Haki Hupiganiwa na Kulindwa, Haiombwi

Mtu akiwa anaongea yaliyoko moyoni usimpangie jinsi ya kuongea acha aongee tu usimzibe mdomo aongee apunguze machungu yake
Mtu aliye na uchungu moyoni huonge kweli yake ndio, ila mtu aliye na busara hawezi ongea lugha ya kuudhi ama matusi. Maana anajua kujielezea bila kumkwaza mtu.
 
Kwahiyo watu wakiongea lugha ya kukwaza dawa ni kuwateka na kuwapoteza?

Una uhakika gani na hicho unachokisema? Kila kitu hutengenezewa mazingira jaribu kutafuta uzi wa wa Iran kapost Habib (the bold) utajua ninachomaanisha. Si kila ovu ni mamlaka imetoa bali wengine hutafuta huruma ya wananchi.
 
Tatizo ni kuegemea upande wa sehemu mona nafikiri Kenya ni mfano mzuri kwako....
Kenya wana katiba ya wananchi ambayo inaipa mahakama nguvu na mamlaka halisi sio usanii usanii.
Pia unaona hata raisi Uhuru ana subira sana na kakubari kuongea na upinzani kumaliza matatizo yaliyopo.
Sasa kwetu katiba ya wananchi imewekwa pending kuna ile mapendekezo ya ccm ambayo nayo sijui yameishia wapi...
Na huo mfano wa kenya uliotoa hayo maandamano ni wapi walipoomba kibari?
 
Una uhakika gani na hicho unachokisema? Kila kitu hutengenezewa mazingira jaribu kutafuta uzi wa wa Iran kapost Habib (the bold) utajua ninachomaanisha. Si kila ovu ni mamlaka imetoa bali wengine hutafuta huruma ya wananchi.
Huruma gani ya wananchi wakati watu wanapotea?
So tundu lissu aliandaa watu wa kumpiga risasi?
Kama ndiyo mbona polisi hawajaweza kutueleza alivyotekereza mpango huo?
Kama siyo mbona mpaka leo hakuna ripoti ya polisi juu ya upelelezi waliofanya?
Jitahidi utateuliwa tu ila ongeza juhudi bado sana
 
Nikiteulkwa ntamuwknda na nikikushika utalia...
 
haya Bwana komaa hizo ideology zako kenya wamefilisika wameungana na upinzani ngoja na bongo tukifilisika tuone tutaelekea wapi
 
Warumi 13 : 1 - Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
Si wote ni wakristo humu. Maandiko kama haya unapotaka kuwakilisha humu jamvini kuna mambo mawili;

1- Kama ujumbe ni maalumu kwa watu wa dini fulani kuwa specific toka mwanzo.

2- Kama ni wa member wote humu fanya utafiti wa maandiko ya dini zote kabla hujaandika.
 
Nimeipenda hiyo Warumi japo hukunukuu maneno baada ya hapo ulipoishia inasema 'mamlaka husimamishwa na Mungu katika vyeo vyao vya kadiri'
Itaeleweka kuwa watawala wetu hawana kadiri, kama tunavyoshuhudia marufuku za mpaka mambo tuliyojikubalia katika katiba, ya kisiasa.
Ukifikiria utawala huu umeingia madarakani, na watu kwa kiasi kikubwa walitokea kuukubali. Sasa marufuku na kuanza kuminywa kwa haki kunachangiwa na nini, binafsi hata sielewi, mmeshashika dola, mnaogopa nini hasa?
Hilo andiko la Warumi linasema tuwape watawala wanachotaka. Wakitaka kodi, ushuru, woga wetu(hii nafikiri ndio wanaitaka zaidi, tuwaogope) tuwape ili tuishi kwa amani na upendo.
Neno linatutaka hivyo, ni ngumu kutekeleza.
 
Kuna vitu vimepangwa vitokee hata kama wewe hupendi. Yesu alipendwa na wengi kwa aliyokuwa akiyafanya na kuyasema, lakini kuna wachache hawakumpenda na hawakupenda alichokuwa akifanya na alichokua akikiongea. Hatimaye waliazimia kuandamana na kumkamata na walimpiga kama kibaka na aliuwawa.
Wapo ambao hawakupenda yaliyomtokea Yesu, lakini ilikuwa ni lazima yatokee yaliyotokea ili kutimiliza maandiko.
Tanzania hawamtaki huyo, na wanataka kuandamana wamtoe madarakani. Hata kama wewe hutaki kuna vitu hupangwa kutokea kwa lazima, ili kutimiza haja ya asili(nature). Hata akiuwawa ikiwa ndivyo ilibidi itokee, acha itokeee. Huwezi kuzuia kila kitu eti kwasababu wewe hupendi, wapo ambao hawakupenda Yesu auwawe, lakini kifo chake kilikuwa ni cha lazima, labda watu wanataka aondoke ili tuone ulazima huo, usizuie kila kitu kuna vitu havizuiliki.
Utashi wako au mapenzi yako hayana maana kwenye nguvu ya mungu, acha waandamane kitokee kilichopangwa kutokea.
 
Si wote ni wakristo humu. Maandiko kama haya unapotaka kuwakilisha humu jamvini kuna mambo mawili;

1- Kama ujumbe ni maalumu kwa watu wa dini fulani kuwa specific toka mwanzo.

2- Kama ni wa member wote humu fanya utafiti wa maandiko ya dini zote kabla hujaandika.

Huu ni kwa watu wote
 
Back
Top Bottom