MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Nikiwa napitia katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini niliona baadhi ya wanaharakati, wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani wakidai kuwa Tanzania inapaswa kujifunza kutoka uchaguzi Mkuu wa Kenya. Wakidai kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki.
Kwa ufuatiliaji nilioufanya katika uchaguzi huo kwa kweli sijaona hicho kinachodiwa kuwa uchaguzi huo ni huru na wa haki. Sioni kama kuna la kujifunza kutoka katika uchaguzi huo kwa sababu zifuatazo:-
#13/08/2022 Daniel Musyoka Msimamizi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi (IEBC) aliripotiwa kutoweka na mpaka sasa haijulikani alipo.
#13/08/2022 iliripotiwa kuhusu uwepo wa dalili za wizi wa kura katika baadhi ya maeneo ambayo inadaiwa William Ruto amepata kura nyingi ambapo ilielezwa kuwa kura katika vifaa vya KIEMS hazilingani na idadi iliyopo katika Makaratasi.
#12/08/2022 iliripotiwa kuwa Maafisa wa Tume wameitisha Kikao cha Dharura baada ya sintofahamu kutokea katika Ukumbi wa kuhakiki kura za Urais, baada ya Kompyuta kuingizwa ukumbini kinyume na Taratibu.
#12/08/2022 iliripotiwa kuhusu msimamizi wa uchaguzi kukutwa na karatasi za kupigia kura katika kituo cha kuhesabia kura cha Jamhuri katika Jimbo la starehe.
#10/08/2022 iliripotiwa kuwa Polisi wawili na Raia mmoja walikutwa na karatasi za kupigia kura zenye tiki. Pia, Miongoni mwa vifaa vingine vilivyokutwa nao ni sahihi moja ya wapiga kura, Madaftari 2 ya matokeo ya Uchaguzi, pakiti mbili za karatasi za kupigia kura za Urais.
# Kubwa zaidi na la kusikitisha ni kwamba mpaka sasa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) haijatangaza matokeo ya kura za Urais pasipo sababu za msingi huku siku zikizidi kwenda hii inatilia mashaka juu ya matokeo yatakayotangazwa kama yatakuwa na uhalisia.
Katika mazingira haya, kweli watanzania wenye akili timamu wanawezaje kuishauri serikali iige kinachotokea Kenya? Ni kweli kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wataweza kusubiri wiki nzima bila kujua aliyeshinda?.
Kitendo cha Vyombo vya habari kutangaza matokeo kiliwafanya wanaharakati pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani kuamini kuwa kufanya hivyo ndio uhuru na haki, tujiulize hiyo haki sasa iko wapi? Hivi hamuoni kuwa mlijichanganya kuwahi kuongea bila kufukiria mwisho wa mnachokisema utakuwa nini? Kutofikiria kwenu kumewafanya mkose la kuongea baada ya hali inayoendelea kujitokeza.
Hii ni ishara ya ukosefu wenu wa uweledi katika mambo makubwa yanayohusu uongozi wa nchi.