a manner as to comply with the requirements of Article 67; or
(c) where a declaration made in virtue of Article 3 is in force, prescribed classes of employees, constituting not less than 50 per cent. of all employees in industrial workplaces employing 20 persons or more.



[h=4]Article 24[/h]1. The benefit specified in Article 22 shall be granted throughout the contingency, except that its duration may be limited--
(a) where classes of employees are protected, to 13 weeks within a period of 12 months, or
(b) where all residents whose means during the contingency do not exceed prescribed limits are protected, to 26 weeks within a period of 12 months.
2. Where national laws or regulations provide that the duration of the benefit shall vary with the length of the contribution period and/or the benefit previously received within a prescribed period, the provisions of subparagraph (a) of paragraph 1 shall be deemed to be fulfilled if the average duration of benefit is at least 13 weeks within a period of 12 months.
3. The benefit need not be paid for a waiting period of the first seven days in each case of suspension of earnings, counting days of unemployment before and after temporary employment lasting not more than a prescribed period as part of the same case of suspension of earnings.
4. In the case of seasonal workers the duration of the benefit and the waiting period may be adapted to their conditions of employment.











Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii

UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU
 
Kila siku mmnaambiwa jiajirini wenyewe hamsikii..haya sasa oneni yanayowakuta. Mwenzenu nimejiajiri na nachangia kwenye voluntary scheme. Naweza kujitoa saa yoyote cuz sheria hainibani.
 
Kila siku mmnaambiwa jiajirini wenyewe hamsikii..haya sasa oneni yanayowakuta. Mwenzenu nimejiajiri na nachangia kwenye voluntary scheme. Naweza kujitoa saa yoyote cuz sheria hainibani.

Wind passing deserves privacy mkuu.......why you doing it in public???????
 
Kaka hii sheria ilipitishwa bunge la mwezi April. Wakat ule ishu kubwa kwa public attention ilikuwa muswada wa sheria ya Katiba watu wakapenyeza na kama kawaida bunge likaitikia ndiyoooooooooooooo. Halafu ikamaliziwa na kiti kikisema "haya, nadhan waliosema ndiyo wameshinda, hivyo muswada huu umepitishwa na bunge kuwa sheria! Kiongozo wenu Mkuu alisaini fastafasta in two weeks time.
HUNA HAJA YA KUWALILIA AKINA LISU MNYIKA HKG maana tulipata fursa kubwa pale Oktoba 30 mwaka 2010 lakini inawezekana na wewe ulikuwa upande wa Kaka kwa ari zaidi na nguvu zaidi. Hatahivyo Bunge letu wengi wape. Na wengi ni wale wanaopigia mistari miswada na kauli zote za serikali. Hadi hapo tumeliwa
 
Back
Top Bottom