Nani ananufaika na uwepo wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971?

Binti 1

Member
Dec 1, 2018
28
64
Ni miaka kadhaa imepita tangu mahakama kuu ifanye uamuzi wa kutaka serikali ibadili sheria ya ndoa ya mwaka 1971 Lakini mpaka leo serikali haifanya utekelezaji.

Pamoja na sababu nyingi za ndoa za utotoni, Lakini moja ya jambo linalochagiza uwepo wa ndoa nyingi za utotoni ni pamoja na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambao inaruhusu binti kuolewa kabla hajatimiza miaka 18 (kwa ruhusa ya mzazi).

Ndoa za utotoni zina athari nyingi, Na mojawapo ya athari hizo ni pamoja na wasichana kushindwa kupata haki ya Huduma za Afya za uzazi. Na hii inatokana na ukweli kwamba wasichana anakosa maamuzi juu ya miili yao baada ya kuolewa.

Bado najiuliza, Kwanini serikali hataki kupeleka bungeni mabadiliko ya hii sheria ili kuzuia wasichana kuolewa chini ya miaka 18?
Je, Nani ananufaika na uwepo wa hii sheria mpaka tusifanye marekebisho kama tulivyoelekezwa na mahakama?
 
Waziri Gwajima na serikali kwa ujumla, tafakarini kuhusu hili
 
Back
Top Bottom