HakiElimu vs Govt: The saga

KadaMpinzani

JF-Expert Member
Jan 31, 2007
3,715
86
Mbunge: HakiELimu itaidondosha serikali
na Tamali Vullu, Dodoma

WABUNGE wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameitaka serikali kuichukulia hatua taasisi isiyo ya kiserikali ya HakiElimu kwa maelezo kuwa matangazo yake yamekuwa yakibeza juhudi za kuendeleza elimu nchini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti bungeni mjini Dodoma jana, mmoja wao alifikia hatua ya kuionya serikali kuwa makini na taasisi hiyo ambayo alisema isipoichukulia kwa umakini inaweza ikaing’oa madarakani kama ilivyotokea nchini Zambia.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi jana, Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (CCM) alisema, matangazo yanayotolewa na HakiElimu yamekuwa yakibeza juhudi za serikali.

Ndugai alionyesha kushangazwa na lengo hasa la HakiElimu kiasi cha kufikia kuhoji taasisi hiyo ipo upande gani na akasema iwapo inafanya kazi zake kisiasa, ni vema ikaandikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Aliishauri serikali kuwa macho na taasisi hiyo na kuitaka kutoendelea kukaa kimya, kwani inaweza kujikuta pabaya baada ya muda.

Akitoa mfano, Ndugai alisema kuwa hali inayofanana na hii, iliwahi kutokea huko Zambia miaka kadhaa iliyopita na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani kung’olewa.

Mbunge mwingine Janet Masaburi (Viti Maalumu-CCM) naye aliunga mkono hoja hiyo ya Ndugai kwa kusema kuwa, matangazo yanayotolewa na taasisi hiyo iliyojipatia umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni, yanajenga chuki miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yao.

Masaburi alisema anaamini si vyema kwa serikali kuchezewa, wakati ikijulikana wazi kuwa imekuwa ikifanya juhudi kubwa kukuza kiwango cha elimu nchini.

Hoja hizo za wabunge zimekuja miezi kadhaa sasa tangu serikali ipige marufuku matangazo ya asasi hiyo isiyo ya kiserikali kabla ya kuifungulia kuendelea na shughuli zake.

Aidha, uamuzi kama huo pia umewahi kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo pia, ilipiga marufuku kurushwa katika redio na televisheni kwa matangazo ya taasisi hiyo yaliyokuwa yakihimiza kuhusu haja ya kutoa elimu bora.

Wakati fulani serikali iliwahi kuifungia taasisi hiyo kutoa matangazo yake kwa maelezo kuwa yanakejeli juhudi za serikali katika kukuza sekta ya elimu nchini.

Awali, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo jana asubuhi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margaret Sitta, alisema kuwa, serikali imepanga kuajiri walimu 14,490 na watumishi wasio walimu 397, sambamba na kuidhinisha maombi ya ajira za walimu 6,000 raia wa kigeni kwa ajili ya shule siziso za serikali.

Alisema wizara hiyo pia itathibitisha kazini watumishi 1,000 na kupandisha vyeo watumishi 10,486 ambao wamekaa katika madaraja waliyonayo kwa muda mrefu.

Sitta alisema wizara hiyo inaandaa mpango ambao utaratibu mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wake 2,110.

“Tutatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wakuu wa vyuo shule/vyuo, wakaguzi wa shule na waratibu wa elimu ya sekondari wa kanda za Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Ziwa na Magharibi kuhusu haki na masilahi ya watumishi, sheria, kanuni na taratibu za utumishi,” alisema Waziri Sitta.

Waziri Sitta alisema katika kufuta ujinga na kujiendeleza katika mfumo usio rasmi, wizara itaendelea kutoa mafunzo kwa vijana nje ya shule, wafanyakazi na watu wazima ambao hawakupata nafasi ya kujiendeleza.

Alisema katika mwaka wa fedha 2007/2008, wizara hiyo itatoa mafunzo ya stashahada ya juu kwa walengwa 244, stashahada ya kawaida kwa watumishi 293 na cheti cha sheria kwa watu 225.

Alisema katika kutoa elimu bora na inayoendana na wakazi, wizara hiyo itaimarisha mitaala na mihtasari ya elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu na elimu maalumu.

Katika kufanikisha hilo, Waziri Sitta, alisema watarekebisha mitaala na kuandika mihtasari ya ualimu ngazi ya cheti, ili iendane na mabadiliko ya mitaala.

Pia alisema watabuni na kuandaa mtaala wa mafunzo ya ualimu unaotumia teknojia ya kisasa (e-learning), ili kuwafikia wadau wengi.

Alisema pia kuwa serikali inatarajia kujenga nyumba za walimu 1,500 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2007/2008, na kiasi cha sh bilioni 13.5 zimetengwa kwa ajili hiyo.

Alisema nyumba hizo zitajengwa katika shule za sekondari za serikali, hususan kwenye maeneo yenye mazingira magumu.

Alisema, katika kipindi hicho, serikali itachangia ujenzi wa hosteli 10 kwa ajili ya wasichana katika maeneo ya wafugaji na yaliyo nyuma kielimu pamoja na kuchangia ujenzi wa madarasa 800 na vyoo 76 katika shule za sekondari.

Waziri alisema pia katika kipindi hicho, wizara hiyo itagharamia wanafunzi 42,710 wa kidato cha kwanza hadi cha nne na wanafunzi 3,352 wa kidato cha tano na sita wanaotoka kwenye familia zenye kipato duni.

“Mafanikio makubwa ya ujenzi wa shule za sekondari zinazojengwa kutokana na mwitiko mkubwa wa wananchi zimesababisha mahitaji makubwa ya walimu, vifaa vya kufundishia, na kujifunzia, nyumba za walimu, maabara, madarasa na majengo ya maabara.

“Baadhi ya wanafunzi kuishi mbali na shule kunaweza kusababisha ongezeko la mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kupata mimba, hivyo kusababisha mahitaji makubwa ya hosteli,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Sitta, alisema wizara itaibua mjadala wa kitaifa kuhusu tatizo la mimba kwa wanafunzi, kukazia sheria ya kuwaadhibu wanaowapa mamba na uwezekano wa kuwarejesha shuleni baada ya kujifungua.

Alisema wizara hiyo pia itapitia upya andiko la Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kwa lengo la kuzingatia upanuzi wa shule za kidato cha tano na sita na vyuo vya ualimu, ili kukidhi mahitaji ya sasa.

Pia alisema watatoa mafunzo kazini hasa kwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi, ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa masomo hayo.

Waziri Sitta, alisema serikali itaendelea kutoa vibali vya kuanzisha shule za sekondari za seriakli 5,000 zinazoajengwa kwa nguvu za wananchi na kusajili shule zisizo za serikali pamoja na kukusanya takwimu za walimu walio kazini kwa ajili ya kuwasajili kutoka halmshauri 47.

Pia, alisema wataratibu na kufuatilia ukarabati wa miundombinu katika shule zenye wanafunzi wenye ulemavu; Moshi Ufundi, Moshi Sekondari, Lugalo, Mpwapwa, Korogwe, Iringa na Kazima.
 
Ndugai alionyesha kushangazwa na lengo hasa la HakiElimu kiasi cha kufikia kuhoji taasisi hiyo ipo upande gani na akasema iwapo inafanya kazi zake kisiasa, ni vema ikaandikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Philosophy ya George Bush hii: Either you are with us or you a terrorist.

CCM ukipingana nao tu basi wanakuuliza uko upande gani, kama siyo upande wao basi upigwe marufuku. Kila linalozungumzwa dhidi ya serikali kwao wao wanaliona ni siasa. Huku ndiko kulewa madaraka ambako hupelekea udikteta.

Yaani hawa wabunge wanadai kuwa kujenga sekondari isyokuwa na maabara ypyote huku ikiwa na mwalimu mmoja na choo kimoja kisichukuwa na paa wa mlango ni juhudi kubwa sana zinazofanywa na serikali kuboresha elimu? Give me a break!! Je, kuna mbunge hata mmja aliyepeleka mtoto wake kwenye hizo sekondari zinazojengwa na serikali?
 
Kuna haja ya wananchi kukaa nje ya bunge na mwisho wa siku kucharaza viboko wabunge wanaotumia vibaya kodi zetu kwa kuongea na kutetea upuuzi.

kadri siku zinavyokwenda serekali ya ari mpya inajioonsha isvyokuwa na uwezo wa kukabili changamoto. Kila anaea kosoa ni mpinzani, ni mwanasiasa. Kwa mwendo huu, upo uwezekano tukasikia wabunge wa CCM wanafukuzwa kwenye chama kwa kukosoa mikakati mibovu ya serekali ya CCM, itatamkwa kuwa wamefanya kazi ya upinzani.

Upuuzi unaoendelea kuzungumzwa na baadhi ya wabunge si jambo la kuvumilika. Zipo jitihada za wazi kabisa za kuturudisha katika ujima.

Matangazo ya Hakielimu ni mazuri sana na yanagusa,hasa haya ya hivi karibuni ambayo yanajaribu kutuasa kungalia hatari ya ufa kati ya wenye nacho na waliokapa. Kama alivyofanya yule waziri hodari na mahiri ambae aliepewa ujumbe kwa sahiri badala ya kuangalia maudhui ya ujumbe ule yeye akajibu shairi na jana wabunge hao wawili wa CCM wamefanya kama kiongozi wao alivyofanya!

Bunge lianaendelea kupoteza maana mapema sana. Tunapaswa kuwa na mikakati ya kuhakikisha bunge lijalo linakuwa na wawakilishi makini na pia kuhakikisha tunapunguza pengo kati ya wabunge wa upinzani na wale wa chama kigumu.
 
Kuna haja ya wananchi kukaa nje ya bunge na mwisho wa siku kucharaza viboko wabunge wanaotumia vibaya kodi zetu kwa kuongea na kutetea upuuzi.

Nimefurahishwa na hili.....mimi naona bakora zinaweza kusaidia japo kidogo.

Diwani acharazwa bakora hadharani

2007-07-08 10:32:46
Na Mwandishi wa PST, Songea

Diwani mmoja katika Manispaa ya Songea, ameonja joto ya jiwe kwa kucharazwa bakora hadharani na mwananchi mmoja mwenye hasira aliyemnasa akiwa na binti yake gesti.

Tukio hilo la aina yake, lilitokea juzi jioni katika mtaa maarufu wa mjini hapa wa Delux, wakati Diwani huyo alipokutwa na mtoto wa mwananchi huyo akiwa amempakia ndani ya gari lake (namba za gari tunazo).

PST ilimshuhudia Diwani huyo akishuka kwenye gari hilo na kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni huku binti huyo ambaye ni mwanafunzi akimsubiri garini.

Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema kuwa muda mfupi baada ya Diwani huyo kuingia katika nyumba hiyo, baba mzazi wa binti huyo alitokea eneo hilo na kumkuta binti yake akiwa ndani ya gari, nje ya gesti.

Ilidaiwa kuwa baada ya binti huyo kuulizwa na baba yake alikuwa anasubiri nini kwenye gari hilo, alishindwa kujibu chochote.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia baba huyo akimshusha binti huyo kwenye gari na kuanza kumcharaza viboko huku akimsindikiza kwenda nyumbani.

Baada ya kipigo hicho kwa binti yake ambaye alitimka, baba huyo alimrejea Diwani huyo ambaye alikuwa anatokea kwenye gesti hiyo na kumvamia kwa kumcharaza bakora mwili mzima.

Diwani huyo alijaribu kujitetea kwa kumtaka mzazi huyo asimpige lakini aliendelea kumcharaza huku akimwambia kuwa amemuonya mara nyingi kuhusu binti yake huyo lakini hataki kusikia.

``Nimekuonya mara ngapi kuhusu binti yangu unajua kuwa ni mwanafunzi unataka kumharibia masomo...nimekutumia mara ngapi wenzako wakuonye kuhusu tabia yako,`` alisema mzazi huyo huku akiendelea kumcharaza bakora Diwani huyo.

Taarifa kutoka kwa marafiki wa karibu wa Diwani huyo zimeeleza kuwa hiyo ni tabia yake ya kuwafuata watoto wa shule na wake za watu na amekwisha onywa mara nyingi kuhusiana na tabia hiyo.

SOURCE: Nipashe
 
Jana tu nilisikia Mbunge mmoja wa CCM akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu na Ufundi akitumia Tangazo la HAkielimu kujenga hoja ya kutetea elimu kwa watoto walemavu na kutoa mfano wa Kapeto mtoto mlemavu ambaye babake hakutaka kumwandikisha shule kwa sababu ya ulemavu; leo Mbunge nahabarishwa Mbunge mwingine wa CCM akitaka Hakielimu idhibitiwe!

Yanayowapendeza kutoka Hakieleimu mnayafurahia, wanapoeleza msiyowapenda mnawachukia. Pendendeni vyote.

TAFAKARI!
 
Jamani Wananachi Wenzangu Jamvini Nadhani Hii Ni Adhabu Ambayo Tunaipata Kwa Makodsa Yetu Ya Kuchagua Mtu Kwa Sura Na Pesa Badala Ya Sera Na Uwajibikaji.
Hawa Wabuge Waliopropozi Hii Ishu Utashangaa Kuna Watun Watawapigia Kura Next Election.
Hakielimu Ni Shirika Binafsi Ambalo Wapenda Haki Wote Duniani Wangelifagilia Ila Kwa Kuwa Serikali Yetu Ni Ya Watu Wasiojali Kuwajibika Na Wasiopenda Kukosolewa.
Mchango Huu Wa Wabunge Hawa Yafaa Uingizwe Kny Kitabu Cha Guinness Kama Mchango Mbaya Kuliko Wowote Liowahi Kutolewa Na Mbunge Duniani
 
Kuna mbunge mmoja wa CCM leo kanifurahisha. Huyu ni bwana James Wanyancha wa Serengeti. Huyu amekuwa na ujasiri wa kusema kuwa sasa hivi elimu yetu imevurugwa kufikia kiwango cha kuwa na watu wengi wanaodai kuwa na PHD lakini ukiwauliza wamechukulia wapi wanakuwa hawana majibu. Akielezea visingizio vya serikali kushindwa mambo mengi kutokana na kukosa fedha, alisema bei ya shangingi moja inatosha kujaza komputa kwenye shule nyingi. Huwezi amini wakubwa walivyokuwa wamemkodolea macho. Sitashangaa nikija kusikia kuwa baadaye aliitwa.
 
Zaidi ya miaka 18, akili timamu na Kada mzuri wa Chama anachotaka kugombea.

nashukuru kwa kunielewesha. Kwa sifa hizi tusishangae wabunge wengine wakiwa wabunge bubu na wengine wakitoa comment kama hizi za kuifanya Hakielimu kuwa chama cha siasa.
 
Mimi nafikiri hilo la "akili timamu" linajadilika maana wakati mwingine hawa waheshimiwa wanapozungumza inabidi uhoji kama "wanazo au zimewaruka".
 
Mimi nafikiri hilo la "akili timamu" linajadilika maana wakati mwingine hawa waheshimiwa wanapozungumza inabidi uhoji kama "wanazo au zimewaruka".

Sifa ya akili timamu inaangaliwa psychiatrically badala ya kuingalia intellectually. Ni vigumu kupima intellectual akili timamu kisheria; kwa hiyo kama mbunge hana akili timamu intellectually, basi lawama zinawaendea wananchi waliomchagua kwa vile ndio waliomwona kuwa anafaa kuwawakilisha bungeni. Tatizo ni pale anapokuwa amateuliwa tu, wala hakuchaguliwa na wananchi!
 
big up kadampinzani wabunge wengine hawajui wako wapi wanakwenda wapi na pia ukae ukijua huyu mbunge aliyesema Ndugai anajikomba komba kwa serikali ili apatw ulaji ndio mana ansema hivyo coz siunaona anakaaaga kwenye kiti cha spika wakati hayupo.
 
Kichuguu, unapokuwa na watu wanne ambao wote zimewaruka lakini wanapopita mtaani wako kimya huku wamevalia vizuri basi wakati mwingine ni vigumu kujua kama ni timamu au la. Kwa watu kama hawa ukiwapeleka kwa psychiatrist wanaweza kupass with flying colours. Ni kama kile kisa cha kule Mirembe ambapo daktari alikuwa anawapima wagonjwa wake wa akili kuona kama wamepata nafuu. Akawacholewa mlango ukutani na kuwataka watoke nje. Wale jamaa kwa vile zilikuwa zimepungua kichwani wakaanza kugombania kufungua kitasa cha kuchora huku wakisukumana. Mmoja wao kama mnavyojua alikuwa ametulia tuli tu akiwaangalia wenzake. Ndipo yule mganga akamwuliza "vipi wewe hutaki kuwafuata wenzako?" Yule mgonjwa akitabasamu akamwambia "miye nawashangaa watatoka vipi wakati funguo ninazo mimi?". Moral of the story, wakati mwingine ni hadi watu waanze kuzungumza ndio tunawajua kama zimo au la. Na hili ndilo linaloendelea hapa Bungeni, wabunge wengi wanaonekana wanazo kweli hadi pale wanapopewa vipasa sauti.

Asante
 
.......interesting
 
Nakuunga mkono na mguu...
 
vizuri, u brought the point out clear !
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom