Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,529
- 41,045
Nayakumbuka maneno ya Hayati Mwalimu Nyerere pale Chuo Kikuu cha DSM siku alipoalikwa na uongozi wa wanachuo.
Wakati ule kulitokea kipindupindu maeneo ya Mtwara. Serikali haikununua dawa kwa sababu haikuwa na hela. Hivyo serikali ikaagiza wananchi wazingatie usafi. Watu wakaendelea kufa na ugonjwa ukaendelea kuenea.
Wakati serikali ikidai haina pesa ya kununulia dawa kwaajili ya wagonjwa wa kipindupindu, lakini ikakubali ombi la wabunge la kutaka kuongezewa posho. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DSM waliandamana kupinga uamuzi wa serikali. Kilichofuatia ni baadhi ya wanachuo kutimuliwa kwa maelezo kuwa wanaipinga serikali.
Baadaye uongozi wa wanachuo walimwalika Mwalimu, na wakatumia nafasi hiyo kumwomba Mwalimu aruhusi wanachuo waliofukuzwa kurudi chuoni. Mwalimu akaridhia. Lakini akaeleza kuwa kuna wakati ukiwa kiongozi huambiwi yote kiufasaha. Halafu akasema yafuatayo:
"Vijana sula la HAKI, uchukulie wewe una kitu chako, unakipenda na kukithamini sana. Kitu hicho kinaitwa HAKI. Sasa siku moja, wakati umekishika hiki kitu chako cha thamani, akaja mtu mmoja, kwa nguvu akakupokonya, akaanza kukimbia nacho. Hapo una mawili, moja ni kusema, nimenyang'anywa, basi nitafanyaje. Ukaacha, na ukabaki ukiwa umepoteza hicho kitu chako cha thamani. Pili ukaamua kumfukuza. Wewe ukaamua kumfukza. Katika kumfukuza, yule aliyekunyang'anya akakimbia, mbele akaingia ndani ya nyumba, mlango akafunga. Hapo una machaguo mawili tena. Moja ni kuamua kuondoka, na ukawa umepoteza hicho kitu chako cha thamani. Uamuzi wa pili ni kuamua kuvunja mlango ili uingie ukichukue hicho kitu chako cha thamani kilichoporwa. Lakini unapoamua kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba, hujui yule aliyekunyang'anya atakuwa ana nini humo ndani. Vijana mtambue mnapopigania haki siyo rahisi yule aliyekudhulumu kukupatia haki yako kama huna ujasiri wa kuonesha kuwa hiyo ni haki yako na hupo tayari kuipoteza"
Uchaguzi wa serikali za mitaa umekuwa ni uthibitisho wa wazi kabisa wa kuwanyang'anya wananchi haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa. Na wanaowanyang'anya wananchi haki hiyo ni watu wadogo sana - watendaji wa vijiji na kata. Unajiuliza ni kwa kiwango gani Watanzania wamekuwa mazezeta hata kukubali katika uwingi wao, kunyang'anywa haki yao na mtu mmoja tu, mtu mwenye macho mawili, mikono miwili na miguu miwili. Wanaodhulumiwa wana macho mawili x idadi yao, miguu miwili x idadi yao, mikono miwili x idadi yao. Yaani wananchi mamia au maelefu wameshindwa kuvunja mlango wa nyumba ambayo mtendaji ameingia na bidhaa yao ya thamani kubwa inayoitwa HAKI! Jambo la kushangaza sana!
Hii ni sawa na yule mzungu aliyekuja Afrika (jina nimesahau) ambaye aliporudi kwao aliandika kuwa alifika dark continent akawakuta viumbe wanaokaribiana sana na binadamu (akimmanisha sisi watu weusi. Hakuamini kama tulikuwa binadamu). Baadaye alipolaumiwa kwa nini aliwaita watu weusi viumbe wanaofanana na binadamu wakati ni binadamu halisi, alijitetea kuwa, hakujua kabisa kama walikuwa wanadamu. Maana viumbe hao weusi mnaowaita ninyi kuwa nao ni wanadamu, niliwaona zaidi ya 150 walikuwa wamefungwa minyororo na Mwarabu mmoja mwenye gobore. Huyo Mwarabu aliwaswaga kama wanyama. Lakini huyu Mwarabu kuna wakati alichoka na kulala. Kuna wakati wakifika kwenye mto walimbeba juu ili kumvusha. Akasema, kama wangekuwa wanadamu, ana uhakika, kwa kushirikiana wasingeshindwa kummaliza yule Mwarabu mmoja kwa kupambana naye. Na hata kama angetumia gobore lake, labda angeweza kuwaua 1 hadi 5 lakini siyo wote. Pili wangeweza kumnyemelea wakati amelala na kummaliza. Au wakiwa wamebeba kumvusha kwenye mto wangeweza kumdondosha ndani ya maji na kummaliza, na wao wakawa huru. Kwa sababu walishindwa kufanya hayo yote, aliamini kabisa, kwa dhamira ya moyo wake wote, wale hawakuwa wanadamu.
Yale waliyoyafanya babu zetu wakati wa biashara ya utumwa, na sisi leo ndivyo tunavyofanya.
Mtu unajiuliza, hata hupati jibu. Inawezekana vipi mtendaji wa kijiji akimbie ofisi au agome kupokea fomu za wagombea, na wanachi katika umoja wao washindwe kumfurusha huyo mtendaji ambaye ni mmoja tu ambaye anataka kuchezea amani na haki za wananchi mamia? Kama wametushinda watendaji tu vijiji, tutawaweza wakurugenzi wa Wilaya mwakani?
Hata kwenye mataifa hayo tunayoyasifia kwa demokrasia na kuheshimu haki za wananchi wao, msidhani walizipokea haki hizo kwa hisani. Bali walizipambania, walizipigania, walijitolea kwa nguvu zao zote na kwa akili na maarifa yao yote kuhakikisha hakuna anayechezea au kuondoa haki zao.
Tunakosa kutimiza wajibu wetu wa kupigania haki zetu za msingi, halafu tunasema, 'MUNGU ATATENDA MUUJIZA'; Ni muujiza gani tunaoungojea toka kwa Mungu wetu? Muujiza mkuu Mungu aliishaufanya kwa mwanadamu - yaani kumwumba tofauti na viumbe vingine. Amempa akili, hekima, utashi na maarifa. Wewe huoni kama ni muujiza mkubwa kajitu kadogo lakini kanamwua tembo? Huoni ni mujiza mkubwa kajitu kadogo kasikoweza kubeba hata kilo 100 lakini kanatengeneza treni inayobeba tani zaidi ya 1,000?
Tusiache kutimiza wajibu wetu wa kuipigania na kuilinda haki yetu kwa maelezo kuwa eti tunasubiri muujiza wa Mungu. Kutotimiza wajibu ni dhambi. Mungu hujivunia watu jasiri na siyo waoga goigoi.
Na viongozi wa dini wasiwadanganye watu wakaamini kuwa uoga, uzembe na ugoigoi ni sehemu ya utakatifu. Mungu wetu ni jasiri, siyo Mungu wa waoga, aliliongoza Taifa lake katika vita mbalimbali na kushinda. Tunapopambana na udhalimu tunafanya kazi Takatifu, na tufanyapo tunatakiwa kumwomba Mungu ili aweke baraka katika yale tunayoyapigania.
Tumeyaona ya serikali za mitaa. Tunajua nini kitafanyika kwenye uchaguzi mkuu. Tushukuru kwa vile Mungu ametupa nafasi ya kujua nini kitafanyika 2020. Hivyo kisaikolojia tunatakiwa kujiweka tayari kuanzia sasa jinsi tutakavyopambana na watendaji wa kata na wakurugenzi watakaokuwa wakifunga ofisi kuzuia wasiowataka wasichukue au wasiudishe fomu. Tujue na tujiweke tayari namna ya kupambana na watendaji wa kata na wakurugenzi watakaoamua kuwaengua wagombea kwa hila. Hakuna haja ya hawa kusubiri kuwapeleka mahakamani maana wao wenyewe hawakutaka kuwapeleka wagombea kwenye mahakama ya umma ili umma uamue nani wanataka awe kiongozi wao.