Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Acha uzushi,
Ulisikia wapi na ktk forum ipi ili tuchangie kikamilifu.

duh kiongozi huna hiyo habari? mbon wale dhaifu pale mjengoni washaijadili na kuipitisha. no premature withdraw mpaka age ya kustafu. n NSSF kwa mbwembwe wameanza kukopesha saccos
 
wana Jamii hili mbona hatulizungumziii ipasavyo inamana tumelidhika na hii taarifa au ni uzushi? kama ni kweli hatukubali kwani mie sina grent ya kufika uzeeni na hiyo ni pesa yangu niliyoitokea jasho.
 
Huo sio uzushi ni kweli sheria inabadilishwa ili tushindwe kuchukua fedha zetu. Kama life expectancy ya mtanzania ni around miaka 45, basi walitakiwa wabase kwenye hiyo na sio miaka 60! Anyway tunajua fedha zetu wame-invest kwenye siasa (miradi ambayo return yake ni almost imposible eg machinga complex, etc)
 
Jamani jana tulikuwa na hawa ndugu wa NSSF, kwa jinsi majibu yao yalivyokuwa hilo lipo laja japo hawajui lini itatokea hili.
 
Jamani mimi habari nazopata zinanitatiza kwa kweli, watu wa NSSF Geita na PPF Mwanza wametoa taarifa kwa umma kwamba hizo habari ni za uzushi, ila taarifa zingine zinasema hizo ni habari za kweli. Tena kwa habari nilizopata ni kwamba NSSF Geita na NSSF Mkoa mwingine jina ninalo nitalitoa mpaka nikipata hiyo taarifa yao waliotoa kwa umma vinapishana. Wakati NSSF Geita wanasema taarifa sio za kweli wakati huo huo NSSF ofisi ninayo wanasema hizo nitaarifa za kweli

Ukweli wanatuchanganya, ila nachoamini ni kwamba hiyo sheria itakua kweli imepitishwa, nasema ivyo kwa sababu zifuatazo:-
1. Kwa uelewa wangu ni kwamba - madhumuni ya mifuko ya kijamii duniani kote ni kwamba kusaidia mtu anapofika umri wakutokufanya kazi kwa maana atakua hana kipato wakati bado anahitaji mahitaji. Kwa hiyo pesa hizo ndio zitamsaidia
2. Pili ni kwamba moja kati ya vyanzo vya pesa katika serikali nyingi duniani ni hiyo mifuko ya kijamii

Angalizo: kwa Tanzania nazani kama wamepitisha sheria hiyo kwa kufwata nchi zilizoendelea wanakosea sana, manake mifumo ni mibovu kabisa. Najua pesa hizo zitakua zinaishia kuliwa na watu wachache kwenye hayo mashirika. Nasema hivyo kwa sababu, umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 45, ila sheria inaruhusu mtu kufanya kazi mpaka miaka 55 hadi 60 hapo ndipo watu wachache watakula pesa zenu ndugu zangu mlioajiriwa

Ila kisheria nawasiwasi sijui kama hii inawezekana kwa wale watu ambao tayari walishakua wanachama kwenye mashirika hayo. Nachokijua mimi ni kwamba kama sheria imepitishwa itakua inasema inaanza lini? Hivyo basi kama itasema inaanza lini mtazamo wangu ni kuwa kwa wale waliokua wameshajiunga na mashirika hayo (NSSF, PPF etc) hawatabanwa na sheria hiyo hata akiacha kazi 2016 sababu sheria haipaswi kufanya kazi "retrospective" Hiyo sheria inatakiwa kuwabana watu wote ambao watakua wamejiunga na mashirika hayo baada ya Tangazo la Serikali kusema hiyo sheria inaanza lini?

Hayo ndio mawazo yangu katika mtazamo wa kisheria

Wenu
Jamuhuri Hussein Rungu
"The problem with the word is that the intelligent people are full of doubts while the stupid ones are full of conifence" – Charles Bukowski
 
Wafanyakazi wa mgodi wa North Mara (Barick) Jana walipokwenda NSSF kuchukua mafao yao baada ya kuwa wameachishwa kazi, waliambiwa wasubiri hadi miaka 60 kwani sheria hiyo imeanza kutekelezwa tangu 01 July 2012.
Swali: Inakuwaje sheria ipitishwe kinyamela pasipo husisha wahusika?
Life span ya Mtanzania ni miaka 45 je hiyo 60 atafikisha lini?
Je, kwa kipindi hicho ambacho hatakuwa na kazi nani atachangia mfuko wake?

IKUMBUKWE KWAMBA maisha ya mfanyakazi migodini ni mafupi sana kutokana na kuathirika kwa kemikali zitumikazo migodini. nA AACHAPO Kazi huenda asipate kazi tena. Ikiwa kijana wa miaka 30 kaacha kazi lini atafikisha miaka 60 wakati tayari keshaathirika?
:flypig:
Naomba Mchango wenu wadau. nawasilisha.
 
Wana JF,

Kuna threads ziko humu kuhusiana na suala la mafao kwa wafanyakazi na nimeona niweke ufafanuzi huu lengo likiwa si kuongeza idadi ya threads bali kuwafanya watu wapate habari hii wa usahihi zaidi. Nimekopi na kubandika hapa kwa hiyo nimeshindwa kukopi header ya barua hii kutoka SSRA lakini ni barua ya jana tarehe 20/07/2012 kwenda kwa menejimenti ya Barrick ambayo ilitumwa kwa wafanyakazi wote wa mgodi wa Bulyanhulu.

Kumb. Na. AE/164/334/Vol.II/2 20 JULAI, 2012


UFAFANUZI KUHUS FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.

Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.

1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.

2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.

3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.

4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia. Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.

5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika

6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria. Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.

7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu

8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.

9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo. Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.

Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii

Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU

My Take: Ni nani atawatetea wafanyakazi wa Tanzania hii? Hili kweli ni pigo kubwa!
 
HELA NI ZETU ama ZAO?

Kwa nini wafanye maamuzi kimya kimya bila kushirikisha wafanyakazi?

TUCTA wako wapi? TUCTA ni lege lege dhaifu

Hata mikopo hatupati halafu wanachezea wafanyakazi ee

Now is time for workers to stand up united and show solidarity.

Hela zetu wameingia mikataba feki ya kifisadi, sasa wanacheza na hela za wavuja jasho eeee.

Mishahara yenyewe kiduchu halafu wafanyakazi.

Now is time for Great Strike!!!
 
tumekwisha maana wengine wanafanya kazi ya mikataba mifupi ya mwaka na uhakika wa kurenew ni mdogo sana, huu ni ujambazi wa mchana.
 
HELA NI ZETU ama ZAO?

Kwa nini wafanye maamuzi kimya kimya bila kushirikisha wafanyakazi?

TUCTA wako wapi? TUCTA ni lege lege dhaifu

Hata mikopo hatupati halafu wanachezea wafanyakazi ee

Now is time for workers to stand up united and show solidarity.

Hela zetu wameingia mikataba feki ya kifisadi, sasa wanacheza na hela za wavuja jasho eeee.

Mishahara yenyewe kiduchu halafu wafanyakazi.

Now is time for Great Strike!!!

Ni wakati wa TUCTA kukunjua makucha yake. Maamuzi ya kijinga sana. Hivi watatupa na guarantee ya kuishi tufikie hiyo miaka ya kustaafu. Afya za watanzania wenyewe siku hizi ziko kimtego mtego tu
 
wabunge kazi yao ni kuunga mkono hoja tu!hiyo mikopo inapatikana vipi kama sio wizi wa wazi wazu
 
Jamani hii ni hatari. Mawazo ya kizamani eti ustaafu ndo ujenge nyumba hayapo siku hizi. Mtupe hela zetu tujipange. Ukimwi, lishe duni, maisha magumu yenye stress ni wangapi watafika sixties. Aise turudi nyuma hii kitu ifutwe. Siwezi ishi maskini halafu uzeeni ndo nipate hela.
 
Ni wakati wa TUCTA kukunjua makucha yake. Maamuzi ya kijinga sana. Hivi watatupa na guarantee ya kuishi tufikie hiyo miaka ya kustaafu. Afya za watanzania wenyewe siku hizi ziko kimtego mtego tu

Mkuu, kwa taarifa yako ni kwamba TUCTA walishirikishwa katika mabadiliko hayo.
 
babu slaa tangaza ukiingia madarakani utazuia uozo huu tukuunge mkono
 
Modes nawashauri katika uzi huu muondoe neno tetesi na muifanye post ya wikolo kama update kwenye uzi huu. Pia uzi huu uwe sticky. Nadhani kina Cookie, Paw na wengine mmenielewa. Hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wale wanaodhani wakiacha kazi watakaa miezi 6 kisha wakachukue chao, kumbe sio.
 
Last edited by a moderator:
Jamani mimi ni form four na nina miaka 27. nilipata ajira ya muda katika kampuni moja ya wakimbizi. Hivi tunavyoongea ni tarehe 10 tu mwezi huu (wa sita) kampuni imepunguza wafanyakazi na mimi nikiwa miongozi mwao. Sina uhakika kama nitarudishwa kazini. Akiba yangu ya NSSF ni kiasi cha 3,500,200/=. Nilikuwa na mpango wa kuifuatilia hii pesa ili nilipe ada katika chuo ambacho nimepata usajiri ili niendelee na masomo ya utaalam na kuachana na hili suala la kufanya kazi bila utaalam. Niasikitika sana kusikia kuwa mpaka nifikishe miaka 55 au 60 ndipo nipate hii pesa ambayo sijui itakuwa na thamani gani tena?

Hayo ni maneo niliyoambiwa na kijana mmoja aliyeko Tabora baada ya kisikia kilio cha NSSF.

Ukweli ni kwamba hii sheria pamoja na kuwa ni muundo wa sheria za ILO lakini ilitakiwa iendane na mazingira ya kazi na nchi. Mfano wa huyu kijana unatosha kutupatia picha ya madhara makubwa yatakayowapata wafanyakazi wa kazi za muda mfupi. Lakini nikifikiria sana nagundua kuwa malengo ya hii mifuko yamebadilika, badala ya kuwafaa watu uzeeni imekuwa ya kutapeli pesa za wafanyakazi. Mtu ambaye anadai 5Mil leo hii akiwa na miaka 25 unapomwambia asubiri miaka 30 kwa ufupi ni kwamba unamfanya asamehe hiyo pesa! tuseme 5mil miaka 30 ijayo iwe na thamani sawa na 100,000/= ya leo hii. Je kuna mtu kichaa wa kufuatilia 100,000/= Dar es salaam ili imufae? Badala yake nadhani kitakachotokea ni NSSF kuitumia hiyo pesa wakiamini kuwa miaka 30 ijayo huyu mtu either atakuwa amekufa au hawezi kuifuatilia kwani ni ndogo kuliko garama za kuifuatilia! Na kama kweli wana lengo la kuwasaidia wafanyakazi walioko katika sekta binafisi basi watumie formula inayotumika kwa watumishi wa Serikali ili na hawa walipwe kwa pension kama ile ya Serikali. Lakini pia ingekuwa na maana kama wabunge pia wangesubiri Pension zao hadi wafikie huo umri.
 
Back
Top Bottom