HakiElimu vs Govt: The saga

Tusisahau kuwa fani ya ualimu imekuwa ndio popular kimbilio kwa wale wote wanaopata division 4 na ziro(mduara!) so we should expect some of hivi vijimambo. I just wish tungekua tunajivunia lugha yetu zaidi na kuitumia kufundishia masomo yote hata mpaka ngazi za juu!
 
Mimi nafikiri tatizo si Lugha ipi itumike,bali ni QUALITY ya wale wanaoingia katika taaluma hii ya ualimu.

Hapo awali miaka ya 60's,70's,80's mpaka 90's mwanzoni, kulikuwa na walimu wale waliofundishwa kipindi cha mkoloni na soon after that.

Backthen Ualimu ilikuwa taaluma yenye heshima,being a Teacher , lilikuwa ni suala la heshima mtaani.Kupata nafasi ya kusomea ualimu ,requirements zake zilikuwa za uhakika,ndiyo maana tukawa na walimu hao ninaowazungumzia hapo.

Mimi nadhani kuwa LUGHA si tazizo.

By the way fikiria haya yafuatayo:

Fikiria vitabu vyote tulivyonavyo katika sekondari na vyuo vibadilishwe kutoka English to Swahili kwa maana ya kuvitafsiri.Je, gharama za posho ya wale wataotafsiri itakuwa kiasi gani? ukizingatia siku zote za mradi huo.

Gharama za makaratasi,gharama za uchapishaji,ghrama za binding n.k
Mradi huu wa kubadilisha Lugha ya kufundishia mashuleni na vyuoni ni mkubwa mno,unahitaji fedha nyingi ambazo hatuna.NDIO MAANA HAO VIONGOZI WETU WANALIZUNGUMZA KISIASA ZAIDI.

Mjapani,Mjerumani,Mfaransa,Mkorea, wameweza kutumia lugha zao kutokana na uwezo wa kumudu gharama hizo na nyingine ambazo zipo associated na mradi kama huo.

Waswahili tunasema kupanga ni kuchagua,je,tupeleke pesa kwenye mradi kama huo au tujenge barabara?

Naomba kuwasilisha.
 
Fikiria vitabu vyote tulivyonavyo katika sekondari na vyuo vibadilishwe kutoka English to Swahili kwa maana ya kuvitafsiri.Je, gharama za posho ya wale wataotafsiri itakuwa kiasi gani? ukizingatia siku zote za mradi huo.
Suppose gharama ndio sababu pekee inayoleta kigugumizi, tunaweza kuichukulia hiyo kama challenge and not as a problem or an obstacle. Ukitizama, hii ni moja ya namna ya kutengeneza ajira.
Utekelezaji wake si lazima uwe wa ghafla.



.
 
Ni kweli suala la lugha katika kufundishia mashuleni imekuwa ni tatizo. Binafsi nimeshuhudia mwalimu mmoja siku si nyingi akifundisha kwa kutumia lugha zote mbili yaani kiingereza na kiswahili. Kwa kweli ni kazi kweli kwa waalimu ingawa nimesikia baadhi ya wana jf wakiwakejeli. Lakini kama mgelijua jinsi waalimu wanavyoangaika kuona kwamba wanafunzi wake wanaelewa anayofundisha wangeonewa huruma. La ajabu leo hao hao wanafunzi waliofundishwa kwa lugha mbaya hiyo, ndiyo waliofanikiwa, na wanawakejeli. Pole walimu msikate tamaa.

Shida kubwa inakuja pale mwanafunzi anapoingia katika exam room ambako kila kitu kinakuja kwa kiingereza tupu naye anatakiwa ajibu kwa kiingereza tu. Au mtahiniwa akijibu kwa kiswahili anaruhusiwa? wale walimu wanaofanya making kwenye mitihani ya O level na A level ebu tutonye kidogo. Na hapo ndipo wasi wasi wangu unakuja kuhusiana na kuwafundisha wanafunzi wa sekondari kiswahili.

Hata hivyo nakubaliana na hoja kwamba ni vizuri kwamba masomo yetu kuanzia msingi hadi chuo kikuu yaendeshwe kwa kiswahili. Hili ni sawa kabisaa. Hata hivyo lazima tukubali na hiyo haina mjadala kwamba bado ni costly exercise kubadilisha kutoka mfumo wa kiingereza kwenda wa kiswahili. Tukubali, tukatae hili ni ghali. Na kama alivyosema Bonnie1974 hili liko katika uchaguzi wetu na vipaumbele vyetu wenyewe kutegemeana na resources zetu pia. Tusianze tu kulaumu bila kuangalia yote haya.

Na kwa upande mwingine nadhani kama tuko serious na jambo hili la kubadilisha kiswahili as media language ya kufundishia, basi nyie wataalamu ebu anza kufukiria ni vipi tunaweza kuanza step by step bila kuathiri wale wanaosonga mbele. Kwa mfano kama tukisema tunaanza na chekechea kisha tunandelea step by step kwenda shule ya msingi yaani darasa la kwanza na kuendelea. Je huyo akija fika O level kabla mabadiliko hayajafika huko itakuwaje?

Miaka ya 70 tulijaribu kufanyiwa hivi hivi baada ya kubadirisha ufundishaji kutoka kiingereza kwenda kiswahili na ilikwenda mpaka la 7 na baada ya hapo kwisha hakuna kilichoendelea. Na kwa kweli wanafunzi walipokuwa wanaingia form 1 ilikuwa kazi kweli. Yaani mtu unaanza tena kujifunza lugha. Nakumbuka mwaka 1972 nilipokwenda form 1 ilikuwa inabidi miezi kama mitatu ya kwanza walimu waanze kufundisha lugha ya kiingereza tu ili tuweze kwenda pamoja. Namkumbuka mwalimu wangu mmoja alikuwa akiitwa Mr. Miller ni mmarekani huyu. Kila alipokuwa akifundisha mimi ilikuwa inanilazimu niuchape usingizi kwa kusikia nyimbo zake zisizoeleweka, maana nilikuwa nikisikia woooo waaa wooo, yaani nilikuwa sipati kitu kabisa. Ilinichukua karibu mwaka mzima hata kuielewa accent yake tu. Hapo utagundua kwamba kuna kazi.

Tunalotakiwa hapa jf ni kujaribu kushauriana je ni njia gani tunaweza kutumia kuleta mabadiliko bila kuathiri upande mmoja. Tusije kuwa kama Mungai ambaye alijaribu kuleta mabadiliko yasiyo na tija bali confussion na sasa inatu cost kubadilisha tena!
 
Na kwa kweli wanafunzi walipokuwa wanaingia form 1 ilikuwa kazi kweli. Yaani mtu unaanza tena kujifunza lugha.
Linguists wamefanya research kadhaa; nimeona discussion moja nadhani ni hapa JF katika reply aliyotoa professor mmoja wa Norway kwa professor Omary wa mlimani (I can't locate it now). Nilichojifunza kwenye hiyo post ni kwamba pengine kilichopungua ni waalimu professional at teaching english as a second language.



.
 
Sasa ina maana hata hatua za kurekebisha hilo tatizo tumeshindwa kuchukua?
ni woga wa viongozi au ni nini?
 
Hali waliyowasilisha ni ya ukweli na si kwa kiwango cha shule za sekondari tu hali ni mbaya kwani ipo ivo ivo mpaka vyuo vikuu thus the reality....watu wanamisingi mibovu sana toka chini matokeo yake hadi vyuoni....ni huruma jamani inabidi kuchangamkia hili
 
Ni tangozo lililobeba sura mbili:ya kwanza linachekesha kuona mwalimu na madenti wake wakiharibu lugha ya wenyewe, ya pili linahuzunisha kwa kuwa ndio ukweli uliopo kwenye shule zetu nyingi.
Yaani ukweli huu unauma na unafhata hamu ya kucheka tunapoliona tangazo hili.

Mwalimu na mapengo yake kingeredha kinakuwa ishu !
 
Ni kweli kabisa lazydog.

walimu mahiri wapatikane wa kufundisha hio lugha, kama somo la lugha, ngoja nisome hio aticle nitarudi.

Hili swala kwa nini halitolewi maamuzi mapema, hata sielewi, mbona ni wazi tu? Au wanaogopa nini.

Mbona watanzania tunapelekwa nchi zingine kufundisha kiswahili, kama hapa hakuna anaekijua kingereza basi tuombe msaada.

Mimi ningependa kifundishwe kwa umahiri kabisa kama foreign language, basi.
kama ni mitihani toefl waweke hio service karibu zaidi na wahitaji.
 
Nimeisoma na nakubali 110% Lazydog. ni muhimu sana lugha ya kwanza ya mtoto ndio iwe lugha ya kujifunzia elimu dunia.
Hatuko hapa wala pale tuko kichakani.
 
Nimepita kwenye banda la maonyesho ya taasisi za umma jana. Ninashukuru kuwa wameona hilo tangazo na wanalichukulia kama changamoto kubwa sana.
Sasa wanaanza na mtaala wa walimu wa walimu ambao utawasaidia kuwapata walimu wazuri, baada ya hpo wataimarisha vyuo vya ualimu hatimaye watafikia wanafunzi, sijui itakuwa lini lakini anyway, Tanzania is poa tu.
 
Elimu au lugha inayotumiwa? Ni ukweli uliowazi kwamba mtu akitumia lugha ya kuzaliwa, mother tongue, katika kujenga misingi ya elimu ni bora sana. Kwani lugha itumikayo nyumbani katika shughuli za kila siku ndio msingi mkuu. Kujaribu kufananisha hali ilivyo katika nchi zilizoendelea, kwa maana ya kwamba walikuwa na ujuzi wa kuweka mawazo yao katika maandishi tangia zamani, na nchi zetu hususa za kiafrika katika matmizi ya lugha mashuleni si sahihi. Nchi zetu zina hicho kilema kikuu cha jinsi ya kutunza kumbukumbu. Nimesoma shule tokea drasa la tano hadi juu kwa lugha ya kiingereza kwa hiyo nafahamu ugumu wa transition toka kiswahili kwenda kiingereza bila kuwa na walimu wa zuri wa lugha na vitabu vya kiada vya kutosha. Tulifundishwa lugha kama nyenzo ya kutuwezesha kuelewa masomo mengine. Naamini ukosefu wa walimu wa kufundisha lugha na vitabu vya kiada ndio tatizo kubwa katika kumwezesha mwanafunzi kuimudu na kuitumia kama nyenzo muhimu katika safari yake ya kutafuta elimu.

Lugha ya kufundishia katika nchi zilizoendelea ni ile ya nyumbani kwani wanavitabu, walimu na 'pride' ya kutumia lugha zao. Naishi Ubelgiji, kila mwaka kuna maonyesho ya vitabu vipya kwa lugha yaoau vilivyotafsiliwa. Nikiangalia kiasi cha vitabu na wingi wa wakazi siamini kuwa vyote hununuliwa lakini hiyo haiwafanyi waache kuchapisha. Serikali yao huwapa ruzuku ya aina fulani ili kuhakikisha lugha yao haiendi kaburini. Masomo toka chekechea hadi digrii ya kwanza ni lazima yawe kwa lugha yao, na hii ndio ilivyo katika nchi hizi. Lugha ya pili (kifaransa au kiholanzi) hufundishwa kuanzia darasa la tano kwakuweza kuongea na wenzao wa kabila jingine. Kiingereza hufundishwa kama soomo kuanzia mwaka wa pili wa sekondari. Kwa mfano huu ni kweli lugha mama ni nzuri kutumika kujenga misingi ya 'kuelimika'na kufikiri endapo tu kuna vitabu vinavyokidhi. Lugha ya pili ni nyenzo ya kuboresha misingi iliyowekwa na lugha mama.

Katika makala za maprofes Omari na Brock-Utne kinachobishaniwa hapa si ukweli wa ubora wa matumizi ya lugha mama bali je katika hali halisi ya nchi za kiafrika ni muafaka?

Binafsi tunahitaji kujenga misingi ya kufikia huko la sivyo kwa kuwekeza katika elimu ya walimu wa lugha, kwetu sisi kiingerza na kiswahili, ili waweze kufundisha vizuri na kwa ubora unaotakiwa katika level mbalimbali. Pili ni kuandika nakuchapishwa kwa vitabu vitakavyowavutia watoto wetu wapende kusoma. Kwa sasa Kiingereza katika mashule ni kwa ajili ya elites na sio umma. Na kwa kuwa wengi wa viongozi wetu wanazo za kuwapeleka watoto wao kwenye ST.'s, Academys na nje, moyo wa kufikiria elimu kwa umma ni finyu.

Miaka iliyopita tulipewa msamaha wa madeni kwa kuwekeza kwenye elimu na afya. upande wa elimu pengine hatukuwa strategic kwa kukimbilia ujenzi wa madarasa 9 kuna kula huko) badala ya elimu ya ualimu. Nadhani hatujachelewa, kwa sasa madarasa yametosha tuwekeze katika elimu ya ualimu ili tuinue kiwango cha elimu yetu itolewayo kwa umma.
 
Hahahahahaaa, kwa kweli nasikia kufa mbavu..!! Namkumbuka ticha mmoja huko Songea, jamaa nahisi alipataga F ya English.

Siku ya introduction, alimalizia speech kwa kupiga "It iz my belief that, I will left with you comfortably".

Haitoshi, siku moja akitangaza matokeo ya mpira kati ya form six na five, akavunja watu mbavu tena "form six team has closed form five 2 goals". Yaani form six wamewafunga form five magoli mawili..!! Sasa hapa unategemea wanafunzi wasilishwe pumba badala ya nyanga za muhimu kweli....!!!...???

Ila mimi sishauri ki-english kitolewe, but walimu wapelekwe skuli ya english ili wawe gado kuwaelekeza wanafunzi. Pia nafikiri ki-english kipewe mkazo toka chini. Serikali isituletee usanii, waingie gharama kuwapeleka walimu kusoma lugha ili pasiwe na aibu mashuleni. Ila kwa upande mwingine huwa naona changamoto hata kwa wanafunzi wa St. Private, utakuta mzazi ana senti but hajakanyaga vidato. Mtoto akifika home inakuwa kero kwa mzazi manake anajua aibu ishakaribia. Akiambiwa good evening anajibu good morning. Hapo ni kazi kweli kweli. Pia hata mtaa anaokaa, watoto anaocheza nao, utakuta ndio wale wa St. Government au St. Kayumba (kama walivyoitwa), then sijui unategemea nini kama sio "lugha gongana".

Kwa kweli swala la kiingereza ni changamoto kali sana hasa ukizingatia umuhimu wake bado ni mkubwa sana hasa kwa ujio wa utandawazi.

Kama mtu anataka wanafunzi wafundishwe kiswahili, sawaaaaaaa, ila mjue kuwa watakuwa na digrii, but kazi = 0 = machinga/mateja/watu wenye frustration ya maisha. Hii ni kutokana na nililosema hapo juu "utandawazi".
 
Mimi nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusiana na maswala yafutayo:

- Kutolewa kwa fimbo mashuleni
- Kutolewa kwa mitihani ya darasa la nne
- Kutolewa kwa mitihani ya kidato cha pili

Nikianza na kutolewa kwa fimbo mashuleni. Ni kweli kuwa fimbo zilitukera sana wanafunzi wa kale, but ukweli ukabaki pale pale kuwa zilitufanya kuwaheshimu walimu na wakubwa zetu. Ilikuwa mwalimu akisema neno, hata kama ana umbo dogo (nusu ya mwanafunzi), but mwanafunzi atatii. Yaani walimu walikuwa na authority katika kurekebisha tabia za wanafunzi. But nini kinaendelea sasa hivi. Wanafunzi wanatukana walimu kwa namna wanavyotaka. Tunaona watoto wana adabu chafu huku mtaani mpaka aibu. Tunaona walimu wanakosa komfo kwa wanafunzi sababu ya power kuondolewa. Sasa hivi mwalimu hata akimpa adhabu mwanafunzi ya kudeki darasa, yaani sio mzazi tu wa huyo mwanafunzi, bali hadi mwenyekiti wa kijiji anachotoka huyo mwanafunzi watamvaa mwalimu wa watu. Na hawatataka kusikiliza A wala B toka kwa mwalimu. Tunakwenda wapi...?? Mimi nafikiri serikali ingetafuta suluhisho katika hili, na sio kukimbilia kuondoa fimbo na adhabu mbadala. Nahisi labda idadi ya fimbo ingewekewa masharti au pangetungwa adhabu mbadala (ingawa sidhani kama ipo).

- Kutolewa kwa mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili. Sijapata uhakika kama serikali ilifikiria hili swala kwa undani au kuchunguza kwa nini liliwekwa. Isije ikawa walikurupuka kama walivyotia aibu (mimi naita kufanya ushenzi) katika kutoa masomo ya biashara, kilimo na ufundi. Hii mitihani ninavyoelewa, hasa mtihani wa darasa la nne, unajua kutoka darasa la kwanza hadi la saba ni safari ndefu sana. Na kwa uhakika wa saikolojia ya masomo, mwanafunzi hata mtu mzima aliyekamilika, kukumbuka kitu alichokisoma 7 or 4 years back ni ngumu sana hasa panapokosekana mtihani wa kumchemsha hapo katikati. The same applies kwa sekondari. Sasa sijajua kwa nini serikali wametoa hiyo mitihani ingawa argument niliyoisikia ni kuwa eti ilikuwa inadiscourage watu kuendelea na shule pale wanapofeli darasa la nne au kidato cha pili..!!!..?? Whaaaaaaaaaaatttttttttt..!!!...?? Nonsense...!!! So are we producing bora wanafunzi au wanafunzi bora..!! Unajua usiseme nina wananchi milioni 20 out of 30/40 million wanajua kusoma na kuandika while they know nothing..!! Hii kwa upande mwingine ni kuwaongezea walimu mzigo wa kufundisha..!!

Naomba maoni ili nifunguliwe kimawazo manake isije ikawa nina uelewa wa tofauti juu ya mada hizi..!!
 
Kama mtu anataka wanafunzi wafundishwe kiswahili, sawaaaaaaa, ila mjue kuwa watakuwa na digrii, but kazi = 0 = machinga/mateja/watu wenye frustration ya maisha. Hii ni kutokana na nililosema hapo juu "utandawazi".

Mimi naomba kutofautiana na wewe hapo,
Kiswahili ni lugha rahisi kufikishia elimu hapa tanzania.
elimu itawafikia watu kwa urahizi zaidi na wataelimika vizuri katika fani mbalimbali za kujenga nchi.
wataalamu wa ngazi za juu ambao hatuna waalimu wa taaluma yao watasoma nje au hapa kwa lugha ambayo taaluma itatolewa (mfn kiingereza)
mimi hapo assumption yangu ni kuwa kiingereza kitafundishwa kwa ufasaha kama lugha ya kwanza ya kigeni.
Hata tunaweza kuomba walimu toka nje ili wanafunzi wakijue kiingereza kama lugha ya kigeni.
Si kama hakuna mwenye ufasaha wa kiingereza wala kiswahili. vyote ovyo tu.
Sababu kubwa ambayo tunaikwepa ya kushuka elimu ni lugha ya kufundishia, ambayo si fasaha, na haieleweki, kwa hiyo ukiongezea na mtaala wa kuungaunga basi mwanafunzi akimaliza form six bado kichwa cheupe kama zamani, zaidi ya maswali machache alioshika kwa ajili ya mtihani.
 
Back
Top Bottom