Hakuna dawa ya kumroga mtu? maana nishaibiwa tayari na ujanja wangu huu

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
Kufanya biashara mtandaoni ni riski kubwa sana pia nawahurumua watu wanaotegemea kufanya biashara mtandaoni maana kadiri mambo yanavyobadilika hamna mtu ataamini vitu vya online ingawa ingekuwa inatumika ipaswavyo ingerahisisha zaidi kwa kuokoa muda na usalama pia.

Ila kadri siku vinavyosonga mbele mtandao unageuka kuwa wizi wa kupindukia, mfano nchi za wenzetu wako vizuri sana ingawa sijui changamoto zao ila mtu anaagiza na kupokea mzigo mlangoni. Sisi kwetu sasa ukiagiza ujue tumbo la kuhara lazima likushike hutulii mpaka mzigo uuone ndio useme afadhali.
Screenshot_20240201-202025_Drive.jpg

Jana nimeona kitu mtandaoni nikakipenda nikasema ngoja nimcheki mshikaji tuyajenge, tumeelewana vizuri na mzigo nimetuma na makubaliano ni leo nipokee changu.

Kilichonikuta Gari ambayo tulielewana anitumie imepita nampigia simu hapokei na simu kazima. Sasa mtu kama huyu anaharibu kula ya wengine wanaotegemea order za watu, na kwa hali kama hii uje unishawishi kuchukua vitu bongo tena online ni ngumu maana tayari nimeona madhara yake.

Siyo mara moja nafanya biashara online nimezoea kuagiza Alibaba.com na AliExpress.com jamaa hawana noma aisee nilishangaa naagiza kitu kimoja AliExpress naletewa mpaka Tanzania hueziamini ni cha Tsh2,000 tu.

Na muda huu napoa andika nimepokea Email ya mzigo wangu
Screenshot_20240201-194734_Outlook.jpg

Hapo nakuwa na amani maana kila hatua najua sasa sisi tunakwama wapi wizi huu mpaka lini??

Pamoja na hivyo, Mwezi wa 1 mwaka huu nimeagiza Laptop Alibaba nimepokea bila shida, na mpaka mzigo unanifikia nilikuwa najua unaenda endaje kila kituo naona kupitia track order.

Sisi watanzania ndio maana hatuaminiki iwe kwenye kazi au hata ukiomba ajira sehemu, kwenye kampuni au kwa mtu binafsi uaminifu ni sifuri, hata ndugu unamuogopa kuja kwako!!
 
Kumroga mtu inabidi umfahamu huyo mtu tofauti na hapo haiwezekani, je unamfahamu maana kunavitu nitavihitaji ilitumtengeneze chap
 
Hamna mkuu simjui najua majina yake kupitia namba zake za simu
Hapo ni changamoto kumroga kwasababu hiyo pesa ulimtumia wewe mwenyewe ingekua amekwapua au kaiba kwa kuingia ndani kwako ilikua haitajiki kumfahamu,
zingatia ndiomaana majambazi maranyingi hawarogeki kwasababu wakifika wanakwambia weka pesa humu ktk begi au wanakwambia chukua nipe hawachukui wenyewe ila vibaka ni rahisi kuwaroga
 
Naona una hamu ya kupigwa tena.
Hapana sema kwenye maisha bila kurisk hakuna kitu utafanya, angalia hata biashara hizi watu wanafungua wakiwa hawana mawasiliano na watakao wauzia ila baada muda na uvumilivu anatengeneza jina na kuwa maarufu hivyo asinge risk angekata tamaa kabla hajafika pale alipo
 
Ila kweli, kama mtu hajawahi kuibiwa hawezi jua maumivu yake... Siku nikikuta mwizi anapigwa aisee nitatoa Hela ya petrol wammalize,, niliwahi kulizwa vibaya mnoo yani😔
Mimi kuna kipindi nilikuwa nasaidia kabisa kuwachoma maana walikuwa wamezidi mtaani kwetu saizi wamehamia mtandaoni, pamoja na kwamba vijana wanaibiwa au watu wanai iwa hurumia zaidi wale kina mama ambao wanahangaika zaidi kula yao ya shida alafu linatokea jitu linamuibia mimi nikikutana na wahivi nitavua hata suluari yangu nilichomee
 
Watz wanapenda maisha ya ujanja ujanja. Hapo Bwana Mwizi Roho yake nyeupe ya baridiiiii.

Hawa Wachina wanaowekeza tz wamewaweza, taarifa zinasambaa Kwenye mfumo Ukiharibu sehemu basi kwa mchina mwengine unatemwa
Hii ni mbaya sana kwa kizazi hiki hamna mtu atakuwa ma huruma na wewe, na sasa hivi kupatakazi mpaka wafuatilie
 
Mimi kuna kipindi nilikuwa nasaidia kabisa kuwachoma maana walikuwa wamezidi mtaani kwetu saizi wamehamia mtandaoni, pamoja na kwamba vijana wanaibiwa au watu wanai iwa hurumia zaidi wale kina mama ambao wanahangaika zaidi kula yao ya shida alafu linatokea jitu linamuibia mimi nikikutana na wahivi nitavua hata suluari yangu nilichomee
Wanakera Sana aisee.. Ila Mungu anawaona
 
Kufanya biashara mtandaoni ni riski kubwa sana pia nawahurumua watu wanaotegemea kufanya biashara mtandaoni maana kadiri mambo yanavyobadilika hamna mtu ataamini vitu vya online ingawa ingekuwa inatumika ipaswavyo ingerahisisha zaidi kwa kuokoa muda na usalama pia.

Ila kadri siku vinavyosonga mbele mtandao unageuka kuwa wizi wa kupindukia, mfano nchi za wenzetu wako vizuri sana ingawa sijui changamoto zao ila mtu anaagiza na kupokea mzigo mlangoni. Sisi kwetu sasa ukiagiza ujue tumbo la kuhara lazima likushike hutulii mpaka mzigo uuone ndio useme afadhali.

Jana nimeona kitu mtandaoni nikakipenda nikasema ngoja nimcheki mshikaji tuyajenge, tumeelewana vizuri na mzigo nimetuma na makubaliano ni leo nipokee changu.

Kilichonikuta Gari ambayo tulielewana anitumie imepita nampigia simu hapokei na simu kazima. Sasa mtu kama huyu anaharibu kula ya wengine wanaotegemea order za watu, na kwa hali kama hii uje unishawishi kuchukua vitu bongo tena online ni ngumu maana tayari nimeona madhara yake.

Siyo mara moja nafanya biashara online nimezoea kuagiza Alibaba.com na AliExpress.com jamaa hawana noma aisee nilishangaa naagiza kitu kimoja AliExpress naletewa mpaka Tanzania hueziamini ni cha Tsh2,000 tu.

Na muda huu napoa andika nimepokea Email ya mzigo wangu View attachment 2890995
Hapo nakuwa na amani maana kila hatua najua sasa sisi tunakwama wapi wizi huu mpaka lini??

Pamoja na hivyo, Mwezi wa 1 mwaka huu nimeagiza Laptop Alibaba nimepokea bila shida, na mpaka mzigo unanifikia nilikuwa najua unaenda endaje kila kituo naona kupitia track order.

Sisi watanzania ndio maana hatuaminiki iwe kwenye kazi au hata ukiomba ajira sehemu, kwenye kampuni au kwa mtu binafsi uaminifu ni sifuri, hata ndugu unamuogopa kuja kwako!!
Ni aina gani ya laptop + specification uliyoagiza alibaba ukaletewe pia naomba na contacts za supplier wako,nataka kuagiza na mm.
(Seeing is believing).ukinisaidia na bei nitashukuru pia.
 
Back
Top Bottom