Wastani wa umri wa kuishi mtanzania ni miaka 50, unataka kulazimisha haki ya mtu hadi miaka 60 hiyo si ni sawa na kumyima hiyo haki yake. Marekebisho ya hiyo yangeangalia zaidi hali halisi ya mtanzania. Tumeshindwa kuendelea na billions of money kutoka kwa wafadhili je leo maendeleo yatakuja kwa kumnyima mtanzania haki yake.
Matarajio yetu sasa ili tanzania iweze kwenda mbele ni kuwajengea uwezo mtu mmoja mmoja ili kuwa na strong middle income people, sasa kwa kuwanyima haki yao ya msingi kwa kisingizio cha kupata fedha za maendeleo hii ni sawa na kuchimba kaburi la maendeleo ya Tanzania katika siku za usoni.
Tahadhari ni kuwa tunaweza kufanya mzaha na likawa kweli, hasa kwa kuwa wtz hatuna umoja katika masuala ya msingi kama hili. Tuendelee kuelimishana. Hata kama Bunge litapitisha basi wafanyakazi wote tuandamane.