HakiElimu vs Govt: The saga

na Tamali Vullu, Dodoma


WABUNGE wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameitaka serikali kuichukulia hatua taasisi isiyo ya kiserikali ya HakiElimu kwa maelezo kuwa matangazo yake yamekuwa yakibeza juhudi za kuendeleza elimu nchini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti bungeni mjini Dodoma jana, mmoja wao alifikia hatua ya kuionya serikali kuwa makini na taasisi hiyo ambayo alisema isipoichukulia kwa umakini inaweza ikaing’oa madarakani kama ilivyotokea nchini Zambia.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi jana, Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (CCM) alisema, matangazo yanayotolewa na HakiElimu yamekuwa yakibeza juhudi za serikali.

Ndugai alionyesha kushangazwa na lengo hasa la HakiElimu kiasi cha kufikia kuhoji taasisi hiyo ipo upande gani na akasema iwapo inafanya kazi zake kisiasa, ni vema ikaandikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Aliishauri serikali kuwa macho na taasisi hiyo na kuitaka kutoendelea kukaa kimya, kwani inaweza kujikuta pabaya baada ya muda.

Akitoa mfano, Ndugai alisema kuwa hali inayofanana na hii, iliwahi kutokea huko Zambia miaka kadhaa iliyopita na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani kung’olewa.

Mbunge mwingine Janet Masaburi (Viti Maalumu-CCM) naye aliunga mkono hoja hiyo ya Ndugai kwa kusema kuwa, matangazo yanayotolewa na taasisi hiyo iliyojipatia umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni, yanajenga chuki miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yao.

Masaburi alisema anaamini si vyema kwa serikali kuchezewa, wakati ikijulikana wazi kuwa imekuwa ikifanya juhudi kubwa kukuza kiwango cha elimu nchini.

Hoja hizo za wabunge zimekuja miezi kadhaa sasa tangu serikali ipige marufuku matangazo ya asasi hiyo isiyo ya kiserikali kabla ya kuifungulia kuendelea na shughuli zake.

Aidha, uamuzi kama huo pia umewahi kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo pia, ilipiga marufuku kurushwa katika redio na televisheni kwa matangazo ya taasisi hiyo yaliyokuwa yakihimiza kuhusu haja ya kutoa elimu bora.

Wakati fulani serikali iliwahi kuifungia taasisi hiyo kutoa matangazo yake kwa maelezo kuwa yanakejeli juhudi za serikali katika kukuza sekta ya elimu nchini.

Awali, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo jana asubuhi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margaret Sitta, alisema kuwa, serikali imepanga kuajiri walimu 14,490 na watumishi wasio walimu 397, sambamba na kuidhinisha maombi ya ajira za walimu 6,000 raia wa kigeni kwa ajili ya shule siziso za serikali.

Alisema wizara hiyo pia itathibitisha kazini watumishi 1,000 na kupandisha vyeo watumishi 10,486 ambao wamekaa katika madaraja waliyonayo kwa muda mrefu.

Sitta alisema wizara hiyo inaandaa mpango ambao utaratibu mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wake 2,110.

“Tutatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wakuu wa vyuo shule/vyuo, wakaguzi wa shule na waratibu wa elimu ya sekondari wa kanda za Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Ziwa na Magharibi kuhusu haki na masilahi ya watumishi, sheria, kanuni na taratibu za utumishi,” alisema Waziri Sitta.

Waziri Sitta alisema katika kufuta ujinga na kujiendeleza katika mfumo usio rasmi, wizara itaendelea kutoa mafunzo kwa vijana nje ya shule, wafanyakazi na watu wazima ambao hawakupata nafasi ya kujiendeleza.

Alisema katika mwaka wa fedha 2007/2008, wizara hiyo itatoa mafunzo ya stashahada ya juu kwa walengwa 244, stashahada ya kawaida kwa watumishi 293 na cheti cha sheria kwa watu 225.

Alisema katika kutoa elimu bora na inayoendana na wakazi, wizara hiyo itaimarisha mitaala na mihtasari ya elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu na elimu maalumu.

Katika kufanikisha hilo, Waziri Sitta, alisema watarekebisha mitaala na kuandika mihtasari ya ualimu ngazi ya cheti, ili iendane na mabadiliko ya mitaala.

Pia alisema watabuni na kuandaa mtaala wa mafunzo ya ualimu unaotumia teknojia ya kisasa (e-learning), ili kuwafikia wadau wengi.

Alisema pia kuwa serikali inatarajia kujenga nyumba za walimu 1,500 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2007/2008, na kiasi cha sh bilioni 13.5 zimetengwa kwa ajili hiyo.

Alisema nyumba hizo zitajengwa katika shule za sekondari za serikali, hususan kwenye maeneo yenye mazingira magumu.

Alisema, katika kipindi hicho, serikali itachangia ujenzi wa hosteli 10 kwa ajili ya wasichana katika maeneo ya wafugaji na yaliyo nyuma kielimu pamoja na kuchangia ujenzi wa madarasa 800 na vyoo 76 katika shule za sekondari.

Waziri alisema pia katika kipindi hicho, wizara hiyo itagharamia wanafunzi 42,710 wa kidato cha kwanza hadi cha nne na wanafunzi 3,352 wa kidato cha tano na sita wanaotoka kwenye familia zenye kipato duni.

“Mafanikio makubwa ya ujenzi wa shule za sekondari zinazojengwa kutokana na mwitiko mkubwa wa wananchi zimesababisha mahitaji makubwa ya walimu, vifaa vya kufundishia, na kujifunzia, nyumba za walimu, maabara, madarasa na majengo ya maabara.

“Baadhi ya wanafunzi kuishi mbali na shule kunaweza kusababisha ongezeko la mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kupata mimba, hivyo kusababisha mahitaji makubwa ya hosteli,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Sitta, alisema wizara itaibua mjadala wa kitaifa kuhusu tatizo la mimba kwa wanafunzi, kukazia sheria ya kuwaadhibu wanaowapa mamba na uwezekano wa kuwarejesha shuleni baada ya kujifungua.

Alisema wizara hiyo pia itapitia upya andiko la Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kwa lengo la kuzingatia upanuzi wa shule za kidato cha tano na sita na vyuo vya ualimu, ili kukidhi mahitaji ya sasa.

Pia alisema watatoa mafunzo kazini hasa kwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi, ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa masomo hayo.

Waziri Sitta, alisema serikali itaendelea kutoa vibali vya kuanzisha shule za sekondari za seriakli 5,000 zinazoajengwa kwa nguvu za wananchi na kusajili shule zisizo za serikali pamoja na kukusanya takwimu za walimu walio kazini kwa ajili ya kuwasajili kutoka halmshauri 47.

Pia, alisema wataratibu na kufuatilia ukarabati wa miundombinu katika shule zenye wanafunzi wenye ulemavu; Moshi Ufundi, Moshi Sekondari, Lugalo, Mpwapwa, Korogwe, Iringa na Kazima.
 
Wabunge wanajali madaraka zaidi kuliko elimu, kama kweeli wanajali elimu waseme je ni kitu gani Haki Elimu wanadanganya!!. Analysis yao iko wazi na nzuri je ya serikali iko wapi??!!. Kwa upande fulani Hawa wazee wa bunge na watu wengine ni lazima waamini wakati wa siri siri umeisha na watanzania wanajua vitu sana hawawezi kudanganya na maneno. Watanzania wa mika ya tisini si wa sasa!!
 
HAYA SASA HAKIELIMU NAONA SASA HIVI WAMERUDI KWA KASI MPYA, EBU SOMA HAPA CHINI:

HakiElimu yaifumua bajeti ya elimu nchini
na Ratifa Baranyikwa na Shabani Matutu


SIKU moja baada ya wabunge wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuitaka serikali ichukue hatua kali dhidi ya HakiElimu, taasisi hiyo imeibuka na kusema fedha nyingi zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini hazitumiki ipasavyo.

Hayo yamo katika uchambuzi uliofanywa na taasisi hiyo kwa kuangalia mwenendo mzima wa bajeti na matumizi yaliyotengwa katika mwaka wa fedha 2006/07 uliomalizika hivi karibuni.

Ikitumia takwimu rasmi za serikali, HakiElimu imechapisha vijarida maalumu vinavyoonyesha mapungufu hayo katika sekta ya elimu ambavyo vilizunduliwa jijini Dar es Salaam, juzi.

Vijarida hivyo vinaainisha mchakato mzima wa bajeti ya elimu, hasa kwa upande wa ruzuku maalumu kwa wanafunzi wa elimu ya msingi.

Kwa mujibu wa vijarida hivyo, wakati ambapo bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka huo ilikuwa sh bilioni 178, matumizi halisi yalikuwa sh bilioni 103 sawa na asilimia 58 ya fedha yote iliyoidhinishwa.

Kijarida cha uchanganuzi wa matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kinaeleza kuwa, fedha nyingi zilizoidhinishwa na Bunge, zinazofikia sh bilioni 75, hazikutumika na kwamba mtazamo wa karibu unaonyesha kuwa, sh bil. 14.6 ziliidhinishwa kwa ajili ya ruzuku maalumu kwa kila mwanafunzi, lakini hakuna fedha zilizotengwa au kutumika.

Taarifa iliyotolewa na HakiElimu na kusainiwa na Mkurugenzi wa shirika hilo, Rakesh Rajan, inaeleza pia kwamba, mbali ya hayo, vipaumbele vilivyoainishwa wakati wa bajeti ya mwaka jana bungeni, havikuzingatiwa.

Akitoa mfano, Rajan alisema kuwa, ruzuku maalumu (capitation grant) kwa wanafunzi wa elimu ya msingi, ilipangwa iwe sh 12,500, lakini kiasi kamili hakifiki mashuleni kwa wakati.

Taarifa hiyo inazidi kueleza kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa shule zimekuwa zikipokea kiwango cha chini ya kile kilichopitishwa katika bajeti na kwamba kwa mwaka 2005/06 fedha nyingi hazikutumika ipasavyo, kinyume na bajeti iliyopitishwa na Bunge.

Kwa mujibu wa kijarida hicho, sh bilioni 12.4 ziliidhinishwa kwa ajili ya shule, lakini hakuna fedha zilizotengwa au kutumika.

Hata hivyo, imebainika kuwa, mishahara na gharama za shule viliendelea kuwa kipaumbele, lakini masurufu, mkutano, ukarimu na safari ambavyo vilipewa asilimia nane ya matumizi ya bajeti, vilichukua sehemu kubwa zaidi ya bajeti.

Kwa mujibu wa uchambuzi wa HakiElimu, maeneo mengine yaliyovuka matumizi ni pamoja na ofisi, huduma na ukarabati vitu ambavyo vinaelezwa kuwa si vipaumbele kwa kuboresha elimu kwenye ngazi ya jamii.

Aidha, kwa upande wa matumizi ya bajeti ya chakula, yalizidi kwa zaidi ya sh bilioni moja, kitu ambacho kimeelezwa kuwa ni cha kushangaza kwa kuzingatia upungufu wa nusu ya kiasi kilichoidhinishwa kilitumika kwenye chakula cha shule.

Kutokana na hali hiyo, HakiElimu imetoa changamoto kwa Wizara ya Elimu kuhakikisha inaandaa bajeti inayotoa vipaumbele bora kwa mambo yatakayoboresha ubora wa elimu kwenye kiwango cha shule, pia kuhakikisha matumizi yake halisi yanarandana na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge.

Taasisi hiyo inashauri kuwa, masuala kama vile ruzuku maalumu kwa kila mwanafunzi, itolewe kama ilivyopangwa kwani ni muhimu katika kuboresha mazingira ya kujifunzia shuleni.

Taasisi hiyo imeitaka pia wizara kuangalia namna ya kupunguza matumizi ambayo si muhimu kwa ngazi za shule, kama vile masurufu kwa wafanyakazi wa wizara.

Hata hivyo, taasisi hiyo imeipongeza serikali kwa kuongeza fedha katika bajeti ya elimu kwa mwaka huu, lakini ikasema kuwa, kuongeza bajeti peke yake haitoshi.

Imeishauri Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuzingatia vipaumbele vya MMEM na MMES, hasa suala la ruzuku maalum kwa kila mwanafunzi kwa kuwa ndiyo fedha muhimu inayotumika kununua vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

Wakati huo huo, watu kadhaa waliohojiwa na gazeti hili, wamepingana na msimamo wa wabunge wawili wa CCM walioitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya matangazo yanayotolewa na HakiElimu.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti jana jijini Dar es Salaam, wananchi hao wameitaka serikali isiwasikilize wabunge hao na badala yake iache HakiElimu itimize wajibu wake wa kuikumbusha pale palipo na mabonde ili wapasawazishwe.

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Anthony, Luis Ibrahimu, alisema kwamba si kweli kwamba matangazo hayo yanaweza yakazuia juhudi za maendeleo.

“Sikubaliani na kauli hiyo, ila mimi kama mwalimu, ninachoamini ni kwamba matangazo ya HakiElimu yanasaidia kuionyesha serikali yetu mahali ambako panakuwa na upungufu na wao kuparekebisha,” alisema Ibrahimu.

Aliendelea kusema kuwa, HakiElimu walitakiwa kupewa ushirikiano kutokana na michango yao katika kuhakikisha kuwa sehemu ambazo zimesahaulika zinakumbukwa.

Naye Kassimu Idrisa alisema kwamba si kweli kwamba matangazo haya yanaleta chuki kati ya serikali na wananchi wake, ila yamekuwa na lengo la kuionyesha serikali kasoro zilizopo katika sekta ya elimu.

“Kama kweli serikali ingekuwa imefanya juhudi kubwa za kuendeleza elimu, sidhani kama matangazo haya yangekuwa yanawashtua kiasi hiki, isitoshe mara baada ya kuingia madarakani serikali ya awamu ya nne iliomba kukosolewa pale inapokosea,” alisema Idrisa.

Aliongeza kuwa, anaamini serikali ya awamu ya nne haitachukua uamuzi kama huo kwa kuwa inaamini mchango wa asasi hiyo kama changamoto kwao, isipokuwa wanaoitaka ifungiwe ndiyo wasiotakia mema maendeleo ya elimu.
 
mmh nnahisi harufu ya kubanwa pumzi ya moja kwa moja hakielimu hauko mbali.

maana sasa inataka kuzidi kuikamata serikali pabaya.

kwa ufupi ni vizuri kuionesha serikali kuwa usoni mwake mna masinzi na iko mbele ya halaiki, kisha nio juu yao kujipangusa au kudharau
 
Sirikali,
Haitaki kushauriwa- na kuambiwa ukweli- hata kama mawazo hayo yataboresha na kuleta mabadiliko!
Bravo Haki Elimu
 
Wabunge wamelala, pesa hazifiki kwenye majimbo yao hata hawajui, wengi wao wanishi Dar na kuzunguka kwenye kamati.

Afadhali HakiElimu, hivi kweli tunahitaji bunge Tanzania?
 
Nimeayaangalia matangzo ya haki elimu kwenye mtandao "ten" na kusema ukweli yanaibua hisia ! kweli serikali ina kazi na hawa watu , mimi nilikuwa sijui haswa haki elimu ni nini , lakini thanks to mtandao .....kwa wale waliona lile tangazo la mtoto anaondoka nyumbani ajanywa chai anasubiri basi kwa masaaa linatia uchungu sana !
 
Hawa jamaa mimi nawafagilia sana, lakini sina uhakika sana na content zao kama ni za uhakika au wanazusha tu. Otherwise nawapa BIG UP maana wanai-challenge serikali
 
Sasa hivi wataombwa waombe serikali Msamaha maanake ndio imekuwa hoja kubwa ya chama!
 
Nawashukuru sana Haki Elimu kwa uchambuzi wao, na kwa kuuelimisha umma kuhusu ukweli wa matumizi ya fedha zao.

Wabunge wanaoogopa ukweli wana lao. Mtu atendaye haki haogopi ukweli. Wezi na waongo hutegemea sana giza ili kuficha mambo. Wanaogopa ukweli ukifichuka. Wanatuabisha sana wabunge wanaotaka Haki Elimu iadhibiwe. Kuna kosa kusema ukweli kuhusu udanganyifu?

Niliona ripoti za tafiti zilizofanywa na NGOs kwenye magazeti yetu wiki chache zilizopita. Tafiti hizo zinadai kugundua kwamba 70% ya fedha zinazopelekwa mikoani kwa ajili ya Elimu huliwa na viongozi. Kama ni kweli, basi kwa vile mwaka jana tulitumia chini ya 10% ya bajeti yote kwa ajili ya Elimu, na zaidi ya nusu ya hizo fedha ziliibiwa na viongozi, ina maana fedha zilizotumika kweli kwa ajili ya Elimu ni kama 3% tu ya bajeti yote!

Usishangae basi kuona shule hazina hata vyoo. Atasomaje mtoto ambaye amebanwa na hana pa kwenda?
 
Augustine Moshi.
Vyoo kweli hakuna hukumbuki serikali iliomba msaada wa vyoo na ikajengewa vyoo na serikali ya Japan.Aibu tupu,Wakati akina Bilali wanasunda mabilioni na huko Wizaraya elimu ndo hayo hayo kwani ndo imekuwa fashion ya utawala wa CCM kila mtu kula pake bila kubughudhiwa.
 
Kazi ipo. Matabaka na tofauti kati yao zinaongezeka. Sasa nchi itakuwa uwanja mzuri wa mazoezi (field work) kwa wanafunzi wa fani zinazohusiana na class struggles na hatima yake. Siku hizi naona influx ya wanafunzi wengi kutoka vyuo vikuu vya ughaibuni wakija hapa kujifunza mambo hayo vijijini na kwenye slum areas za mijini. Tutamulikwa na hizo flash za kamera zao hadi tuchakae!
 
Jamani mimi nadhani nitakuwa tofauti kidogo kuhusu hawa jamaa wa HAKI ELIMU. Kwanza napenda kuwapongeza sana kwa Ubunifu wao maana katika Civil Society Organization ambazo zimefanikiwa nafikiri inaongoza, ila sasa tatizo langu ni moja hata kama wana-analyze matatatizo ya ELIMU nchini lakini wanachokosea WANGEJARIBU KUTOA BASI HATA PROPOSED SOLUTION kwa Serikali na Wizara Husika sasa nafikiri haya ndio waliyotakiwa wabunge wetu wale wawili wayaseme na sio Kufutwa. Kila la Kheri Haki Elimu ila mjaribu Kupendekeza MAWAZO JENZI kwa serikali na sio kulaumu tuu.
 
Sawa! Lakini Boss Wa Haki elimu bado Ana nishangaza!! hana hata Mtoto Mmoja anaye soma Shule ya serikali!!-Haoni Badala Yake ange wakosoa moja kwa moja wazazi!! Mfano wazazi walevi!!wanachelewa kurudi!! Mfumo Dume na Elimu!!- Haki Elimu
Ni nzuri!! Lakini wasifikiri hapo walipo ni zaidi ya wengine!!

Wanapaswa waende zaidi ya hapo!! la sivyo result itakua sio hiyo wanayo itaka....!!
 
Gigo ananichekesha pale anaposema mkuu wa Haki Elimu hana mtoto anayesoma shule ya serikali. Kuna ubaya gani hapo? Wenye uwezo wa kusomesha shule binafsi wafanye hivyo, ili waache nafasi kwa ajili ya wengine kwenye shule za serikali.

Hata mawaziri wetu wengi (kama sio wote) hawana watoto wanaosoma shule za serikali. Kutosomesha serikalini hakuna maana ya kutojali Elimu na Maendeleo ya Tanzania. Binafsi, sijawahi kutumia kodi ya Watanzania kusomesha watoto wangu, lakini naijali sana nchi yangu.

Serikali inadanganya sana kwenye takwimu. Nawashukuru Haki Elimu kwa kuangalia tofauti kati ya takwimu zinazotamkwa na matumizi yanayofanyika.

Hapa chini, nimeweka takwimu zilizotolewa na serikali. Zinadanganya mambo kadhaa. Kwa mfano, zinadanganya kwamba katika mwaka wa fedha wa 2006/2007, serikali ilitenga zaidi ya shlilingi bilioni mia tisa na nusu kwa ajili ya Elimu. Ukweli unaoonekana kwenye hotuba ya bajeti ya Mama Sitta ya 2006/07 na kwenye matamshi ya hapa na pale ya Msolla (bajeti speech yake ya 2006/07 haionekani angani) ni kwamba serikali ilitenga chini ya shilingi bilioni mia nne kwa ajili ya Elimu, kipindi hicho.
==============================

Education sector budget as per cent of total government budget: 1995/06-2006/07
Year Total Budget (mill.) Education budget (mill.)
1995/96--------500,116.00-------------6,504 (15.3%)
1996/97--------730,878.00------------ 92,631 (12.7%)
1997/98--------975,639.00------------ 102,343 (10.5%)
1998/99------- 927,732.00------------ 107,457 (11.6%)
1999/00------ 1,168,778.00----------- 138,583 (11.9%)
2000/01------ 1,307,214.00----------- 218,051 (16.7%)
2001/02------ 1,462,767.00----------- 323,864 (22.1%)
2002/03------ 2,106,291.00----------- 396,780 (18.8%)
2003/04------ 2,607,205.00----------- 487,729 (18.7%)
2004/05------ 3,347,538.00----------- 504,745 (15.1%)
2005/06------ 4,178,050.00----------- 669,537 (16.0%)
2006/07------ 4,850,588.00----------- 958,819 (19.8%)

Source: BEST 2006-2006, June 2006, p.89
 
Ila Augustine Nakubaliana na wewe ila wakale walisema ukitaka kujua Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze na kama ni hivyo Bwana Rakesh alitakiwa awe na experience hata ya Mtoto 1 ndani ya shule moja ya Manispaa.
 
Back
Top Bottom