Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Hakuna binadamu anayekupenda kwa dhati

Karne hii inataka binadamu akupende!!!! mweeh.... Jipende mwenyewe. Jali afya yako, kazi inayokuingizia kipato, jali ndoto zako. Mungu akikujalia familia ipende na ihudumie lakini usibweteke maana hata watoto wako wanaweza wasikupende... jiwekee akiba. Furahia maisha. Mtegemee Mungu maana amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu.
 
Tumesha sema na tunarudia kusema marafiki unaokutana nao ukiwa umeshafanikiwa au mmekutana nao kazini hao kuwa nao Makin wengi wao siyo marafiki maana siku ukianguka au ukapoteza kazi Basi na urafiki wenu utakua umeishia hapo na mazoea hatataka kabisa.

Jaribu kufikiria kipindi ukiwa haujafanikiwa au ulipokua hauna kazi kuna marafiki hata kama siyo wengi basi Kuna rafiki ambae alikua mtu wako wa karibu na alishakusaidia mambo flanflan hata kama siyo ya kipesa lakin hata ushauri wake au alikupa moyo ukiwa kwenye majaribu fulani , hao ndo wanakuaga marafiki wa kweli lakin kwa bahat mbaya huwa tukifanikiwa kidogo huwa tunawatupa hata Salam tunakata na badae tunaanzisha urafiki na watu fake.

Marafiki weng wa kazn urafiki wao huwa unakuzwa sana nyakati za starehe na pombe, ukiweza kujitenga na pombe au mambo ya starehe hapo kazin kwenu hautakua na rafiki wa karibu hata mmoja isipokua utabak urafiki wa kukutana ofisin tu.
Maneno kuntu kabisa.Aisee Barikiwa Sana Mkuu.Nimejifunza Sasa hivi MUNGU akinisaidia nikarudi kwenye mstari nitakuwa makini Sana,Bora nimsaidie maskini asiye na uwezo,naamini nitapata thawabu kwa MUNGU kuliko rafiki aliyejileta wakati nikiwa na hali nzuri.
 
Karne hii inataka binadamu akupende!!!! mweeh.... Jipende mwenyewe. Jali afya yako, kazi inayokuingizia kipato, jali ndoto zako. Mungu akikujalia familia ipende na ihudumie lakini usibweteke maana hata watoto wako wanaweza wasikupende... jiwekee akiba. Furahia maisha. Mtegemee Mungu maana amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu.
Sawa Mkuu.Ishu ni kwamba wewe unakuwa mtu mwema kwa wenzako kwa kuamini kuwa ni watu wema hivyo ni watu wa upendo, hivyo unajitoa ktk shida zao,lkn sasa ukija kubanwa na matatizo makubwa unakuta wanakukumbia na kukugeuka kabisa,hapo ndo shida ilipo.
 
Rafiki wakweri ata kwenye shida yuko tayali kukusaidia, huyu ndiyo rafiki wakweli.

Mimi cna rafiki bwashee
Umeamua kuto kuwa na rafiki au umeona hakuna mtu anayefaa kuwa rafiki yako??.
 
Sawa Mkuu.Ishu ni kwamba wewe unakuwa mtu mwema kwa wenzako kwa kuamini kuwa ni watu wema hivyo ni watu wa upendo, hivyo unajitoa ktk shida zao,lkn sasa ukija kubanwa na matatizo makubwa unakuta wanakukumbia na kukugeuka kabisa,hapo ndo shida ilipo.
Nimekuelewa. Ninachosema ni kuwa karne hii ishi kwa akili. Tenda mema lakini usibweteke. Jiwekee na ujiandae na maisha bila kumtegemea binadamu.
 
20210915_095959.png
 
Umekata tamaa sana, kuna wanaokupenda ila hawajapata access na wewe. Mwanadamu yoyote anapendwa na wastani wa watu wasiopungua 5 kati ya billion 7 waliopo.

Kule kwetu kuna usemi wa "mbwa hakosi wifi" ukilenga kumaanisha hakuna "aso mtu"..
 
Back
Top Bottom