Fahamu chuki ni tatizo la kifikra zaidi na dawa yake hii hapa

Vincenzo Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
12,141
25,419
Sisi binadamu namna yetu rahisi ya kuelewa na kukumbuka mambo ni kwa kuyaweka mambo katika makundi mfano tunawagawa watu katika makundi kama marafiki, ndugu, watoto, maadui, warefu, wafupi, n.k. Makundi haya yanatusaidia kujenga picha ya haraka hata kama wakati fulani hatuwezi kuelezea wazi wazi kundi husika ni nini haswa na pia kunaweza kuwa na tofauti kati ya watu au vitu katika kundi husika.

Mtindo huu wa kutambua vitu au watu kwa makundi ndio unaopelekea pia kuwepo kitu tuiitacho kwa kiingereza PREJUDICE yaani CHUKI.

Kwakuwa umezoea kuwaweka watu katika makundi fulani, na kuwatambua watu kwa makundi kutokana tayari na aina ya picha ya kundi husika , basi waweza kujikuta ukiwaweka tuu watu katika makundi na kuwatafsiri hivyo, ingawaje sio sahihi kwani ingawaje wewe unafikiria na kutambua kwa njia ya MAKUNDI, kumbuka kuna utofauti mkubwa kati ya mtu aliyepo katika KUNDI na maana unayoipa KUNDI husika.

Hivyo unaweza kumtafsiri mtu kuwa MVIVU/MWIZI/MWONGO kwa sababu tuu unamuona yupo katika kundi fulani ambalo wewe huwaita wavivu/Wezi/waongo, ila kiukweli huyo mtu mmoja sivyo unavyodhani.

Mara ngapi umesikia mtu akisema "Vijana wa siku hizi wavivu", na wengine wamekosa kazi kwa sababu tuu eti wamemaliza chuo fulani hivyo "hawana ujuzi".

CHUKI au PREJUDICE ni pale unapowatafsiri watu wengine VIBAYA kwa sababu kiakili yako wapo katika MAKUNDI ambayo ni mabaya. Unaamini kwa mfano kila anayefanya biashara ONLINE ni tapeli, kila mwenye NGO basi ni tapeli, kila MNIGERIA ni mwizi, n.k

Kumbuka ili kuzuia CHUKI ya namna hii jitahidi kufikiria na kuwaona watu kama mtu mmoja mmoja na sio sehemu ya kundi.

Kuwa makini na namna unavyotafsiri watu kwa kuangalia UMRI , JINSIA, UTAIFA, DINI, KABILA, AINA YA KAZI, MIJI WANAPOTOKA, MAHALI WANAPOISHI n.k

Pia jichukulie wewe ndio ungekuwa una tafsiriwa vibaya ungejisikiaje ?
 
Binadamu Huwa tunawawazia wengine vibaya,ndo maana kwenye biblia imehimizwa kumpenda jirani Yako kama nafsi Yako!
 
matatizo mengi mathalani afya ya akili na magonjwa ya moyo na mashinikizo ya damu, yamechochewa pakubwa sana na chuki binafsi ambazo tunang'ang'ana nazo kila siku na hatimae huchakaza afya za mioyo yetu na kukatisha zawadi ya uhai tulopewa na Mungu gafla.

Ukiachlia magonjwa,
chuki huchochea mafarakano, mapigano, mauaji na maangamizi mabaya sana ya kimwili na kiroho..

Tumuombe Mungu atujalie atujalie sote tuwe wepesi wa mioyo yetu migumu kusameheana kwani hiyo ni miongoni pia mwa tiba mujarabu ya chuki...
 
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom