Haki Hupiganiwa na Kulindwa, Haiombwi

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,950
2,000
Nayakumbuka maneno ya Hayati Mwalimu Nyerere pale Chuo Kikuu cha DSM siku alipoalikwa na uongozi wa wanachuo.

Wakati ule kulitokea kipindupindu maeneo ya Mtwara. Serikali haikununua dawa kwa sababu haikuwa na hela. Hivyo serikali ikaagiza wananchi wazingatie usafi. Watu wakaendelea kufa na ugonjwa ukaendelea kuenea.

Wakati serikali ikidai haina pesa ya kununulia dawa kwaajili ya wagonjwa wa kipindupindu, lakini ikakubali ombi la wabunge la kutaka kuongezewa posho. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DSM waliandamana kupinga uamuzi wa serikali. Kilichofuatia ni baadhi ya wanachuo kutimuliwa kwa maelezo kuwa wanaipinga serikali.

Baadaye uongozi wa wanachuo walimwalika Mwalimu, na wakatumia nafasi hiyo kumwomba Mwalimu aruhusi wanachuo waliofukuzwa kurudi chuoni. Mwalimu akaridhia. Lakini akaeleza kuwa kuna wakati ukiwa kiongozi huambiwi yote kiufasaha. Halafu akasema yafuatayo:

"Vijana sula la HAKI, uchukulie wewe una kitu chako, unakipenda na kukithamini sana. Kitu hicho kinaitwa HAKI. Sasa siku moja, wakati umekishika hiki kitu chako cha thamani, akaja mtu mmoja, kwa nguvu akakupokonya, akaanza kukimbia nacho. Hapo una mawili, moja ni kusema, nimenyang'anywa, basi nitafanyaje. Ukaacha, na ukabaki ukiwa umepoteza hicho kitu chako cha thamani. Pili ukaamua kumfukuza. Wewe ukaamua kumfukza. Katika kumfukuza, yule aliyekunyang'anya akakimbia, mbele akaingia ndani ya nyumba, mlango akafunga. Hapo una machaguo mawili tena. Moja ni kuamua kuondoka, na ukawa umepoteza hicho kitu chako cha thamani. Uamuzi wa pili ni kuamua kuvunja mlango ili uingie ukichukue hicho kitu chako cha thamani kilichoporwa. Lakini unapoamua kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba, hujui yule aliyekunyang'anya atakuwa ana nini humo ndani. Vijana mtambue mnapopigania haki siyo rahisi yule aliyekudhulumu kukupatia haki yako kama huna ujasiri wa kuonesha kuwa hiyo ni haki yako na hupo tayari kuipoteza"

Uchaguzi wa serikali za mitaa umekuwa ni uthibitisho wa wazi kabisa wa kuwanyang'anya wananchi haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa. Na wanaowanyang'anya wananchi haki hiyo ni watu wadogo sana - watendaji wa vijiji na kata. Unajiuliza ni kwa kiwango gani Watanzania wamekuwa mazezeta hata kukubali katika uwingi wao, kunyang'anywa haki yao na mtu mmoja tu, mtu mwenye macho mawili, mikono miwili na miguu miwili. Wanaodhulumiwa wana macho mawili x idadi yao, miguu miwili x idadi yao, mikono miwili x idadi yao. Yaani wananchi mamia au maelefu wameshindwa kuvunja mlango wa nyumba ambayo mtendaji ameingia na bidhaa yao ya thamani kubwa inayoitwa HAKI! Jambo la kushangaza sana!

Hii ni sawa na yule mzungu aliyekuja Afrika (jina nimesahau) ambaye aliporudi kwao aliandika kuwa alifika dark continent akawakuta viumbe wanaokaribiana sana na binadamu (akimmanisha sisi watu weusi. Hakuamini kama tulikuwa binadamu). Baadaye alipolaumiwa kwa nini aliwaita watu weusi viumbe wanaofanana na binadamu wakati ni binadamu halisi, alijitetea kuwa, hakujua kabisa kama walikuwa wanadamu. Maana viumbe hao weusi mnaowaita ninyi kuwa nao ni wanadamu, niliwaona zaidi ya 150 walikuwa wamefungwa minyororo na Mwarabu mmoja mwenye gobore. Huyo Mwarabu aliwaswaga kama wanyama. Lakini huyu Mwarabu kuna wakati alichoka na kulala. Kuna wakati wakifika kwenye mto walimbeba juu ili kumvusha. Akasema, kama wangekuwa wanadamu, ana uhakika, kwa kushirikiana wasingeshindwa kummaliza yule Mwarabu mmoja kwa kupambana naye. Na hata kama angetumia gobore lake, labda angeweza kuwaua 1 hadi 5 lakini siyo wote. Pili wangeweza kumnyemelea wakati amelala na kummaliza. Au wakiwa wamebeba kumvusha kwenye mto wangeweza kumdondosha ndani ya maji na kummaliza, na wao wakawa huru. Kwa sababu walishindwa kufanya hayo yote, aliamini kabisa, kwa dhamira ya moyo wake wote, wale hawakuwa wanadamu.

Yale waliyoyafanya babu zetu wakati wa biashara ya utumwa, na sisi leo ndivyo tunavyofanya.

Mtu unajiuliza, hata hupati jibu. Inawezekana vipi mtendaji wa kijiji akimbie ofisi au agome kupokea fomu za wagombea, na wanachi katika umoja wao washindwe kumfurusha huyo mtendaji ambaye ni mmoja tu ambaye anataka kuchezea amani na haki za wananchi mamia? Kama wametushinda watendaji tu vijiji, tutawaweza wakurugenzi wa Wilaya mwakani?

Hata kwenye mataifa hayo tunayoyasifia kwa demokrasia na kuheshimu haki za wananchi wao, msidhani walizipokea haki hizo kwa hisani. Bali walizipambania, walizipigania, walijitolea kwa nguvu zao zote na kwa akili na maarifa yao yote kuhakikisha hakuna anayechezea au kuondoa haki zao.

Tunakosa kutimiza wajibu wetu wa kupigania haki zetu za msingi, halafu tunasema, 'MUNGU ATATENDA MUUJIZA'; Ni muujiza gani tunaoungojea toka kwa Mungu wetu? Muujiza mkuu Mungu aliishaufanya kwa mwanadamu - yaani kumwumba tofauti na viumbe vingine. Amempa akili, hekima, utashi na maarifa. Wewe huoni kama ni muujiza mkubwa kajitu kadogo lakini kanamwua tembo? Huoni ni mujiza mkubwa kajitu kadogo kasikoweza kubeba hata kilo 100 lakini kanatengeneza treni inayobeba tani zaidi ya 1,000?

Tusiache kutimiza wajibu wetu wa kuipigania na kuilinda haki yetu kwa maelezo kuwa eti tunasubiri muujiza wa Mungu. Kutotimiza wajibu ni dhambi. Mungu hujivunia watu jasiri na siyo waoga goigoi.

Na viongozi wa dini wasiwadanganye watu wakaamini kuwa uoga, uzembe na ugoigoi ni sehemu ya utakatifu. Mungu wetu ni jasiri, siyo Mungu wa waoga, aliliongoza Taifa lake katika vita mbalimbali na kushinda. Tunapopambana na udhalimu tunafanya kazi Takatifu, na tufanyapo tunatakiwa kumwomba Mungu ili aweke baraka katika yale tunayoyapigania.

Tumeyaona ya serikali za mitaa. Tunajua nini kitafanyika kwenye uchaguzi mkuu. Tushukuru kwa vile Mungu ametupa nafasi ya kujua nini kitafanyika 2020. Hivyo kisaikolojia tunatakiwa kujiweka tayari kuanzia sasa jinsi tutakavyopambana na watendaji wa kata na wakurugenzi watakaokuwa wakifunga ofisi kuzuia wasiowataka wasichukue au wasiudishe fomu. Tujue na tujiweke tayari namna ya kupambana na watendaji wa kata na wakurugenzi watakaoamua kuwaengua wagombea kwa hila. Hakuna haja ya hawa kusubiri kuwapeleka mahakamani maana wao wenyewe hawakutaka kuwapeleka wagombea kwenye mahakama ya umma ili umma uamue nani wanataka awe kiongozi wao.
 

emrema

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
268
0
Nimeshuhudia siku ya jana ikitawaliwa na mapambano makali kati ya Polisi (Chombo cha dola) na wananchi ambao ni jamii ya watanzania waliotelekezwa kwa makusudi na Serikali walioipa dhamana ya kuwahudumia. Nikiwa mmoja wa wafanyakazi wa Chuo Kikuu nilipata usumbufu mkubwa kupita katika barabara ya kuingia kazini. Nilipata hasira sana.

Waziri mkuu anasimama bungeni na kudai maandamano yanakwamisha maendeleo anaonyesha upeo mdogo wa kujua kwa nini watu wanaandamana mfano wasomi wa chuo kikuu. Mishahara siku hizi kwa wafanyakazi hata wa vyuo vikuu inalipwa tarehe 5 hadi 10 hapa je si kupalilia maandamano zaidi?

Wanafunzi wamedai haki yao ya kuishi hawajapata na hata kupewa majibu ya kutia moyo.Nimeshuhudia mwanafunzi yupo ndani ya eneo la chuo anapigwa na polisi kama mwizi bila msaada wowote. Hebu fikiria yale tunayoyaona, mwanafunzi anaingia darasani nusu saa tu anaonyesha kuchoka na kusinzia sababu ya njaa hapo ni lecture ya masaa 2. Wewe mwalimu unaona zaidi ya nusu ya wanafunzi wapo kwenye hali hiyo, je unapata morali kweli ya kufundisha darasa kama hilo?

Wanafunzi wengi wanachelewa kuingia darasani sababu inabidi watembee kwa miguu kwa kukosa nauli. Wengi wanaomba misaada kwetu walimu je tutawasaidia wangapi na kwa muda gani? Kibaya zaidi tunawaletea polisi wawapige mabomu na mitama. Ndio hata sisi tulipigwa sana tu miaka hiyo ya 2000 ila je hakuna mbinu nyingine ya kudeal na hili. Nashauri Wanafunzi waendelee KUPIGANIA haki yao HAKI HAIOMBWI.

Wamachinga ni watanzania wenye haki ya kuishi, na hii inawezekana tu kwa kupata riziki, tunapowatoa kwa nguvu bila kuwaandaa wateja wao na wao pia si tunawanyima riziki. Wasingegoma kama mazingira yanaboreshwa. Mfano pale Mbeya waende wapi wakati eneo la muda walilopewa liteketa kwa moto? Nchi hii ni yetu wote si ya RC na vigogo tu. WAMACHINGA ENDELEENI KUDAI HAKI YENU.

Wasomi wenzangu hasa mlio vyuo vikuu UNAFIKI umezidi. Tumeona na tunaendelea kuona mateso kwa wanafunzi wetu hata sisi wenyewe maslahi yetu hayako sawa, lakini tumejiziba midomo sababu ya vibaraka wachache, tunajenga Taifa gani? Ndio maana wengi wanafikiria kuingia kwenye siasa kukimbia haya. WASOMI tutazame wasommi wa Kenya juzi tu wamegoma. Kama baba (WALIMU) ni mwoga watoto watakuwaje? .TUACHE UNAFIKI TUDAI HAKI ZETU ZIPO NA ZINAWEZEKANA.

Utabiri wangu kwa hali hii maandamano yataendelea na kuwa mabaya zaidi. Tukumbuke hata wananchi wa kawaida wameanza kutoogopa tena dola, wameanza kutojali kwenda rumande na hata gerezani HII NI HATARI. Wengi wanajua silaha japo dhaifu za kukabiliana na polisi. siku moja watavumbua silaha imara zaidi. Waziri mkuu atalalamika sana lakini dawa ni moja kufanyia kazi chanzo cha matatizo na sio matokeo.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Ikiwa Waalim ni waogo wanafunzi watakuwaje?, wewe saa ngapi ulikuwa kwenye foleni ya kushindwa kuingia ofisini? saa ngapi ulikuwa unamsikiliza Waziri Mkuu saa ngapi unaingia JF kufanya uchochezi?

Njia za kudai haki si maandamano, hii biashara ya machinga Mbeya, kama haijadhibitiwa na kuondolewa mabarabarani inakuwa ni kero kwa wenye maduka, kwani hawa wa machinga hupanga vitu vyao nje ya maduka ya watu, nnauhakika kuna tatizo na ufunbumzi wake ni kutengewa sehemu kamili za kufanyia biashara na nnauhakika hili walifanyiwa huko Mbeya.

Kuhusu wanafunzi kugoma, hili nalo limekuwa ni kawaida yao, na Serikali imejitia kitanzi kwa wema wake, pale ilipoamuwa kuwa kila mwanafunzi atakopeshwa, sasa wakigoma unashindwa hata kuwafukuza, utatowa wapi bajeti ya kuwapa wengine ukiwafukuza hao uliokwisha walipa? hapo sasa.

Mimi naona ingerudishwa vilevile, bajeti ya mwanafunzi itoke "serikalini" na wawe wanalipwa kwa mahudhurio yao na si kupewa kitita "in advance" ili watapogoma ndio watokomee na wapatiwe hiyo fursa wanafunzi wengine wasiodekadeka.
 

trachomatis

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
3,723
2,000
Naamini hakikuwa kichwa kimoja kilichokurupuka na kuanzisha HELSB.. Halafu adhabu ya kaburi aijuaye maiti. Usimshangae huyo lecturer kuongea namna. Na ukitaka kuujua uhondo wa ngoma uingie ucheze! Mi naona hizo huzielewi Faizafoxy. We unaelewa ile moja ya mwamba ngoma ngozi huvutia kwakee.....
 

lyimoc

Senior Member
Feb 20, 2011
140
0
Alie shiba hamjui mwenye njaa wewe ni gamba shika adabu yako watu wanatafuta riziki unasema wanasababisha msongamano we we ni mtu gani usiewajali wenzako
 

Leopold.Rweyemamu

New Member
Dec 31, 2015
2
45
Kwa yeyote ambaye amekuwa akiduatilia kauli zinazotolewa na serikaliya mapinduzi pamoja na CCM, juu ya majadiliano yanayo endelea kuhusu kufutwa na mwenyekiti wa ZEC uchaguzi mkuu uliopita upande wa tanzania visiwani.kinyume na sheria.

Bila shaka atakuwa amebaini ya kwamba mshindi kwenwa urais kwenye uchaguzi huo ndiye anaonekana kushika kwenye makali na waporaji wa ushindi wake kwenye mpini. Katika hali hiyo inaonekana dhahili mshindi badala ya kudai ushindi wake anaomba atendewe haki.

Hata kama huko mbele ya safari waporaji wake watamuonea huruma na kumtangaza mshindi uenda itakuwa ni kwa sharti la kutekeleza Ilani ya CCM na wala siyo ya chama chake.
 
Last edited by a moderator:

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,309
1,500
Ukawa mjifunze kudai haki. Vinginevyo mtaonewa sana na chama tawala. Huu sio uchochezi ni kwa mujibu wa katiba. Viongozi wa chama fulani wanatekwa na kuuwawa, halafu munaomba uchungu? Chama tawala yawezekana wanajua au hawajui, kwamba watu wanapotea na kuuwawa. Sawa dunia ni uwanja wa fujo lakini sio hizi fujo za kuuwana.

Tanzania ni nchi ya amani na najua CCM ni wahubiri wazuri wa amani na rais ni mpenda amani. Sidhani kama haya ya kutekana na kuuwana anayajua.

Naomba serikali ijitokeza wazi kujitoa kwenye haya matukio yanaotendwa na waahalifu kuteka wapinzani na kuwauwa au kuwaumiza. Hii sio itikadi ya chama tawala, na sidhani kama matendo haya yana faida kwa serikali na, taifa kwa ujumla. Inaonekana kuna watu wakereketwa aidha wa chama tawala wasiopenda upinzani kwa ushabiki na wanatumia madaraka yao vibaya kuchafua serikali na chama tawala ili vionekene vinauwa na kukandamiza demokrasia nchini. Naomba serekali ijiepushe na vitendi kama hivi na kuwaumbua hawa wa huni.

Serikali ya muheshimiwa Rais Magufuli ina mambo mengi ya kijamii yakufanya, na sidhani ina muda wa kuuwa au kuteka wapinzani.

Kama kuna wanachama pande zote kama wanafanya figisu za kuharibiana waache mara moja. Wanaochonganisha serikali na wananchi, waache mara moja. Serikali ijitokeze kwa kuwafichua hawa wasioipenda Tanzania, wanaendekeza umwagaji damu.
Mungu ibariki Tanzania na kuiepushia mbali na watu wanao taka kusambaza chuki ndani ya nchi nzuri kama hii. Taifa hili ni ya watanzania wote, na tuishi kwa kupendana na umoja.

Hitimisho: CCM au upizani pakiwa jambo lisilopendeza taifa, kuandamana ni haki ya kikatiba, na njia pekee ya amani ya kuonyesha kutofurahiashwa na tukio au jambo fulani.
 

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,309
1,500
Serikali inafahamu fika kwamba wapinzani wana hoja. Kuwapiga, na kuwakataza mikutano na kuandamana, niuoga wa chama tawala na serekali yake.

Kama unafanya vizuri, unaogopa nini kukosolewa?

Kwani lazima kila mmoja apende chama tawala au pinzani? Sio lazima, wananchi wapo huru to belong or not to belong to any political party.
 

kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,806
2,000
Ushaambiwa andamaneni mkione!! Utadaije haki kama hata kukutana huruhusiwi? Tec wamesema lkn wapi hawaeleweki...tusali tuu
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,291
2,000
Dawa ni kuandamana, bwana yule akiua halaiki ya watu huo utakuwa mwanzo wa mwisho wake.
 

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Siku tukijua kuwa machozi haYAleti haki bali mapambano.

Siku tukijua kuwa mtesi hana huruma.

Siku tukijua haki haiombwi ila inanyakuliwa.

Siku tukijua utekeleza wa katiba sio ombi bali ni lazima

Siku tukijua kodi ni mali za walipa kodi wananchi

Siku tukijua kuwa sisi ndio walinzi wa katiba.

Siku tukijua kuwa uhuru wa kuongea kukutana, kuandamana, kufanya mikutano na kuchagua tumpendaye ni takwa la Katiba.

Siku tukijua anayezuia haki za msingi za binadamu ni mhaini

Siku tukijua matumizi ya nguvu ni mauji.

Tukiyajua yote hayo: Tutasimama na kukataa uonevu, mauji utekaji, lugha za kebehi, matumizi mabovu ya kodi zetu kutumika kuuwa wananchi, haki ya kuchagua na tutalifumua jeshi la polisi usalama wa taifa na ikulu itaanza upya. - Sio risasi, polisi, jeshi wala amri zitaweza kutuzuia.
 

xav bero

JF-Expert Member
Nov 24, 2016
5,058
2,000
Usisahau na kutii sheria bila shuruti ni lazima
Siku ukijua kulipa kodi kwa kila raia ni lazima
Siku ikujua magu hajaribiwi mjaribu
 

Nktlogistics

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
2,157
2,000
...Tatizo katiba inasema : Ili uchaguliwe uwe kiongozi ni lazima ujue kusoma na kuandika . hata ukiwa wa standard seven unaweza kuwa mbunge na ukawatalawa wenye Masters. hii ni kwa Tanzania tu ulimwenguni kote.
 

Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Habari wana JF!

Leo nimekumbuka huu msemo "wanatafuta haki pasipo haki", sina hakika ni nani alisema lakini nakumbuka aliyesemema ni mwandisho aliyehamina Tanzania toka nchi za nje na vitabu vyake hutumika kufundishia mashuleni. Imekuwa muda mrefu hivyo sina kumbukumbu nzuri ni kitabu gani lakini hayo maneno mpaka leo nayakumbuka.

Sisi binadamu tuna hulka ya kujiona tupo juu ya kila kitu, hivyo kuna vingi tunafanya ilitupate kuonekana tuna nguvu.

Watu tulio katika daraja la chini tuna tabia ya kutafuta nguvu ambayo itatulinda mbeleni. Haijalishi ni kwa njia gani lakini kuna wakati tunahitaji kuwa na uweza wa kuamuru kitu fulani ili tupate kujilinda, kutoka kwa maadui au wasio maadui nikiwa na maana kitu chochote kinachoonyesha hatari ya kukwapua hiyo nguvu.


Hivyo katika kutafuta haki ya kumiliki hiyo nguvu inatupelekea kuitafuta pasipo haki. Yaani mtu hutafuta haki pasipo haki, mfano umeend kutibiwa hospitali badala ya kufata utaratibu utakuta mtu anatafuta njia ya panya ili apate matibabu angali kutibiwa ni haki yake. Lakini moja y kitu kinachopelekea mtu kutafuta haki pasipo haki ni uvumilivu hakuna.


Watu wako radhi wafanye maandamano angali kuna njia mbadala ya kufikisha mawazo yao na kusikia, wengine huenda mbali zaidi kutengeneza tatizo ili fulani aonekane mbaya ilikusudi apate huruma fulani kwa wanaomtazama wakati wangejua siri iliyopo moyoni ni mbwa mwitu.
Nchi nyingi zinazopelekea vita vya wao kwa wao ni matokeo ya ushauri mbaya wa watu wanaopatiwa ili kutimiza jambo fulani pasipo kujua wanatumika kujiua wenyewe. Mfano Iran kipindi cha nyuma na hata Libya ya sasa ni matokeo ya kutafuta hicho kitu kinachoitwa haki kukitafuta pasipo haki.

Mahali popote duniani Mungu alipotupa kumiliki kunautawala ambao unaongoza, na hivyo kila mamlaka iliyowekwa inapaswa kuheshimiwa "
Warumi 13 : 1 - Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
OneLink.To " hivyo kitu kila tunalotaka kufanya inatupasa kufikiri je! Ninachoenda kufanya ni sahihi? Hauwezi kwenda kupigana na ndugu zako kisa wewe tu unataka kupata haki pasipo haki.. Kama kunatatizo mahali toa tarifa ama njia mbadala ni nini kifanyike ili kuwezea kuelewana. Kama tatizo hakuna maji si sababu ya wewe kuitisha kijiji kizima kupeleka maandamano ili mpate maji bali itisha wingi huo mkajadili ni njia gani ya kufanya ili mpate maji, pengine ahadi itachelewa lakini si sababu ya wewe kwenda kuandamana. Kama hauna uvumilivu basi jitowe wewe kuwezesha maana popote palipo na mwanga huchanua.


Usijaribu kutafuta haki yako pasipo haki, maana kadri utavyozidi kuficha njia uliyotumia kupata haki ndivyo unavyozidi kufanya uovu. Jionye mikono yako palipo na haki.

Hauwezi kuwa huru kwa kuua nafsi ya mtu mwingine, pia uhuru tumepewa si kutumia kufanya vitu vyovyote bali tumepewa tutafakari lipi jema tutende na baya tuepuke.

Tafuta haki kwa njia sahihi sio njia ya panya.
 

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,992
2,000
Jinsi unavyomzingua paka ndivyo anazidi kukunja mkia....

Ukizuia kitu kisipunguze pressure ikizidi kitaripuka waacheni watu wawe huru kuongea inasaidia kupunguza machungu mbona JK alisemwa sana hadharan bungeni na majukwaani lakini alimaliza muda wake...

Muogope mtu asiyependa kuzungumza yaliyoko moyoni ni hatari kuliko anayezungumza...
 

Fernando Jr

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
2,080
2,000
Hivi kwanini mnatumia nguvu kubwa sana kuwatisha watu? Zingatieni katiba muwe na amani, la sivyo pressure na sukari hazitowabakisha.
 

Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
924
1,000
Jinsi unavyomzingua paka ndivyo anazidi kukunja mkia....
Ukizuia kitu kisipunguze pressure ikizidi kitaripuka waacheni watu wawe huru kuongea inasaidia kupunguza machungu mbona jk alisemwa sana hadharan bungeni na majukwaani lakini alimaliza muda wake...
Muogope mtu asiyependa kuzungumza yaliyoko moyoni ni hatari kuliko anayezungumza...

Hakuna anaye kufunga mdomo ila tu uongee kistaarabu si kwa jazba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom