Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 59
Nilijua tu kuwa hawa Rai wanaongopa. Hii ni taarifa ya Mnyika kwa vyombo habari:
Kama Kikwete alizani anapata breki, basi ajiandae for mambo zaidi yake yawekwe wazi hapa. Kuna uwezekano zaidi wa kupata mikataba mingine ya madini iliyosainiwa wakati wa Kikwete na kama kawaida ya JF, hiyo mikataba itawekwa hapa mchana kweupe!
Hizi propaganda za Rostam zitampoteza Kikwete!
Kikwete nimeahidi kukupa zawadi kama ukisalenda kwa wapinzani na kuvunja baraza lako la mawaziri, kuwaomba msamaha watanzania, na kuomba upewe second chance ili ufanye the right thing!
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VIONGOZI WA USHIRIKIANO WA VYAMA VYA UPINZANI KUZUNGUMZA NA WANANCHI KUHUSU UFISADI
• ‘Kuanika' jinsi mabilioni mengine ‘yalivyochotwa' benki kuu
• Kutaja viongozi wa serikali walivyohusika na ‘kampuni hewa' ilivyotumika
• Kugawa mkataba wa Richmond kwa umma
Viongozi wa Ushirikiano wa Vyama Vya Upinzani vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na TLP siku ya jumapili tarehe 28 Oktoba, 2007 watazungumza na wananchi katika mkutano wa ndani kutoa taarifa kwa umma kuhusu ufisadi.
Mazungumzo hayo ya ndani ambayo wananchi mbalimbali wanaalikwa kushiriki yatafanyika katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Manispaa ya Kinondoni Jimbo la Ubungo Mkoani Dar e salaam kuanzia saa 4 mpaka saa 5 na nusu asubuhi.
Katika mazungumzo hayo viongozi wa Vyama vya Upinzani wataanika jinsi mabilioni mengine zaidi yalivyochotwa katika benki kuu ya Tanzania na kutaja viongozi wa serikali walivyohusika na ‘kampuni hewa' ilivyotumika.
Itakumbukwa kwamba tarehe 15 Septemba, 2007 katika mkutano wa hadhara uwanja wa Mwembeyanga uongozi wa ushirikiano wa vyama vya upinzani ulitaja orodha ya mafisadi nchini yenye kueleza ufisadi, wizi na/au ubadhirifu au matumizi mabaya ya rasilimali za taifa.
Pamoja na viongozi wengine pia, Dr Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu(CHADEMA) atazungumza katika mkutano huo. Dr Slaa ndiye aliyeibua hoja ya kutaka kuundwa kwa kamati teule ya kuchunguza tuhuma za ufisadi katika benki kuu na kupelekea kutangazwa kwa orodha ya mafisadi. Dr Slaa amerejea hivi karibuni kutoka Marekani ziarani nchini Marekani na Mkutano wa Bunge la Kusini mwa Afrika SADC nchini Malawi.
" Katika mkutano huu hatutataja orodha nyingine ya mafisadi. Tutajenga katika orodha ya awali ya mafisadi. Katika mkutano huu kitakachotajwa ni ufisadi mwingine uliopelekea mabilioni mengine kuchotwa katika benki kuu. Pia katika Mkutano huo tutagawa mkataba wenye utata wa Richmond kama tulivyofanya kwa mkataba wa Madini wa Buzwagi ili umma"
Imetolewa na 26/10/2007:
John Mnyika
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi na
Mkurugenzi wa Vijana Taifa(CHADEMA)
0754694553
__________________
Kizazi Kipya, Maisha Mapya
New Generation, New Life
Mabadiliko ya Kweli, Uhuru wa Kweli
Real Change, Real Freedom
John Mnyika
Kama Kikwete alizani anapata breki, basi ajiandae for mambo zaidi yake yawekwe wazi hapa. Kuna uwezekano zaidi wa kupata mikataba mingine ya madini iliyosainiwa wakati wa Kikwete na kama kawaida ya JF, hiyo mikataba itawekwa hapa mchana kweupe!
Hizi propaganda za Rostam zitampoteza Kikwete!
Kikwete nimeahidi kukupa zawadi kama ukisalenda kwa wapinzani na kuvunja baraza lako la mawaziri, kuwaomba msamaha watanzania, na kuomba upewe second chance ili ufanye the right thing!