Kama itapita hakika itakuwa kilio kwa wafanyakazi wengi;
Kwa maisha ya sasa yalivyo na ugumu wa kila hali; magonjwa ya kila aina , BP, kisukari, HIV/AIDS , TB , malaria etc. Bado wanategemea watu tufike 55- 60yrs old. ..............Eeh Mungu tusaidie waja wako.
Hi wana JF,
Nimesikia kuwa kuna sheria imepitishwa kuwa HAKUNA TENA kuchukua hela za NSSF ukiacha kazi HADI UMRI wa kustaafu
ufike.
Mwenye kujua UKWELI atuhabarishe zaidi (NSSF au watunga sheria wetu).
Wafanyakazi wa sekta binafsi mnalijua hili?
hujaelewa tuu kwa sasa hakuna sheria ila ndio muswaada unaenda bungeni!Si kweli. Mimi nina miaka 30, nimechukua hela yangu Nssf Ijumaa Juni 22, 2012, na hadi leo Jumapili hakuna sheria yoyote iliyotungwa na bunge. Kinachosubiri umri huo ni pensheni, yaani malipo ya kila mwezi kwa waliochangia miaka 15 mfululizo na kufikia umri wa kustaafu i.e. Miaka 55 ya hiyari au 60 ya lazima
Bargain,
Hii sio tetesi maana haijawa kama hivyo. Lakini umefanya vizuri kuleta hii habari katika kipindi hiki na kuwafanya waajiriwa wote Tanzania wakae mkao wa kula.
Ukweli ni kwamba serikali ina mpango wa kupeleka bungeni marekebisho ya muswada wa sheria wa mafao ya wafanyakazi kama ulivyopitisha ba bunge ili sasa kufanya wafanyakazi wote wanaokatwa akiba ya mafao (PPF,NNSF, PSPF,LAPF,GEPF n.k) kulazimika kutopata mafao yao kama hawajatimiza umri wa kustaafu(55-60).Mpango huu unaletwa kwa sababu serikali yenu haina namna ya kufanya na ingependa kupata boost ya mapato toka mifuko hii ili kuleta pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mpango huu wa aibu na kandamizi utawaathiri wafanyakazi zaidi ya 700000 serikalini lakini kwa kipekee utaathiri na kuua ndoto za wafanyakazi zaidi ya 3000000 walio katika sekta binafsi kama vile makampuni, NGOs na wale waliojiajiri wenyewe na ambao wanatumia mifuko hii.
(Una imani kubwa kwamba wabunge wetu hasa wa upinzani wataupigia ngumu mpango huu nyonyaji ambao ni wa aina yake katika nchi zote za Afrika. Hii pia inatoa fursa kwa wafanyakazi wote nchini (hasa vijana) kutafakari na kuona jinsi serikali yenu inavyopanga kufifisha mipango yenu ya muda mfupi na ile ya kati. Kazi kwenu simameni na Chukueni Hatua Sasa.
HABARI NDO HIYO
Hi wana JF,
Nimesikia kuwa kuna sheria imepitishwa kuwa HAKUNA TENA kuchukua hela za NSSF ukiacha kazi HADI UMRI wa kustaafu
ufike.
Mwenye kujua UKWELI atuhabarishe zaidi (NSSF au watunga sheria wetu).
Wafanyakazi wa sekta binafsi mnalijua hili?
Sijashangazwa na michango yenu humu kwa sababu nafikiri Watanzania bado hatujaelewa maana ya pensheni ni nini, lakini huu ni utaratibu wa watu angalau kuweka akiba, ili unapofikisha umri mkubwa huna uwezo wa kufanyakazi upate maisha yenye hadhi kwa kutumia ile akiba yako ambayo sasa inaweza kufidia kiasi cha fedha kwa kukosa mshahara, maana wakati huo hujiwezi. Humu ndani kutokana na hulka ya kupenda kutumia bila kuweka akiba mnaona kama huo mpango eti utafifisha ndoto zenu wakati ile ni just 5% ya mshahara ama 10% kwa sekta binafsi, 90% unaachiwa na hufiki popote na ndoto zako, najua hii hamtaipenda, hebu jiulizeni hapo mlipo mna akiba kiasi gani mmeweka wenyewe benki voluntarily, wengi ni kutumia tu, bia na kiti moto! mimi ningeona kweli hiyo ni sawa kabisa, let u guys be forced to save because hamwezi wenyewe, eti mtu atasema anataka ajenge nyumba, tumia hiyo 90% yako. Labda sasa tungesema kwamba okay, hatuchukui fedha lakini tutunze akaunti zetu huko na tukipata pesa kwa namna yeyote basi we can conribute ila mafao labdayaongezeke zaidi. lakini siyo kuzitumbua tu hizo fedha, nchi haina savings kabisa watu wanakula bata tu. hiyo sheria na ipite ili tulazimishwe kuweka akiba. Naunga mkono hoja.