Kuelekea Uchaguzi, Mbinu zipi hutumika kuiba kura?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,542
Salaam, Shalom!

Wakati tukielekea uchaguzi, vyama hutoa malalamiko kuwa wanaibiwa kura na kwakuwa tunapambana kuhakikisha, tunapata Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, ni vyema tukazizua Mbinu waovu ambazo huzitumia kuiba kura.

Unapokaribia uchaguzi, kuna viongozi hupita nyumba hadi nyumba wakirekodi namba za vitambulisho vya wapiga kura, matumizi hasa ya namba hizo ni zipi?

Kinga ni Bora kuliko Tiba.

Karibuni 🙏
 
2020 hapa mtaani kwetu kituo cha kupiga kura ilikuwa ofisi ya kitongoji. Siku ya kupiga kura badala ya kuwa na kituo kimoja, vikawa vitu vitatu- yaani watu wakapiga kura 1) ndani ya ofisi ya kitongoji, 2) ndani ya room nyingine iliyo kwenye jengo hilo na 3) kwenye nyumba nyingine iliyo jirani kama MITA 20 Hivi. Sasa vyama vya upinzani vilikuwa na wakala mmoja mmoja tu, ambao hawangeweza kuona nini kinaendelea katika sehemu zote tatu. Walinzi mgambo waliokuja kusimamia usalama (hawakuwa wenyeji) kila mmoja alikuwa na kibegi cha mgongoni- vinavyofanana. Saa ya kuingia vibegi vimejaa vyote, saa ya kutoka vyote tupu. Chakula kuna ma ntilie aliwahidumia. Jiongeze mwenyewe ujie nini kiliendelea hapo.

Kuna mtu aliwahi kusema wanazo mbinu zaidi ya elfu moja
 
2020 hapa mtaani kwetu kituo cha kupiga kura ilikuwa ofisi ya kitongoji. Siku ya kupiga kura badala ya kuwa na kituo kimoja, vikawa vitu vitatu- yaani watu wakapiga kura 1) ndani ya ofisi ya kitongoji, 2) ndani ya room nyingine iliyo kwenye jengo hilo na 3) kwenye
Tuseme labda waliona idadi ya wapiga kura ni kubwa, wakafanya hivyo kuondoa msongamano.

Mawakala waliruhusiwa kuingia ndani ya kituo mlichokitilia mashaka?
 
Salaam, Shalom!!

Wakati tukielekea uchaguzi, vyama hutoa malalamiko kuwa wanaibiwa kura na kwakuwa tunapambana kuhakikisha, tunapata Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, ni vyema tukazizua Mbinu waovu ambazo huzitumia kuiba kura.

Unapokaribia uchaguzi, kuna viongozi hupita nyumba hadi nyumba wakirekodi namba za vitambulisho vya wapiga kura, matumizi hasa ya namba hizo ni zipi?

Kinga ni Bora kuliko Tiba.

Karibuni 🙏
Kuna kuiba kura na kuiba uchaguzi.

Ukiwa na ujinga kama kupita bila kupingwa, ukiwa unateua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, ikiwa unachanganya resources za serikali na chama kwenye uchaguzi, hapo unaiba uchaguzi, huibi kura tu.
 
Kura huwa haziibiwi Bali washabiki wa chadema Huwa ni kelele za majukwaani tu, ikifika muda wa kupiga kura hawaendi kwenye vituo vya kupiga kura!
Hilo Lina UKWELI,

Lakini nimewahi kusikiza shauri Moja la kukata shauri la mgombea wa upinzani,

HOJA yake ilikuwa kura kuzidi,

Yaani waliopiga Kwa Mfano ;

Idadi jumla ya wapiga kura iwe10,000/=

Mgombea chama A apate kura 7,000

Mgombea chama B apate kura 4,000

Wagombea wengine kura 500

Kura zilizoharibika 500.

Anahoji kura 2000 zilitoka wapi? Na ziliingiaje ndani ya Sanduku la kura, au zimeongezeka wakati wa kutangaza matokeo?
 
Leo tunajadili kura zinaibiwaje!

Karibu
Sasa unajadili kura zinaibiwaje wakati watu wanapita bila kupingwa hata kura hawapigiwi?

Unajadili kura zinaibiwaje wakati hata kura zisipoibiwa matokeo yanaweza kubadilishwa?

Kwa nini unaona kujadili kura zinavyoibiwa ni muhimu kuliko kuangalia mfumo unaowezesha kura kuibiwa?

Ukiweza kudhibiti kura zinavyoibiwa leo, wakati umebakisha mfumo ule ule unaowezesha kura kuibiwa, huoni kwamba bado umeacha mwanya wa kura kuibiwa kivingine kesho?

Una kifua kikuu kinachokufanya ukohoe sana, kwa nini unapoteza muda mwingi kupata dawa ya Cofta ya kupunguza kikohozi, kupunguza daliki tu, wakati ugonjwa wa msingi, kifua kikuu, unauacha?
 
Hatuwezi kujadili mambo yote Kwa pamoja,

Jikite kwenye mada.
 
Ww utakuwa ni mzee lazima, wazee ndio Bado wanatembea na hii propaganda outdated.
Mkuu ila kuna ukweli pia kwamba wafuasi wa CHADEMA ni wavivu kupiga na kuzilinda kura zao, kuna wingi wa kura ukifikia hata kuibiwa na matokeo kupinduliwa inakuwa vigumu sana, ndio maana wabunge wengi wa upinzani wanaoshinda na kufanikiwa kuupata ubunge huwa wanashinda kwa gap kubwa sana la kura.
 
Sasa unajadili kura zinaibiwaje wakati watu wanapita bila kupingwa hata kura hawapigiwi?

Unajadili kura zinaibiwaje wakati hata kura zisipoibiwa matokeo yanaweza kubadilishwa?

Kwa nini unaona kujadili kura zinavyoibiwa ni muhimu kuliko kuangalia mfumo unaowezesha kura kuibiwa?

Ukiweza kudhibiti kura zinavyoibiwa leo, wakati umebakisha mfumo ule ule unaowezesha kura kuibiwa, huoni kwamba bado umeacha mwanya wa kura kuibiwa kivingine kesho?

Una kifua kikuu kinachokufanya ukohoe sana, kwa nini unapoteza muda mwingi kupata dawa ya Cofta ya kupunguza kikohozi, kupunguza daliki tu, wakati ugonjwa wa msingi, kifua kikuu, unauacha?
Kwa maana hii ni kwamba hakuna maana saana ya wafuasi wa upinzani kujisumbua kupiga kura kabla mfumo haujabadilishwa?
 
Salaam, Shalom!

Wakati tukielekea uchaguzi, vyama hutoa malalamiko kuwa wanaibiwa kura na kwakuwa tunapambana kuhakikisha, tunapata Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, ni vyema tukazizua Mbinu waovu ambazo huzitumia kuiba kura.

Unapokaribia uchaguzi, kuna viongozi hupita nyumba hadi nyumba wakirekodi namba za vitambulisho vya wapiga kura, matumizi hasa ya namba hizo ni zipi?

Kinga ni Bora kuliko Tiba.

Karibuni 🙏
Hakuna wa kuiba kura msiwe na wasi wasi aliyekuwa anaiba kura ameshakufa mwendazake
 
Msimsingizie,

Yeye hakuwahi kutuhumiwa kuiba kura,

Mfumo ulliiba uchaguzi,

Kuhusu kuiba kura, aliyenadi msemo wa BAO la mkono, anatakiwa achangie hapa.
 
Mkuu ila kuna ukweli pia kwamba wafuasi wa CHADEMA ni wavivu kupiga na kuzilinda kura zao, kuna wingi wa kura ukifikia hata kuibiwa na matokeo kupinduliwa inakuwa vigumu sana, ndio maana wabunge wengi wa upinzani wanaoshinda na kufanikiwa kuupata ubunge huwa wanashinda kwa gap kubwa sana la kura.
Mkuu achana na hizo story, kwa macho yangu nimeshuhudia kura za wizi tena kwa uratibu wa polisi na msimamizi wa uchaguzi. Kisha utetezi ukawa wapiga kura wa upinzani hawajitokezi! Na wale waliomua kutetea uchafu ule kwenye uchaguzi wakapewa kesi ya kutaka kuvuruga uchaguzi!

Haya ni mambo yanayofanyika kwa uwazi sana. Kipindi Cha Magufuli uchaguzi ndio ukawa uchafu wa hali ya juu. Na huu ushenzi unaoendelea kwenye chaguzi zetu sio jambo la hisia ama kusikia, na ushahidi wa wazi upo. Kwa Sasa nikiona mtu anaendelea kwenda kushiriki kwenye hizi chaguzi za kishenzi chini ya mazingira haya, namuona hana kazi za kufanya, ama ni mfaidikika wa huo mfumo mbovu.
 
Hakuna wa kuiba kura msiwe na wasi wasi aliyekuwa anaiba kura ameshakufa mwendazake
Magufuli hakuiba kura, Bali alipora mchakato wa uchaguzi, wezi wa kura ni ccm na mfumo huu mbovu wa uchaguzi. Kama Bado tume ya uchaguzi itaendelea kuwajibika kwa mwenyekiti wa ccm, ni ujinga kama ujinga mwingine kuendelea kushiriki huo uhayawani.
 
Back
Top Bottom