Hakuna malipo ya NSSF, PPF hadi umri wa kustaafu ufike!

Kwa mambo yanayofanywa na hii serikali ni kielelezo tosha kabisa kuwa kuwepo kwao madarakani kutaendelea kudidimiza nchi, maamuzi kama haya hayana tija yoyote kwa mfanyakazi na kwa mwananchi yeyote kwa ujumla; wanaendelea kutuaminisha kuwa wamefikia tamati ya ubunifu, mabadiliko ni lazima ili kunusuru nchi!
 
Wafanye wanavyofanya ila wakipitisha hiyo sheria wapitishe na ya kulipa unemployment benefits kama huko mbele vile, ili nikipoteza akzi niendelee kuishi hadi kapenshen katapoiva au nikipata ajira ingine naendeleza kujazia pension yangu.
 
Wafanye wanavyofanya ila wakipitisha hiyo sheria wapitishe na ya kulipa unemployment benefits kama huko mbele vile, ili nikipoteza akzi niendelee kuishi hadi kapenshen katapoiva au nikipata ajira ingine naendeleza kujazia pension yangu.

Naam Mnama! Mfumo wa kusubiri mafao hadi uzeeni unatakiwa uje pamoja na mfumo wa Unemployment Benefits kwa kipindi mtu unapokuwa huna ajira. Wajanja sifanye kukopi viti nusunusu kwa manufaa ya 'wajanja' wachache.

It's 51 years down the independence lane.
 
Mwenye ufahamu wa hili jambo atujuze kwa mapana iwapo ni muswaada au ni sheria inasubiri kusainiwa na rais au ni sheria imeshapitishwa. Lakini kwa vyovyote vile (kama ni kweli) hili ni sawa na msumari wa mwisho kwenye jeneza la mfanyakazi wa tanzania kwani kwa bunge lililopo sina uhakika kama kuna wakupinga hii kitu jamani. Kuna maswali mengi nchi hii hayana majibu:- je nssf wanapoamua kuwekeza kwa fedha za wafanyakazi kwenye vitega uchumi nani huwa anawapa ruhusa kuwekeza au huwa wanamuuliza nani? Faida inayopatikana kutokana na kutumia fedha hizo kama mtaji je kila mwanachama anapata gawio la asilimia ngapi? Je kwa kukaa na fedha za mwanachama (bila mwanachama kuzichukua) wanampatia mwanachama faida (riba ) ya asilimia ngapi kwa mwaka?
Tukiacha hayo ya nssf serikali nayo inatafuta vyanzo cha mapato, hivi kuna sababu gani ya msingi inayowazuia kutoza kodi mapato ya wabunge kama sehemu ya kupanua wigo wa kukusanya kodi? Na migodi ya madini? Wachumi class "a" wapo wapi jamani?
Mwisho ushauri wangu ni kuwa mafao ya wabunge (tshs. 40,000,000 sina uhakika na figure) yazuiwe kwa wabunge ambao hawajafikisha miaka 60 mpaka hapo watakapotimiza umri huo ili na wao waone machungu anayopata mfanyakazi wa tanzania.
 
Bargain,

Hii sio tetesi maana haijawa kama hivyo. Lakini umefanya vizuri kuleta hii habari katika kipindi hiki na kuwafanya waajiriwa wote Tanzania wakae mkao wa kula.

Ukweli ni kwamba serikali ina mpango wa kupeleka bungeni marekebisho ya muswada wa sheria wa mafao ya wafanyakazi kama ulivyopitisha ba bunge ili sasa kufanya wafanyakazi wote wanaokatwa akiba ya mafao (PPF,NNSF, PSPF,LAPF,GEPF n.k) kulazimika kutopata mafao yao kama hawajatimiza umri wa kustaafu(55-60).Mpango huu unaletwa kwa sababu serikali yenu haina namna ya kufanya na ingependa kupata boost ya mapato toka mifuko hii ili kuleta pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Mpango huu wa aibu na kandamizi utawaathiri wafanyakazi zaidi ya 700000 serikalini lakini kwa kipekee utaathiri na kuua ndoto za wafanyakazi zaidi ya 3000000 walio katika sekta binafsi kama vile makampuni, NGOs na wale waliojiajiri wenyewe na ambao wanatumia mifuko hii.

(Una imani kubwa kwamba wabunge wetu hasa wa upinzani wataupigia ngumu mpango huu nyonyaji ambao ni wa aina yake katika nchi zote za Afrika. Hii pia inatoa fursa kwa wafanyakazi wote nchini (hasa vijana) kutafakari na kuona jinsi serikali yenu inavyopanga kufifisha mipango yenu ya muda mfupi na ile ya kati. Kazi kwenu simameni na Chukueni Hatua Sasa.

HABARI NDO HIYO

another part of silly? kweli tuna watumishi wanaofikiri kwa kutumia ubongo wa nyuma!wanawaogopa wawekezaji na magepu wanayafil kwa kodi za wananchi!
 
Wanchi tunatakiwa tuwe makini na hao wabunge , tuwanote kwa majina, atakaye sema ndiyo lazima 2015 asirudi na chadema mkitupa nchi lazima sheria hiyo tuifute ndani ya siku 30 za utawala wetu
 
Hahahaaa, kweli huu ni musmari wa moto, naona wameamua kutuchoma kote kote. I wonder inakuaje kama mtu anahama kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine. Nahisi kutakuwa na Upotevu mkubwa wa Fedha kwa hali hii. Wanataka kutukatisha tamaa hatimaye tuwaachie waji-enjoy wenyewe.
 
Ujambazi mwingine kwa mali ya raia wasionahatia; Kwanini serikali ipange matumizi ya mapato yangu??? kwa hiyo nikipata shida utawajibika kwa mipango hiyo??? Iache wizi wa kijanja na kijinga kwa pamoja. Wabunge wetu hili hatutaki vinginevyo kweli tutakuwa hatuaminiana tena kutokea hapo.
 
Hapo kwenye nyekundu, hii ni KASHFA ya wazi. WHY BARRICK??????

Mtoa huja yupo sahihi nusu, ukweli ni kuwa wafanyakazi wote wa migodini, bila kujali unafanaya Barrick au kampuni gani ili mradi tu uwe kwenye minind sector ndani ya wiki 1 tu pesa yako hiyo inatoka, hii ina miaka kama 5 hivi sasa.

Anyway, turudi kwenye maada, hivi hatuwezi mtafuta mwanasheria mzuri akatutete mahakani ili muswada huu usijadiriwe Bungeni? to me nafikiri hapa ndio pakuanzia vinginevyo tuanze kuandamana!
 
Mawazo ya kusubiri kustaafu ni ya kizamani na yanatoka watu wasio na mawazo ya kijasiliamali, wakati wa kumtumikia muajiri kwa miaka 30 au 40 umepita. Kwa sasa mtu unafanya kazi miaka mitano unavuta NSSF yako kuongezea capital unaendeleza ujasiriamali na kutoa ajira kwa watanzania wenzio. Kufanya kazi miaka 40 waachiwe walimu na madaktari ambao hamtaki kuwapa mishahara mizuri.
 
Hii serikali sasa imeshatuona sisi hamnazo ni wa kuburuzwa tu, hiyo sio fair kabisa life expectancy ya mtanzania mwenyewe inazidi kushuka siku hadi siku, au waseme tu kwamba serikari inataka ianzishe chanzo kingine cha mapato kwa wafanyakazi.
 
Bora sisi tuendelee kubeba mabox tu!! Kama mambo yenyewe ndo haya!!

This has fired up my efforts!!! Endeleeni kupiga siasa tu huko... Kwa hiyo wanataka kutumia hela za watu kwenye miradi inayokufaga tu!! Duh kina MKJJ walisemaga haya tukawashambulia! Naanza kupata picha...
 
GreatThinkers,
Nimepata taarifa za uhakika toka Migodini ya kuwa NSSF na PPF wamefanya semina elekezi na kuwataarifu rasmi kuwa Ukiacha au ukiachishwa kazi hakuna kuchukua chako hadi ufike umri wa kustaafu. Sheria hiyo itaanza kutumika wakati wowote mwaka huu.
Hali hiyo imechanganya watu kiasi kwamba hadi muda huu tunaozungumza idadi ya watu isiyopungua 18-North Mara wameacha tangia Jumatatu Juzi,24 katika Mgodi wa Geita tokea Juzi, 13-Buzwagi, na bado wanaendelea. Hali hiyo pia imeendelea kuathiri migodi mingine kama Tulawaka na Kakola.

  • Tafsiri iliyopo kwa hao Jamaa kwa mujibu wa Source ni kuwa hawaamini kama watafikia huo Umri na vile vile wanahofu kuwa serikali imetumia hizo pesa ndiyo maana inataka kupitisha sheria hiyo.
  • Wanaogopa kukosa mafao yao kama walivyonyimwa wastaafu wa Afrika Mashariki.
Habari ndo hiyo.

Source za ziada.
Wasiliana na wadau walioko migodini
Uliza ofisi yoyote ya NSSF/PPF:israel:
 
Du. Kweli mfanyakazi wanaonewa sana. Mbona wabunge hawasubiri miaka 60 wakimaliza tu miaka mitano wanavuta chao.

Imefika wakati sasa wafanyakazi kuchukua hatua juu ya dhuluma inayofanywa kwao.
 
Niweke waz kaka! Watu wameacha nin? Ulitaja idad ya walioacha! Hv ni lazma kujiunga na hyo mifuko? Na naweza kujitoa kama nimeshajiunga? Mnisaidie jaman
 
Mi mwenyewe namtafuta afisa utumishi aniweke wazi katika hili, siamni kama tunaelekea kuzikwa tukiwa hai
 
Huwa nasemavkila siku tatizo la watanzania nikushindwa kufanya maamuzi magumu siku zote hawa wanachekewa tu dawa ni kuharibu hali ya hewa mazima nchi inuke tu kuanzia magogoni mpaka migodini kinyume na hapo sekta zote mtakuwa mnalia tu miaka nenda miaka rudi.
 
Kama mdau wa migodini naomba wabunge wawatetee hawa wtz wanaotaka kunyonywa na hii serikali kwa kisingizio cha kusaidia uzeeni,maisha ya migodini ni hatarishi sana kiasi hakuna uwezekano wa mtu kufika 60?
 
Kuna umuhimu mkubwa kuangalia kwa umakini mkubwa miswaada kama hii.
Mimi mwenyewe sitaki ingawa niko mjini Je hao walio chini ya ardhi migodini wakihangaika???
 
Mimi mwenyewe ni mfanyakazi wa geita gold mine na jana HR alikuja kutoa feedback ya kilicho ongelewa na NSSF na PPF,ukweli hali ya hewa sio sawa jana pekee watu 8 wali resign na bado hali ni tete.
Ni bora tufanye maamuzi magumu kuliko kuacha fedha zetu ziliwe na serikali hii dhalimu.
 
Back
Top Bottom