Kenya 2022 Hakika hakuna cha kujifunza kutoka katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya

Kenya 2022 General Election
Usishindane na dola yoyote kwenye masuala ya uchaguzi, matokeo yake huwa yanajulikana ukifanya nao ushindani wa aina yoyote ile. Watakachokuambia kazi yako ni kutii tu bila shuruti.
 
1660475924469.png
 
Habari za weeknd wakuu..!

Kwa wale tunaoendelea kufuatilia uchaguzi wa majirani zetu naomba nitangulize pole zangu za dhati kwa wote kutokana na kile kinachoendelea.

Baadhi yetu tuliposema kwamba Tume ya uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) inajiandalia bomu yenyewe kwa kuruhusu media kurusha matokea ya uchagzui huo wapo wana JF walikuja na na mapambio ya media freedom.

View attachment 2323548

Wengine mlikuja na miluzi mingi ya oooh....tujifunze kwa wenzetu...mara oooh kenya baba wa demokrasia...!! Kiko wapiiii?? hadi leo IEBC wanarukaruka na sarakasi za matokeo huku pande zote TEAM BABA (ODINGA) NA TEAM HUSTLERS (RUTO) zimeshaitangaza washindi kutokana na matokeo ya vyombo vya habari ...kwanza nchekee...ha ha ahaaa.

KWA MATUKIO HAYA NDUGU ZANGU NAWAAMBIA WAMESHAFELI...TUWAOMBEE TU WASIPIGANE MAANA HAYA YANAYOENDELEA HAYATAWAACHA SALAMA NA NATHUBUTU KUSEMA TANZANIA HATUNA CHA KUJIFUNZA KATIKA UCHAGUZI WA KENYA ILA IEBC INAPASWA KUJIFUNZA KWETU.
Kenya wote wezi
 
Ukiwa na akili timamu, mkweli wa nafsi na asiye na unafiki, utakiri kikamilifu, bila shaka kuwa uchaguzi wa Kenya ni mfano mzuri wa pekee kwa Afrika nzima, na Asia (ukiondoa Japan, Singapore na Malaysia).
Uwongo mtupu, mbona mpaka sasa hawajatangaza matokeo? Kenya kuna ushindani wa ki kabila,na sio uchaguzi. Hakuna la kujifunza Kenya.
 
Hayo ni mapungufu kidogo sana tofauti na Tanzania ambapo mapungufu ni mengi sana
We huna akili, yaani kwenye kituo watu wamejuandisha 100,alafu Kura ziwe 1700 kwenye kituo hicho hicho,alafu useme hayo ni mapungufu madogo?!
 
Hayo uliyoyataja ni mapungufu madogo kutokana na watu ambao sio waadilifu na hao kokote wanakuwepo,Bali IEBC inachelewa kutangaza matokeo kwakua inapitia na kujiridhisha Kila hatu na kura zote kwa usahihi na uwazi ili Kila upande mwisho wa siku uridhike.Laiti Kama ingekua ni bongo rais mteule kashajulikana kwakua tume Haina muda wa kujiridhisha kwamba mweny kura nyingi kazipataje pataje ni vurumai tu.
IEBC Ina vission na mission tofauti na NEC yetu ambayo haijui hata inatekeleza Nini na kusimamia Nini yapelekwa na serikali nawala hakuna Cha kuifanya kwakua yalindwa na serikali.
 
Nikiwa napitia katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini niliona baadhi ya wanaharakati, wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani wakidai kuwa Tanzania inapaswa kujifunza kutoka uchaguzi Mkuu wa Kenya. Wakidai kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki.

Kwa ufuatiliaji nilioufanya katika uchaguzi huo kwa kweli sijaona hicho kinachodiwa kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki. Sioni kama kuna la kujifunza kutoka katika uchaguzi huo kwa sababu zifuatazo:-

#13/08/2022 Daniel Musyoka Msimamizi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) aliripotiwa kutoweka na mpaka sasa haijulikani alipo.

#13/08/2022 iliripotiwa kuhusu uwepo wa dalili za wizi wa kura katika baadhi ya maeneo ambayo inadaiwa William Ruto amepata kura nyingi ambapo ilielezwa kuwa kura katika vifaa vya KIEMS hazilingani na idadi iliyopo katika Makaratasi.

#12/08/2022 iliripotiwa kuwa Maafisa wa Tume wameitisha Kikao cha Dharura baada ya sintofahamu kutokea katika Ukumbi wa kuhakiki kura za Urais, baada ya Kompyuta kuingizwa ukumbini kinyume na Taratibu.

#12/08/2022 iliripotiwa kuhusu msimamizi wa uchaguzi kukutwa na karatasi za kupigia kura katika kituo cha kuhesabia kura cha Jamhuri katika Jimbo la starehe.

#10/08/2022 iliripotiwa kuwa Polisi wawili na Raia mmoja walikutwa na karatasi za kupigia kura zenye tiki. Pia, Miongoni mwa vifaa vingine vilivyokutwa nao ni sahihi moja ya wapiga kura, Madaftari 2 ya matokeo ya Uchaguzi, pakiti mbili za karatasi za kupigia kura za Urais.

# Kubwa zaidi na la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haijatangaza matokeo ya kura za Urais pasipo sababu za msingi huku siku zikizidi kwenda hii inatilia mashaka juu ya matokeo yatakayotangazwa kama yatakuwa na uhalisia.

Katika mazingira haya, kweli watanzania wenye akili timamu wanawezaje kuishauri serikali iige kinachotokea Kenya? Ni kweli kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wataweza kusubiri wiki nzima bila kujua aliyeshinda?.

Kitendo cha Vyombo vya habari kutangaza matokeo kiliwafanya wanaharakati pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani kuamini kuwa kufanya hivyo ndio uhuru na haki, tujiulize hiyo haki sasa iko wapi? Hivi hamuoni kuwa mlijichanganya kuwahi kuongea bila kufukiria mwisho wa mnachokisema utakuwa nini? Kutofikiria kwenu kumewafanya mkose la kuongea baada ya hali inayoendelea kujitokeza.

Hii ni ishara ya ukosefu wenu wa uweledi katika mambo makubwa yanayohusu uongozi wa nchi.
Mmmmh yaani upuuzi wa Tanzania ya ccm,unasema unafanana na Uchaguzi wa Kenya!?inawezekana Uchaguzi wa Kenya usiwe Bora kwa asilimia 100,lakini huwezi kulinganisha na upuuzi mavi wa chaguzi za Tanzania,ni bongo pekee,ambapo Kuna watu wanapita bila kupingwa!!simu haziruhusiwi kwenye vyumba vya kuhesabia kura,mgombea anapata kura nyingi kuliko idadi ya wapiga kura!!ilitokea chato hii,kwa shetani Jiwe.
Kenya kuna wagombea binafsi,bongo hakuna,tume ya Kenya haichaguliwi na Raisi,hii ya kwetu ni kama mahouse boy wa Samia na Ikulu,Kenya matokeo ya Uraisi yanapingwa mahakamani,bongo yakishatangazwa yanakuwa msahafu.
 
Kujifunza inatakiwa uangalie na utathmini yote mazuri na mabaya na kuyafanyia kazi. Uchaguzi wa Tz 2019/2020 ulikuwa mavi ya kuku (kwa sauti ya kibaki-rip). Hatukuwa na uchaguzi bali uchafuzi.
 
Hapa ni uhalifu tu. Na kama kweli umefuatlia, inadaiwa matukio ya kupotea kwa watu ktk eneo hilo ni ya kawaida. Kwahiyo hayana uhusiano na uchaguzi.

Acha kujikuna upele wenye harufu mbele za watu halafu (uchafuzi Tanzania) ukaufananisha na chunusi (uchaguzi Kenya)
Kweli kabisa hata hapa tz wapo wanao kimbia madeni na kwenda nje ya nchi na wengine hufanya uhuni kibao mitaani wakiajibishwa na jamii utasikia sababu za kisiasa tu ndio zilizowaponza
 
Back
Top Bottom